Mwijage: Ndani ya miaka miwili tumejenga viwanda 3,006

Mwijage: Ndani ya miaka miwili tumejenga viwanda 3,006

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2014
Posts
1,488
Reaction score
2,762
​


Habari wakuu, katika kuelekea Tanzania ya viwanda waziri husika mh Charles Mwijage amesema ndani ya miaka 2 wamefanikiwa kujenga viwanda 3006..

Wakuu hebu tusaidiane kutaja hivyo viwanda ili tuvijue binafsi mimi sivifahamu

=====

Waziri Mwijage ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Mkutano huo ulikuwa wa kutoa taarifa ya maonyesho ya viwanda ambayo yataanza tarehe 7 hadi 11 Desemba.

Kaulimbiu ya maonyesho hayo ni 'Tanzania sasa tunajenga viwanda'.Pia kutakuwa na semina na mijadala mbalimbali.

Lengo lingine ni kutangaza masoko kwa bidhaa za kitanzania. Waziri Mwijage ameongeza kuwa Tanzania kila mwaka inanunua bidhaa jamii ya chakula zenye thamani ya bilioni 3 ambayo ni karibu asilimia 10 ya bajeti ya nchi yetu. Bidhaa tunazonunua sana kutoka nje ni maziwa, tomato sause, pilipili, maji ya dripu n.k

Waziri Mwijage ameshukuru sana washirika wao UNIDO kwa kuwaunga mkono katika maonyesho hayo.

​
 
Habar wakuu,Katika kuelekea Tz ya viwanda wazir husika mh Charles Mwijage amesema ndani ya miaka 2 wamefanikiwa kujenga viwanda 3006..

wakuu hembu tusaidiane kutaja hivyo viwanda ili tuvijue binafsi mm sivifahamu
kimoja wapo ni cha kwangu cha utiaji viraka suruali na chupi za watu. Maana nina cherahani 4.
 
ni vizuri wakati mwingine akitoa takwimu hizo wasaidizi wake waje watueleze zimeajili watumishi wangapi, zimechangia pato la taifa kwa kodi kwa kiasi gani hasa PAYE kwa mwaka, zimetengeneza ajira zingine zisizo rasmi kwa kiasi gani na jamii zimefaidika nini kwa hilo eneo angalau itakuwa imekaa sawa.
 
Habar wakuu,Katika kuelekea Tz ya viwanda wazir husika mh Charles Mwijage amesema ndani ya miaka 2 wamefanikiwa kujenga viwanda 3006..

wakuu hembu tusaidiane kutaja hivyo viwanda ili tuvijue binafsi mm sivifahamu
Hivi Mwijage aliwahi kuwa mchekeshaji wa TV ? Hivyo viwanda anavyosema vinatengeneza nini ikiwa toothpick zinaagizwa china ?
 
labda anazungumzia viwanja! atuambie vimefungwa vingapi na vilivyofunguliwa vimeajiri watu wangapi

Na kama mtu anajua kiwanda kilichofunguliwa ataje na mahali ilipo
 
Nashauri tu viwanda vipunguzwe kama kasi ni hii kufikia 2020 si vitakuwa 200000 na tunajua athari ya viwanda kuzalisha hewa ukaa.

Punguzeni kasi
Hali ya hewa itakuwa kama china na hatuwezi kuhimili huo uchafuzi
 
Hivyo viwanda ni vingi sana jamani!!
ndo maana labda umeme unasua sua
 
Viwanda 3000 na ushee! huu sasa ni 'uchochezi' viko wapi? vinafanya nini? nahisi vitakuwa vimeshushwa au kuota ila kujengwa huo ni UONGO ambao anatakiwa ashtakiwe kwa uchochezi.
 
Back
Top Bottom