PostGE2025 Mwigulu: Vurugu za Oktoba 29 zilipangwa ili kuharibu uchaguzi. Hakuna katiba inayopatikana kwa miezi sita

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema wanaharakati walijipanga kuhamasisha vurugu Oktoba 29, 2025 kwa lengo la kuharibu uchaguzi mkuu ili wasipatikane viongozi na kutoa nafasi ya maandamano ya kudai viongozi wapya kwa maandamano.

Akiongea na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Nchemba amesema kila anayedai haki anapaswa kujua wajibu wake badala ya kupelekeshwa na watu wasioipenda nchi yao na kuwagawa kwa maslahi ya watu wachache.
 
UKWELI DAIMA USEMWE. JARIBIO LA KWANZA NA LA MWISHO KATIKA TAIFA LETU . HATUWEZI RUHUSU MAPANDIKIZI YA MAPINDUZI . AMANI MILELE.
 
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema wanaharakati walijipanga kuhamasisha vurugu Oktoba 29, 2025 kwa lengo la kuharibu uchaguzi mkuu ili wasipatikane viongozi na kutoa nafasi ya maandamano ya kudai viongozi wapya kwa maandamano.

Akiongea na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Nchemba amesema kila anayedai haki anapaswa kujua wajibu wake badala ya kupelekeshwa na watu wasioipenda nchi yao na kuwagawa kwa maslahi ya watu wachache.
Walifanikiwa, hakukua na uchaguzi siku hiyo. Kilichotokea ni wasimamizi wa uchaguzi kujaza karatasi za kupigia kura kwa kumpigia kura mgombea WA CCM wa udiwani, ubunge na raisi.
Kwa kifupi NRNE ilifanikiwa sana!
 
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema wanaharakati walijipanga kuhamasisha vurugu Oktoba 29, 2025 kwa lengo la kuharibu uchaguzi mkuu ili wasipatikane viongozi na kutoa nafasi ya maandamano ya kudai viongozi wapya kwa maandamano.

Akiongea na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Nchemba amesema kila anayedai haki anapaswa kujua wajibu wake badala ya kupelekeshwa na watu wasioipenda nchi yao na kuwagawa kwa maslahi ya watu wachache.

Hivi hawa viongozi wanapataje madaraka makubwa hivi biala kuwa na exposure!!?

Aende tu hapo Namibia au Botswana ajifunze ni jinsi gani katiba bora inaweza kupatikana ndani ya miezi mitatu tu. Katiba ya Bostwana ilitengenezwa ndani ya miezi mitatu na ilishirikisha watu kama akina Sindwe Warioba na Mizengo Pinda.

Tatizo la maCCM hawana nia ya katiba mpya. Wanataka katiba kwa ajili ya maslahi yao tu.
 
Anaposema hakuna Katiba inayoweza kupatikana Kwa miezi sita anamaanisha nini?

Yeye kama waziri Mkuu hajui kuwa kwenye nchi yetu mpaka tulishawahi kuwa na bunge la Katiba?

Anawezaje kuongea kama vile madai ya Katiba mpya ni wazo jipya?
 
Ni dharau kwa sisi wana daresalama kuzungumza huo uharo wake hapa, he better shut up.
 
Ujinga MTUPU! kama katiba ya miezi 6 imeshindika waliona wapi ugumu kuahirisha uchaguzi mpaka hapo itakapokamilika? Kwa hiyo wakaona kheri waue maelfu ya watanzania?
 
Back
Top Bottom