Mwigulu Nchemba Utawaua bure Maafisa ktk Halmashauri mbalimbali hapa Nchini

Kwa hili nampongeza. Huwez kuamini mwezi huu fedha tarehe 19, tayari ishaingizwa moja kwa moja kutoka hazina na siyo utumishi tena! Hapa namkubali jamaa ni jembe. Hata hivyo nampongeza tu kama mtu neutral mwenye fikra huru na nitampongeza yeyote bila kujali ni wa mrengo gani. Big up mh Nchemba, kwa hapa nakupongeza.

Ahaaaaahaah!!Hvi huwa mnalipwa sh.ngapi na hawa mnaokesha mkiwasifia....eti tarehe 19 mshahara umeingizwa...umeingzwa kwako labda ila sisi tunaofanya kaz serikalini tunajua nini kinaendelea
 
Niliwahi kusema humu kuwa Mwigulu alitakiwa kujilaumu badala ya kujisifia kwa sababu utaratibu wa Mwezi Julai (baada ya kugundua makosa wameacha,utaratibu wa kawaida unaendelea) wa kulipa mishahara ulisababisha watumishi hewa au wasiostahili nao walipwe.
Lakini juzi tena amerudia kusema maneno ambayo nimegundua kuna mambo hayajui vizuri.Kwa mfano amesema kuanzia sasa malipo ya mishahara yatatoka hazina.mbona miaka yote yanatoka huko.pia alisema pesa ya miradi haitatolewa tena.naona hajui anachosema.pia ameongelea pesa inayotolewa kupitia mikoani kwenda wilayani. sikuelewa anaongelea pesa ipi.
Baada ya kusikia akiongea yote hayo bila utekelezaji wowote nimegundua hajapona ugonjwa wake wa kuropoka.nadhani anafikiri sisi watumishi wote wa umma ni chadema.
 
Watanzania tujifunze kuacha kumsifia mtu anaetekeleza majukumu yake.

Hapo angefanya "beyond" aliyiagizwa ndio tungemsifia, but kama ni "within " his job descriptions basi kawaida tu!!
tuna iq ndogo
 
Watanzania tujifunze kuacha kumsifia mtu anaetekeleza majukumu yake.

Hapo angefanya "beyond" aliyiagizwa ndio tungemsifia, but kama ni "within " his job descriptions basi kawaida tu!!

Kuna kila haja ya kumpongeza, ukisema ni within his job descriptions mbona mawaziri wa fedha waliopita hawakufanya ili au haikua kwenye job description zao? bado ameokoa billion 13 zingine hewa kwenye malimbikizo ya walimu, Kiukweli jamaa anastahili pongezi,Tujifunze kupongeza pâle panapostahili.
 
Lakini wadau mbona mnaigiza ushatani? kila kitu ni kupinga tu! nyie ni viumbe wa namna gani? kama mtu kafanya vizuri kwanini tusimpongeze kwa alilolifanya? hata baba anapotekeleza wajibu wake vizuri anapaswa kupongezwa na famili husika na majirani pia. Mwigulu kafanya vizuri kwanini tusimpongeze japo ni wajibu wake kweli; je ni viongozi wangapi wameshindwa kutekeleza wajibu wao? Hata Mbowe na Slaa huwa wanapongezwa pale wanapofanya vizuri kama wajibu wao. Sitaki kuamini kua upinzani ni ushetani. Tubadilike baadhi ya MAGAMBA wakifanya vizur tuwapongeze japo wanamapungu mengi.
 
kama amesaidia hicho kiasi cha bil 40 zigawanywe mishahara iongezeke... si ilikuwa inatumika bila kujulikana? sasaimejulikana basi iendelee kutumika ila kwa style ya kuwamitivate wafanyakazi...
 
Back
Top Bottom