Mwigulu Nchemba: Rais Yuko kazini, hakutani na Watendaji wa Kata kama Mwenyekiti wa Chama

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Anaandika Dr Mwigulu Nchemba

Bwana ZITTO, Elewa kuwa Rais Yuko kazini, Hajakutana na watendaji Kama mwenyekiti wa Chama. Hata angekutana kwa ajili ya UCHAGUZI kwa mtu mwenye akili timamu ungejua kuwa UCHAGUZI wowote huandaliwa na Serikali iliyoko MADARAKANI kwa kutumia watumishi wa UMMA.

1) CCM Ni Chama Cha Wakulima na Wafanyakazi wakiwepo watumishi, Hivyo watumishi wakikiunga mkono Chama na Chama kikawategemea sio dhambi. Vyama vingine havina kundi lolote la WATANZANIA vinategemea wakoloni.

2) Rais Hana haja ya kuwaelekeza Ma DSOs Na Ma RSOs kuiba kura kwa sababu kwa KAZI alizofanya kura tayari anazo, Shida yako ZITTO hata jimboni kwako hutembelei ujue kuwa kura anazo. Jimboni KWANGU Rais hata asipokuja kufanya Kampeni, Miradi ya maendeleo imeshampigia KAMPENI KURA ANAZO. HAYA MAMBO UNAYOTAKA KUIBA, KUELEKEZA, tunajua lengo Ni kuchafua na kuandaa visingizio.

USHINDI ITAKAOPATA CCM Serikali za Mitaa na USHINDI ATAKAOPATA RAIS MAGUFULI 2020 UTAKUWA WA KIHISTORIA AMBAO HAUJAWAHIPATIKANA. ITAKUWA CHAGUA MAGUFULI KAZI IENDELEEE.......
 
Kama kweli ameandika haya Mwigulu, uwezo wake wa kufikiria umeshuka sana na ana msongo mkali wa mawazo
Toka apate PHD ndo kawa mbumbumbu sana sijui hyo elimu kwa sasa imekuaje refer prof wa majalalani. Vizazi vitakavyokuja kuwasoma akina mwigulu vitakua na maswali mengi sana kuliko maswali yanayowahusu akina mangungo wa msovero na kinjekitile
 
USHINDI ITAKAOPATA CCM Serikali za Mitaa na USHINDI ATAKAOPATA RAIS MAGUFULI 2020 UTAKUWA WA KIHISTORIA AMBAO HAUJAWAHIPATIKANA. ITAKUWA CHAGUA MAGUFULI KAZI IENDELEEE.......
hawa mataahira wa lumumba hua wanaongea vitu kama maskhara vile kumbe wanamaanisha....
 
Back
Top Bottom