Mwigulu Nchemba: Nimeombwa kugombea Urais 2015

Mwigulu Nchemba: Nimeombwa kugombea Urais 2015

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,718
Reaction score
29,142
.Adai kutumiwa ujumbe na wazee kutoka Butiama
.Pia wapo vijana wa kutoka vyuo vikuu

mWIGULU-August18-2014.jpg


Wakati baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiendelea kupigana vikumbo kuwania urais wa 2015, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amesema ameombwa na watu mbalimbali wakiwamo wazee na wasomi kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo, Nchemba amesema kwa sasa hafikirii suala hilo kwani amebanwa na utekelezaji wa jukumu alilokabidhiwa na Rais.

Nchemba, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, aliyasema hayo jana wakati akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni nchini.
Alisema amekuwa akipokea ujumbe mwingi kutoka kwa wazee wa kijiji cha Butiama, mkoani Mara na kutoka kwa vijana wa vyuo vikuu wakimuomba awanie urais mwaka 2015, lakini suala hilo haliwekei umuhimu.

Badala yake, alisema anatekeleza jukumu kubwa alilopewa na Rais la Naibu Waziri wa Fedha.

Wakati Nchemba akitoa kauli hiyo, zipo taarifa kuwa aliwaalika makatibu wa CCM wa wilaya kutoka mikoa 11 kuhudhuria mkutano aliokuwa ameundaa jijini Mwanza siku ya Idd Mosi na Idd pili.

Pia mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa mkoa wa Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba, na mkutano mwingine wa ndani uliofanyika katika hoteli moja maarufu jijini Mwanza usiku, inadaiwa kwamba aliigharimia yeye.

Nchemba anadaiwa kulipia gharama za makatibu hao kutoka vituo vyao vya kazi kwa maana ya usafiri na posho.

Mbali na mkutano wa Mwanza, Nchemba anadaiwa kuwaalika tena makatibu wa CCM 51 mjini Dodoma wakati wa Bunge la Bajeti mwaka huu na kuwagharimia usafiri, posho na malazi.

Wakati akilipa gharama hizo, kwa miezi ya Juni na Julai, vyama vya siasa vilikuwa havijapewa ruzuku na kwa kiasi kikubwa watendaji wote wa CCM kama walivyo wa vyama vingine vya siasa, walikuwa hawajalipwa mishahara yao ya Juni na Julai.

Makatibu wa CCM wa mikoa na wilaya Tanzania Bara kimsingi wanawajibika kiutendaji kwa Nchemba kama Naibu Katibu Mkuu CCM Bara.

Hata hivyo, akizungumza na NIPASHE katika mahojiano kwa simu jana, alisema kimsingi kila kazi nzuri inayofanywa na kiongozi inawafanya watu waone ni harakati za kutaka urais 2015 japo ndiyo kipimo cha kuaminiwa.

"Nilichosema wakati nahojiwa na kituo cha televesheni nilisema sitangazi, lakini nafanya kazi niliyopewa ya Naibu Waziri wa Fedha hivyo lazima nihakikishe bajeti ya serikali inatekelezwa,"alisema.

Nchemba alisema yeye ni kiongozi wa chama anayepaswa kuwa mfano wa kuheshimu kanuni na taratibu za chama hivyo hawezi akakurupuka na kutangaza kwamba atawania urais.

"Mwanza nilifanya mkutano wa hadhara ambao msingi wake ilikuwa ni kusisitiza masuala ya kodi na ajira,"alisema.

Pia alisema hakulipia gharama za makatibu waliosafiri hadi Mwanza, kwa kuwa chama kina taratibu za kulipia watendaji wake gharama kama hizo.

Nchemba anakuwa kiongozi wa pili ndani ya CCM na serikali kutamka hadharani ama anautaka urais au anasukumwa na watu kujitokeza kuuwania mwaka 2015.

Mwingine ni Naibu Waziri wa Sayansi na Tekinolojia, January Makamba, ambaye alisema kwamba amekwisha kufanya kazi ya kujiandaa kwa asilimia 90 na kilichobaki ni kuonana na viongozi wa dini tu.

Wapo wanachama kadhaa ambao wameonyesha nia ya kutaka kuwania urais mwaka 2015 kupitia CCM.

Miongoni mwao ni mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.

Akizungumzia suala la ajira, Nchemba alisema kuna haja kwa wananchi kuachana na fikra kuwa ajira pekee ni ile ya kuajiriwa serikalini.

Alisema ili kukabiliana na tatizo la ajira nchini, halmashauri za wilaya na majiji zinatakiwa kuhakikisha zinapopima viwanja vya makazi, zinafanya hivyo kwa kutenga maeneo ya uwekezaji ambako kutajengwa viwanda vitakavyotoa ajira kwa vijana.

Alitaka kuwapo na muda maalum kwa mwekezaji anayepewa eneo la uwekezaji na anaposhindwa kuliendeleza, anyang'anywe na kupewa mwingine.

Alisema hilo litasaidia kuondokana na tatizo la baadhi ya wawekezaji kuhodhi maeneo ya uwekezaji na kushindwa kuyaendeleza kwa muda mrefu.

Nchemba alisema kumekuwa na tatizo la ukosefu wa uadilifu na bidii ya kufanya kazi kwa baadhi ya wananchi wanaopewa fursa ya kazi.

Alisema hali hiyo wakati mwingine inawafanya wawekezaji hususan nchini, kuchukua hatua ya kuajiri watu kutoka nje ya nchi.

"Kuna baadhi ya nchi kama Marekani, mfanyakazi anapokuwa kazini, haruhusiwi hata kuongea na simu au kusoma gazeti. Lakini hapa kwetu watu hawaonyeshi bidii ya kufanya kazi kwa lengo la kuongeza uzalishaji," alisema.

Chanzo: Nipashe

MAONI YANGU
JK ameufanya urais uonekane ni kazi rahisi sana ambayo hata mwendawazimu anaweza kufanya. Amesababisha kila mwanasiasa ajitangazie kuutaka urais. Tangu tupate uhuru mwaka 1961 hakuna kipindi ambacho watu wameutaka urais kuliko kipindi hiki cha JK. Mwaka ujao kuna hatari ya wabunge wengi kutorejea bungeni kwa kua wengi wao wanatamani kukalia kiti cha urais.

:israel:
 
JK amekula sana raha Ikulu nakujikusanyia utajiri mkubwa kiasi kwamba kila mtu anatamani awe km yeye.
Ila dhana ya Ikulu hakuna biashara aliondoka nayo Nyerere.
 
..inasikitisha.lakini ni heri ya mwigulu....ila hawa wengine duuh.
kinachomuharibia Mwigulu ni mcc mno.jamaa anajua ukweli ila anaigiza.
 
Hata wewe unaweza kugombea ukitaka ni haki yako ya kikatiba...kila mtu atatangaza nia ila rais atakuwa mmoja tu,,kwa iyo acha kukariri dunia imebadilika kama wewe hujiamini kaa kimya...!
 
Huyu nae n Dr Siku hizi! Akiwa presdaa wa nchi hii lazima itakuwa dictator , all in all atasubir sana
 
Hata utakwe na jamii yote ya Watanzania, lakini ukiwa ni mwanachama wa CCM basi matumaini yote ya Watanzania hufifishwa kama mshumaa uliotiwa moto...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kama Ngulu Chemba atakuwa rais waziri mkuu atakuwa nape Mnawie, na waziri wa fedha atakuwa Aden Rage
 
namuunga mkono dr mwigulu nchemba,yaani akitangaza nia nitamchukulia fomu kwa gharama zangu
 
MAONI YANGU
JK ameufanya urais uonekane ni kazi rahisi sana ambayo hata mwendawazimu anaweza kufanya. Amesababisha kila mwanahizaya ajitangazie kuutaka urais. Tangu tupate uhuru mwaka 1961 hakuna kipindi ambacho watu wameutaka urais kuliko kipindi hiki cha JK. Mwaka ujao kuna hatari ya wabunge wengi kutorejea bungeni kwa kua wengi wao wanatamani kukalia kiti cha urais.

:israel:

Ni kweli JK amefanya watu waone kuwa urais ni jambo raihisi kwa vile wanaangali mambo kama haya:
1. Kwa miaka 9 amejenga barabara mara mbili zaidi ya awamu zilizo tangulia.
2. Madaraja makubwa yalihitajika 5 yeye amejenga 3 kati ya hayo
3. Kwa miaka yake 9 Vyuo vikuu vimekuwa ni mara 4 zaidi ya alivyovikuta.
4. Amezalisha umeme mara mbili zaidi ya awamu zilizotangulia
5. Waliounganishiwa umeme ni mbili zaidi ya awamu zilizotangulia
6. Amepeleka umeme vijijini
7. Sekondari kila kata.
8. Amesogeza huduma za afya karibu wa wananchi
9. Pamoja na maajabu mengine kama
-Chuo kikubwa kuliko vyote EAC,
-Chuo cha Sayansi kikubwa kuliko vyote EAC,
-Barabara ya mabasi yaendayo haraka.
-Bomba la gesi
-Daraja la Kigamboni
-Katiba mpya
-Vitambulisho vya Taifa.
Kwa kasi hii 2015, kila mmoja anaona kumbe ni shughuli nyepesi kumbe JK ana kipaji cha pekee.

 
nakumbuka. mwigulu nchemba aliitisha kikao cha wana iramba dar wakaudhuria mke wake na watoto tu.sasa urais itakuweje?
 
Kwahiyo ile kamata kamata yake dhidi ya wale Wahindi kumbe ni moja ya kampeni zake za kujiaandaa kuusaka urahisi wa nchi hii!Hata Kikwete naye alianza kwa kuzikamata fedha za marehemu Malima kule nchini Uingereza,Wananchi wakasema "mkombozi si ndiyo huyu?",Angalia alipotufikisha kama taifa leo hii.Naona sinema ile ile inajirudia tena,ila safari hii ikiwa imefanyiwa remix kidogo.
 
Urais wa Tanzania umekuwa raisi mpaka vilaza wanatangaza nia? Nchemba tokea lini amekuwa Waziri?
 
Huyu nae n Dr Siku hizi! Akiwa presdaa wa nchi hii lazima itakuwa dictator , all in all atasubir sana

Hata nikiambiwa mwigulu ni prof. sitabisha kwa maana hata jk naye ni Dr, nchimbi naye ni Dr, mrema pia ni Dr. Hakuna taabu.
 
Bila kumung'unya maneno nasema Mwigulu Nchemba ni benevolent dikteta.(dikteta mwenye manufaa). Anatufaa wtz kwa kipindi hiki kuliko mwanaccm yeyote...........mwigulu anamajibu ya kisayansi ya changamoto za uchumi wetu bila hata kulalamika. Nani kati ya hawa anaweza kumsogelea mwigulu....Lowasa,membe,sitta(zee nafiki),wasira(zee lisilotaka mabadiliko), ngeleja (kijana mwenye harufu ya kifisadi),sumaye(zee lalamish), makamba(makamba(mtume wa baba yake).....!? Mwigulu ananishawishi kwa misimamo yake,anajua nini maana ya umasikini hawa wengine ni wasakatonge.
 
Huyu gaidi ameishakuwa waziri kamili wa fedha?? Heri ya Mwigulu ana ajenda zake za uraisi kuliko hao wengine kama Joka la Mdimu wanaotumwa na watu wengine kugombea kwa lengo la kutafuna nchi. Akipata hata kura 5,000 nchi nzima sio mwanzo mbaya
 
Ni kweli JK amefanya watu waone kuwa urais ni jambo raihisi kwa vile wanaangali mambo kama haya:
1. Kwa miaka 9 amejenga barabara mara mbili zaidi ya awamu zilizo tangulia.
2. Madaraja makubwa yalihitajika 5 yeye amejenga 3 kati ya hayo
3. Kwa miaka yake 9 Vyuo vikuu vimekuwa ni mara 4 zaidi ya alivyovikuta.
4. Amezalisha umeme mara mbili zaidi ya awamu zilizotangulia
5. Waliounganishiwa umeme ni mbili zaidi ya awamu zilizotangulia
6. Amepeleka umeme vijijini
7. Sekondari kila kata.
8. Amesogeza huduma za afya karibu wa wananchi
9. Pamoja na maajabu mengine kama
-Chuo kikubwa kuliko vyote EAC,
-Chuo cha Sayansi kikubwa kuliko vyote EAC,
-Barabara ya mabasi yaendayo haraka.
-Bomba la gesi
-Daraja la Kigamboni
-Katiba mpya
-Vitambulisho vya Taifa.
Kwa kasi hii 2015, kila mmoja anaona kumbe ni shughuli nyepesi kumbe JK ana kipaji cha pekee.


Mbona umesahau kuwa wajawazito wanalala wanne kitanda kimoja, watoto wanaokaa chini shule za msingi na sekondari kwa sasa ni wengi kuliko wakati wowote toka tupate Uhuru, mishahara ya watumishi wa umma ni kitendawili...
 
Ni kweli JK amefanya watu waone kuwa urais ni jambo raihisi kwa vile wanaangali mambo kama haya:
1. Kwa miaka 9 amejenga barabara mara mbili zaidi ya awamu zilizo tangulia.
2. Madaraja makubwa yalihitajika 5 yeye amejenga 3 kati ya hayo
3. Kwa miaka yake 9 Vyuo vikuu vimekuwa ni mara 4 zaidi ya alivyovikuta.
4. Amezalisha umeme mara mbili zaidi ya awamu zilizotangulia
5. Waliounganishiwa umeme ni mbili zaidi ya awamu zilizotangulia
6. Amepeleka umeme vijijini
7. Sekondari kila kata.
8. Amesogeza huduma za afya karibu wa wananchi
9. Pamoja na maajabu mengine kama
-Chuo kikubwa kuliko vyote EAC,
-Chuo cha Sayansi kikubwa kuliko vyote EAC,
-Barabara ya mabasi yaendayo haraka.
-Bomba la gesi
-Daraja la Kigamboni
-Katiba mpya
-Vitambulisho vya Taifa.
Kwa kasi hii 2015, kila mmoja anaona kumbe ni shughuli nyepesi kumbe JK ana kipaji cha pekee.

mkuu usiangaike na UKAWA.com, hawa wanataka Rais atakaye ruhusu gongo iuzwe kisheria, shangaa hawapo milembe tupo nao mtaani.
 
Back
Top Bottom