Mwigulu Nchemba ndani ya Tano bora CCM

Mwigulu Nchemba ndani ya Tano bora CCM

Robert PR

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2014
Posts
591
Reaction score
57
KUELEKEA 5 BORA NDANI YA CCM,GAZETI LA MWANANCHI LIMEFANYA UPEMBUZI YAKINIFU KWA KUNDI LA VIJANA AMBAO WANAWEZA PENYA 5 BORA.
MWIGULU ANAKWENDA TANO BORA.

Kundi la vijana limeweka changamoto kubwa kwenye ucha:guzi wa CCM mwaka huu, likiongozwa na makada kama January Makamba, William Ngeleja, Dk Mwele Malecela, Luhaga Mpina, Dk Hamisi Kigwangalla, Mwigulu Nchemba na Lazaro Nyalandu na baadhi ambao si maarufu na wengine hawana sifa zinazotakiwa kikatiba.

Nchemba ndiye anaongoza kwa kupewa nafasi katika kundi hili la vijana na kuna uwezekano akaingia tano bora. Alijiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara ili ajikite kwenye mbio hizo za urais.

Kwa kutumia nafasi yake, ameweza kujijenga ndani ya CCM huku misimamo yake wakati wa sakata la escrow, Bunge la Katiba na udhibiti wa matumizi ya Serikali vikimpatia umaarufu ndani ya chama hicho.

Pia, yupo January Makamba ambaye amekuwa mwandishi wa hotuba wa Rais kabla ya kugombea ubunge wa Jimbo la Bumbuli na baadaye kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Makamba ameeleza bayana kuwa CCM inahitaji fikra mpya na hivyo kutakiwa kuongozwa na kijana ambaye atafanya mageuzi. Lakini alianza kukosolewa mara tu alipotangaza nia, huku Rais Kikwete akieleza kushtushwa na taarifa hizo.

Dk Kigwangalla ni kijana mwingine mwenye kuthubutu, lakini wachambuzi wanasema muda wake kuwa kiongozi wa nchi bado haujafika, anahitaji kupikwa kwanza. Vivyo hivyo, kwa mbunge Luhaga Mpina ambaye kiukweli bado hajafahamika miongoni mwa wajumbe wengi ndani ya CCM.

Chanzo: Mwananchi
 
Hakuna namna mwigulu nchemba anafaa ni moja ya kijana mahiri na mtendaji anayeweza kuendana na kasi ya kizazi hiki.....
 
Mda bado jamani.
Acheni kupiga filimbi kisa mmekuja nazo uwanjani.
Mda si mrefu kipenga kitapulizwa na refa.
Tulieni.
Wote mtavua daruga tu hamna haraka
 
Wapatie maji ya dawa ....ORS na Flagyl yao ni Lowasa
 
KUELEKEA 5 BORA NDANI YA CCM,GAZETI LA MWANANCHI LIMEFANYA UPEMBUZI YAKINIFU KWA KUNDI LA VIJANA AMBAO WANAWEZA PENYA 5 BORA.
MWIGULU ANAKWENDA TANO BORA.

Chanzo: Mwananchi[/B]

Kundi la mteule mbadala

"Dk Magufuli, ambaye ameingia kwa mara ya kwanza kwenye mbio za urais, ndiye anayeweza kushangaza wengi iwapo atapitishwa na Kamati Kuu kwenda kupigiwa kura. Rekodi ya utendaji wake ni bayana na karibu mawaziri 10 waliochukua fomu wametumia ujenzi wa miundombinu ya usafiri kuwa ni mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne ambayo alihusika.

Dk Magufuli hana madoa ya ufisadi wala utendaji mbovu na daima amekuwa akionyesha unyenyekevu kwa Rais Kikwete kila alipozungumzia mafanikio ya wizara yake. Nguvu ya Kanda ya Ziwa ndani ya chama inamfanya awe na nafasi kubwa ya kupitishwa kugombea urais iwapo jina lake litapelekwa kwenye Mkutano Mkuu.

Ufinyu wa nafasi yake kuteuliwa ni pale Kamati Kuu itakapokata jina lake na kumweka mtu mwingine kutoka kanda yake"

Chanzo: Mwananchi.

Tano bora katika wezi, na matapeli?? Acheni ushabiki wa kipuuzi
 
Hakuna namna mwigulu nchemba anafaa ni moja ya kijana mahiri na mtendaji anayeweza kuendana na kasi ya kizazi hiki.....

Mwigulu Nchemba ni mwadilifu, mwaminifu, mwajibikaji na mzalendo wa kweli ndani ya Taifa letu.
 
Robert PR

Jamani huu uzi mbona hakuna mahali mwigulu ametajwa au mimi sioni?
 
Last edited by a moderator:
Jamani huu uzi mbona hakuna mahali mwigulu ametajwa au mimi sioni?

Kundi la Vijana

Kundi la vijana limeweka changamoto kubwa kwenye uchaguzi wa CCM mwaka huu, likiongozwa na makada kama January Makamba, William Ngeleja, Dk Mwele Malecela, Luhaga Mpina, Dk Hamisi Kigwangalla, Mwigulu Nchemba na Lazaro Nyalandu na baadhi ambao si maarufu na wengine hawana sifa zinazotakiwa kikatiba.

Nchemba ndiye anaongoza kwa kupewa nafasi katika kundi hili la vijana na kuna uwezekano akaingia tano bora. Alijiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara ili ajikite kwenye mbio hizo za urais.

Kwa kutumia nafasi yake, ameweza kujijenga ndani ya CCM huku misimamo yake wakati wa sakata la escrow, Bunge la Katiba na udhibiti wa matumizi ya Serikali vikimpatia umaarufu ndani ya chama hicho.

Pia, yupo January Makamba ambaye amekuwa mwandishi wa hotuba wa Rais kabla ya kugombea ubunge wa Jimbo la Bumbuli na baadaye kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Makamba ameeleza bayana kuwa CCM inahitaji fikra mpya na hivyo kutakiwa kuongozwa na kijana ambaye atafanya mageuzi. Lakini alianza kukosolewa mara tu alipotangaza nia, huku Rais Kikwete akieleza kushtushwa na taarifa hizo. Dk Kigwangalla ni kijana mwingine mwenye kuthubutu, lakini wachambuzi wanasema muda wake kuwa kiongozi wa nchi bado haujafika, anahitaji kupikwa kwanza. Vivyo hivyo, kwa mbunge Luhaga Mpina ambaye kiukweli bado hajafahamika miongoni mwa wajumbe wengi ndani ya CCM.

Mwananchi Leo
 
Promo tu hiyo! mtu hajawahi kuwa waziri kamili (ni naibu tena miezi michache tuu)apewe urahisi.utamlinganishaje mwigulu na Samwel Sita aliyeshika uwaziri kamili tangu enzi za mwalimu.

Kigwa hajawahi hata kupewa dhamana ya uwazi hata ya unaibu, hawezi kabidhiwa nchi.

January amewahi kuifanyia nchi hii kitu gani cha kihistoria na ajabu (unique) katika nchi hii???? MB 8 zilimshinda ataweza wananchi mil 40.after all hajawahi hata kuwa waziri kamili
 
Kwani Hayati Baba wa Taifa aliongoza Taifa hili akiwa na uzoefu upi!!!!
 
Back
Top Bottom