Mwigulu Nchemba, muombe radhi Rais!

Mwigulu Nchemba, muombe radhi Rais!

Huyo dogo naye kalewa madaraka tena mapema kabisa. hajui huyo kikwete ndo amemfikisha hapo alipo otherwise angekuwa kama akina kibajaji tu.

Mkuu Mwigulu Nchemba,leo hukuongea kauli nzuri kiutawala. Leo umemkosea heshima Rais wa Tanzania. Afadhali ungeishia kusema tu kuwa unatamani kuwa Rais wa Tanzania (lengo kuu la kila mwanasiasa wa Tanzania). Kusema kuwa unatamani kuwa Rais ili uwafunze watu adabu ni kumkosea heshima Rais wa nchi. Ina maana kuwa Rais anaongoza watanzania/wapinzani wasio na adabu?

Ina maana kuwa Rais wa Tanzania hana uwezo wa kuwashikisha/kuwafunza adabu wananchi wake na wapinzani wake? Hii si kauli ya kiuongozi na kiungwana. Ukiwa kama Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali inayoongozwa na Rais Kikwete, na kwa staha na ustaarabu wa kisiasa, ingawa umetamka maneno hayo Bungeni, huna budi kumuomba msamaha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na maneno yako au ya aina hiyo hayapaswi kurudiwa tena.
 
Kwa hiyo kakubaliana na mnyika kwamba ------ ni dhaifu
 
Mwigulu amemgundua kuwa rais ni dhaifu, lakini pia hajui kuwa kila kitu kinaongozwa na sheria za nchi

Huwezi kumfundisha adabu kiongozi mwenzako kama mtoto wako.
 
Mkuu Mwigulu Nchemba,leo hukuongea kauli nzuri kiutawala. Leo umemkosea heshima Rais wa Tanzania. Afadhali ungeishia kusema tu kuwa unatamani kuwa Rais wa Tanzania (lengo kuu la kila mwanasiasa wa Tanzania). Kusema kuwa unatamani kuwa Rais ili uwafunze watu adabu ni kumkosea heshima Rais wa nchi. Ina maana kuwa Rais anaongoza watanzania/wapinzani wasio na adabu?

Ina maana kuwa Rais wa Tanzania hana uwezo wa kuwashikisha/kuwafunza adabu wananchi wake na wapinzani wake? Hii si kauli ya kiuongozi na kiungwana. Ukiwa kama Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali inayoongozwa na Rais Kikwete, na kwa staha na ustaarabu wa kisiasa, ingawa umetamka maneno hayo Bungeni, huna budi kumuomba msamaha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na maneno yako au ya aina hiyo hayapaswi kurudiwa tena.

Udhaifu w JK una tupeleka pabaya sana watanzanis,kila kitu kinaenda kiudhaifu dhaifu tu.
 
Last edited by a moderator:
kwa ufupi Nchemba anakili kuwa haridhiki na uongozi wa jk, yahani jk ni dhaifu full stop. (rejea kauli ya J mnyika..rais ni dhaifu)
 
Mwigulu ana katabia kaajabu sana na ni mtu ambaye kwa uongozi wake atakuja kuwa ni dikteta na muuaji wa kutisha zzaidi ya akina sadam hussein.

Huongea kile anacho kiwaza na si kile anacho fikiria,huyu mwigulu siku c.c.m ikitoka madarakani atajinyonga.
Ni mimi.
 
Kwa sisi waelewa mwigulu amedhuhirisha kauli ya mnyika taasisi ya rais ni dhaifu ameshindwa kuongoza na anatamani aongoze yeye.
 
Pongezi kubwa kwa mwigulu ni kukubali kuwa anaongozwa na kiongozi dhaifu,ndiyo maana anatamani angekuwa yeye.
 
Uzuri alitamka hadharani na ridhiwani akiwepo,hivyo naamini ujumbe ulifika moja kwa moja kwa mlengwa wa magogoni.
 
-------- akishalewa madaraka hujikuta anaropoka ovyo ,na kujisahau kama yupo hapo kwa sababu ya mtu fulani,
Acha maisha yaendelee huko tuendako tutakujakuona nani ni mwanaume halisi.
 
Wapinzani nao wajithmini zaidi kwa kuangalia Muda uliobaki je,unatosha kuibomoa CCM kwa nguvu ya kususa vikao vya bajeti ambayo sio sheria au katiba isiyobadlilka kila mwaka?
Nakumbuka wakati Slaa akiwa bungeni alipata umaarufu mkubwa kwa hoja zake ndani ya bunge.
Ukweli ni kwamba CUF ina wabunge waliokomaa kisiasa kuliko Chadema na NCCR.
CCM watatawala daima kwa mtizamo huu wa wapinzani wasiotaka kujizatiti vijijni na kushirikiana na wananchi kwnye shughuli za maendeleo.
Mfano tu Tundu Lisu asiporudi jimboni kwke atapoteza lile jimbo.Wtanzania wana asili ya ujamaa kwa hiyo wakimuona mtu anakataa kushiriki kwenye kazi hata ya kuchimba msingi wa jengo la shile basi ujue huyo mtu hawezi kukubaliwa na wazee kijijini.
Chadema wanashindw kucheza na siasa za Tanzania zenye makindi makuu 6:
-Watu wa mjini
=Watu vijijini
-Watu wa dini
-Matajiri
-Maskini ambao ni mtaji wa kura
-Makabila yaliyoendelea dhidi ya makabila yaliyobaki nyuma(hawa ni walamba miguu ya viongozi)
Siasa za Mwigulu ni siasa za kijamaa na zinakubalika sana kwa wazaee wa zamani wanaoona kama uhuru umekua mkubwa sana na unatumika vibaya.

Naomba nikuhakikishie kwamba UPINZANI na hasa CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 watapaa maradufu na niku-tip tu kwamba watatawala Bunge hili na CCM watapata shida sana na hii CCM ya kijani ndiyo itakayoporomoka kama ambavyo imekuwa ikiporomoka mwaka hadi mwaka tangu mfumo wa vyama vingi uingie mwaka 1992!!.... Kwenye nafasi ya Urais hilo tujadilianeni

Hili linathibitika kwa sababu tangu uchaguzi mkuu wa kwanza wa mwaka 1995 CHADEMA haijawahi kushuka chini zaidi ya kupaa kwa umaarufu na kuongeza idadi ya wawakilishi katika vyombo vya maamuzi (wenyeviti wa vitongoji/mitaa,vijiji,madiwani na wabunge). Na tukukumbushe tu kuwa hata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 CHADEMA na UPINZANI kwa ujumla ulikuwa umeshinda viti vingi zaidi vya ubunge lakini CCM walitumia vyema mfumo wa kiserikali ambao ndani ndani yake imo National Electoral Commission unaowapendelea ku-minimize ushindi wa jamaa zetu hawa. Si hivyo tu hata kura za Urais na ushindi wa Kikwete wa CCM wa 61% ulikuwa wa Dr W.P. SLAA lakini kitu kiligeuzwa upside down!!..

Kwa hiyo nikuambie kitu kimoja tu kuwa Tundu Lissu atawagaragaza tena CCM kule jimboni kwake Singida Mashariki na tutakutana tena mwakani immeaditely baada ya uchaguzi mkuu hapo mwakani tukipeana taarifa!!
 
Mkuu Mwigulu Nchemba,leo hukuongea kauli nzuri kiutawala. Leo umemkosea heshima Rais wa Tanzania. Afadhali ungeishia kusema tu kuwa unatamani kuwa Rais wa Tanzania (lengo kuu la kila mwanasiasa wa Tanzania). Kusema kuwa unatamani kuwa Rais ili uwafunze watu adabu ni kumkosea heshima Rais wa nchi. Ina maana kuwa Rais anaongoza watanzania/wapinzani wasio na adabu?

Ina maana kuwa Rais wa Tanzania hana uwezo wa kuwashikisha/kuwafunza adabu wananchi wake na wapinzani wake? Hii si kauli ya kiuongozi na kiungwana. Ukiwa kama Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali inayoongozwa na Rais Kikwete, na kwa staha na ustaarabu wa kisiasa, ingawa umetamka maneno hayo Bungeni, huna budi kumuomba msamaha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na maneno yako au ya aina hiyo hayapaswi kurudiwa tena.
jamaa anafikiri inchi hii ni ya baba yake....................................
 
Back
Top Bottom