Mwigulu Nchemba, muombe radhi Rais!

Mwigulu Nchemba, muombe radhi Rais!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,143
Mkuu Mwigulu Nchemba,leo hukuongea kauli nzuri kiutawala. Leo umemkosea heshima Rais wa Tanzania. Afadhali ungeishia kusema tu kuwa unatamani kuwa Rais wa Tanzania (lengo kuu la kila mwanasiasa wa Tanzania). Kusema kuwa unatamani kuwa Rais ili uwafunze watu adabu ni kumkosea heshima Rais wa nchi. Ina maana kuwa Rais anaongoza watanzania/wapinzani wasio na adabu?

Ina maana kuwa Rais wa Tanzania hana uwezo wa kuwashikisha/kuwafunza adabu wananchi wake na wapinzani wake? Hii si kauli ya kiuongozi na kiungwana. Ukiwa kama Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali inayoongozwa na Rais Kikwete, na kwa staha na ustaarabu wa kisiasa, ingawa umetamka maneno hayo Bungeni, huna budi kumuomba msamaha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na maneno yako au ya aina hiyo hayapaswi kurudiwa tena.
 
Last edited by a moderator:
Hivi spika aliyasikia hayo?Hivi wabunge wajao watatuonaje watanzania wa leo?Kuna sababu ya wabunge waCCM kuwatukana wapinzani kila wakati?Hivi ningependa Mwigulu aulizwe,ukiwa MPINZANI ni sheria gani ya nchi umeivunja?Inasikitisha sana
 
Mkuu Mwigulu Nchemba,leo hukuongea kauli nzuri kiutawala. Leo umemkosea heshima Rais wa Tanzania. Afadhali ungeishia kusema tu kuwa unatamani kuwa Rais wa Tanzania (lengo kuu la kila mwanasiasa wa Tanzania). Kusema kuwa unatamani kuwa Rais ili uwafunze watu adabu ni kumkosea heshima Rais wa nchi. Ina maana kuwa Rais anaongoza watanzania/wapinzani wasio na adabu?

Ina maana kuwa Rais wa Tanzania hana uwezo wa kuwashikisha/kuwafunza adabu wananchi wake na wapinzani wake? Hii si kauli ya kiuongozi na kiungwana. Ukiwa kama Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali inayoongozwa na Rais Kikwete, na kwa staha na ustaarabu wa kisiasa, ingawa umetamka maneno hayo Bungeni, huna budi kumuomba msamaha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na maneno yako au ya aina hiyo hayapaswi kurudiwa tena.

Kuna sehemu umejijibu hapo, Rais anaongoza wapinzani wasio na adabu.
 
haya ndio matunda ya Mheshimiwa mwenyewe, acha avune alichopanda
 
Kila Rais ana haiba yake na utashi wake, Mwigulu kwa mtazamo wake anaona angekuwa Rais angewafunza adabu hawa wahuni, lakini Rais Kikwete hicho sio kipaumbele chake, na pia sio dhambi anavyowaacha tu, maana anaamini watafunzwa na ulimwengu. Kosa la Mwigulu liko wapi hapo?
 
Mkuu Mwigulu Nchemba,leo hukuongea kauli nzuri kiutawala. Leo umemkosea heshima Rais wa Tanzania. Afadhali ungeishia kusema tu kuwa unatamani kuwa Rais wa Tanzania (lengo kuu la kila mwanasiasa wa Tanzania). Kusema kuwa unatamani kuwa Rais ili uwafunze watu adabu ni kumkosea heshima Rais wa nchi. Ina maana kuwa Rais anaongoza watanzania/wapinzani wasio na adabu?

Ina maana kuwa Rais wa Tanzania hana uwezo wa kuwashikisha/kuwafunza adabu wananchi wake na wapinzani wake? Hii si kauli ya kiuongozi na kiungwana. Ukiwa kama Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali inayoongozwa na Rais Kikwete, na kwa staha na ustaarabu wa kisiasa, ingawa umetamka maneno hayo Bungeni, huna budi kumuomba msamaha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na maneno yako au ya aina hiyo hayapaswi kurudiwa tena.

Kuna sehemu umejijibu hapo, Rais anaongoza wapinzani wasio na adabu.

Wapinzani wanaweza kuwa hawana adabu kama tu wataangaliwa kwa jicho la CCM. Na kwa nini wawe na adabu kama wanafanya CCM hailali, kila kukicha viongozi wake wako barabarani kujieleza, mara kujitetea au kulalamika hadharani? Kwa nini waonekane wana adabu kama wanapinga yale ambayo yana maslahi ya CCM? kwa mtazamo huo, hawawezi kuwa na adabu asilani.

Lakini kauli kuwa rais anaongoza wapinzani wasio na adabu, nadhani kauli hii ina kasoro. Kwanza rais haongozi wapinzani. Hana ubavu huo , wala uwezo huo. Na nna uhakika anawaogopa kuliko hata ukoma. Na ndiyo maana kuna wakati aliwahi kutamka (kwenye kampeni za 2010) kuwa ni afadhali Dr.W.Slaa awe rais kuliko Tundu Lissu awe mmbunge! ....Kwa hiyo kumbe Slaa na Lissu ni tatizo kwake, ila afadhali ya Slaa kidogo...

Tukirudi kwenye kauli ya Mwigulu, kusema kuwa anatamani aongoze nchi hii ili awatie adabu wapinzani, hii ni kauli ya kipuuzi iliyojaa dharau, kiburi na kulewa madaraka. Ni kauli inayomdharau hata rais kuwa ameshindwa kazi ndiyo maana wapinzani wanajisikia wako peponi! Nadhani kwa maneno mengine anasema RAIS NI DHAIFU! Hiyo siyo kauli ya kumtoka mmbunge wa CCM hasa ikimhusu bosi wake. Ila kwa vile mle kuna watu wasiotaka kutumia vichwa vyao vizuri, sitashangaa kama hawatajua hata alisema nini.

Kwa upande mwingine nadhani alichokuwa anasema ni kuwa ule ushetani na mauaji aliyokuwa anayaratibu, anatafuta nafasi nzuri ya kuyafanya kwa mapana, hivyo anasubiria wakati ufike. 2015! Nadhani ana mbinu mpya zaidi ya tindikali, risasi na mabomu. Na hii ni kauli ya wazi ya kuvunja katiba na kukiuka demokrasia na siyo ya kuichekelea!
 
Hao wote wanaotaka kugombea urais wanautamani, mwigulu hana kosa lolote, ana haki ya kuutamani urais
 
Wapinzani nao wajithmini zaidi kwa kuangalia Muda uliobaki je,unatosha kuibomoa CCM kwa nguvu ya kususa vikao vya bajeti ambayo sio sheria au katiba isiyobadlilka kila mwaka?
Nakumbuka wakati Slaa akiwa bungeni alipata umaarufu mkubwa kwa hoja zake ndani ya bunge.
Ukweli ni kwamba CUF ina wabunge waliokomaa kisiasa kuliko Chadema na NCCR.
CCM watatawala daima kwa mtizamo huu wa wapinzani wasiotaka kujizatiti vijijni na kushirikiana na wananchi kwnye shughuli za maendeleo.
Mfano tu Tundu Lisu asiporudi jimboni kwke atapoteza lile jimbo.Wtanzania wana asili ya ujamaa kwa hiyo wakimuona mtu anakataa kushiriki kwenye kazi hata ya kuchimba msingi wa jengo la shile basi ujue huyo mtu hawezi kukubaliwa na wazee kijijini.
Chadema wanashindw kucheza na siasa za Tanzania zenye makindi makuu 6:
-Watu wa mjini
=Watu vijijini
-Watu wa dini
-Matajiri
-Maskini ambao ni mtaji wa kura
-Makabila yaliyoendelea dhidi ya makabila yaliyobaki nyuma(hawa ni walamba miguu ya viongozi)
Siasa za Mwigulu ni siasa za kijamaa na zinakubalika sana kwa wazaee wa zamani wanaoona kama uhuru umekua mkubwa sana na unatumika vibaya.
 
UNAJARIBU KUWA MWALIMU WA KUWAFUNDISHA WENDAWAZIMU!!!!!
utajipa shinikizo la moyo bure ndugu yangu. HAO WAJINGA WA UPINZANI mbona shughuli yao imekwisha. kinana anawapiga majukwaani..... akina MUHONGO wanawapiga bungeni. come 2015 hawa wajinga tutawachimbia kaburi
 
Hao wote wanaotaka kugombea urais wanautamani, mwigulu hana kosa lolote, ana haki ya kuutamani urais

Hujajibu hoja yoyote hapo, hoja sio kugombea, bali kauli ya Mwigulu yenye uelekeo wa kutorishwa na uongozi wa Rais ambaye ndiye mteuzi na Mwenyekiti wake.
 
weka dstv mkuu, huo muda mi nilikuwa namwangalia ERIC OMONDI kwenye Churchil Show
 
Upinzani kwani wamekosa adabu gani mpaka mwigulu aseme vile? Kwa vile wametoka nje au kuna lingine wamefanya?kutoka nje ya bunge ni kukosa adabu? hiyo si ndio njia ya kuonesha kutokubaliana na jambo? si ndivyo inavyofanyika ktk mabunge mengi duniani? in fact hawa wa kwetu ni wapole sanawenzetu mbona kuzipiga ni kawaida tu! au kuna lingine wamefanya?
 
Back
Top Bottom