Mwigulu Nchemba kiepuke kikombe hicho mapema vinginevyo jumba bovu linaenda kukuangukia wewe

Mmachinga wameadhiri sana biashara zinazolipa Kodi, kitambulisho cha 20,000 kimegeuzwa Chaka.
Imagine njia za kuingilia madukani kwa gari hazipitiki kwa namna biashara zilivyiwekwa barabarani
Duh mnataka muonge wakurugenzi muwafukuze machinga mjini. Aisee mtajua hamjuiii kwa kitakachotokea
 
JK m800/700 kwa mwezi na mfanyabiashara unapewa mpaka chai ukienda TRA. Halmashauri nazo zilikusanya pesa zake hazikwenda TRA. Zingechanganywa huenda ingekuwa 1.5T
JK alikusanya Bil.800 sio mil. Na hapo halmashuri zote zilikuwa zinajikusanyia zenyewe mapato yao yanabaki halmashauri husika.

Bwana yule kachukua pesa zoote hadi za halmashauri kapeleka hazina hadi pesa za NSSSF zoote hazina , kusanya hadi budget ya kupandisha mishahara watumishi peleka kule, kamata pesa za kuajiri watumishi zoote peleka kule , kamata pesa za wabadirisha fedha kamata zoote peleka kule , kamata wafanyabiasha wenye pesa mingi bank nyang'anya pesa zote peleka kule ,kamata pesa za wastaafu zoote peleka kule, kamata NssF Peleka kule, hahahaaa hakuna mtu kuleta fyoko fyoko wakati huo kazungukwa na mindege angani jummer, bomb detectors, mitutu ya mabunduki na silaha nzito nzito.

Halafu badae anajitokeza uraiani anajichekesha chekesha kwa wananchi alio wabatiza unyonge anagawa vi laki laki na vimilioni hahahaa halafu anamalizia kwa kudhalilisha watendaji wake wa chini mbele ya wanyonge basii wanyonge hao majuha wanafurahiiiii..

Eee ! MUNGU TANZANIA TISIPATE TENA RAIS WA AINA YA MAGUFULI KAMWE TUNAKUOMBA SANA.
 
Duh mnataka muonge wakurugenzi muwafukuze machinga mjini. Aisee mtajua hamjuiii kwa kitakachotokea
Hii ilijulikana kutoka mwanzo mwendazake , aliwatumia machinga kama ngao,
Lakini kumbuka mfanyabiashara anapoanguka machinga naye anazama mazima, hakuna machinga anaweza agiza kontena la nguo au electronics kutoka china.
 
Katika wizara zote wizara yenye kazi ngumu ni wizara ya fedha na Mipango

Mwigulu kazi anayo sio siri
Ni dhahiri mama amekuja na muelekeo wa kujenga nchi kwa kuwategemea WAHISANI.

Aingii akilini eti hata tukiyumba kwa miezi mitatu halafu tutapanda tena as if kila kitu kitabaki constant.
 
Hivi kufuata sheria na kanuni ni kubembelezana? Sikulijua hilo! Ndiyo maana watu wanaswekwa ndani bila kufuata sheria na kanuni kwa kuogopa kuonekana wanabembeleza watu! Kuna watu wanatandikwa viboko hadharani bila kufuata utaratibu, kumbe sababu ni hiyo! Ee Mola tunusuru!
 
Hivi mbona mnataka kutuuaminisha kwamba bila kutumia mabavu kodi haikusanywi??
Hivi wakati mnasoma huko vyuoni hamkujifunza njia bora za kukusanya kodi au ndo hivyo mnataka kuhalalisha upigaji wenu.
wameshazoea ile method ya kutumia force. na hapa JPM alifanikiwa kuwa brainwash watu.
wanaona haiwezekan wkt ni possible , just tu usimamiz mzuri unahitajika
 
Tanzania inaenda kushuhudia anguko kuu la makusanyo ya kodi ambalo limeruhusiwa kwa makusudi na kiongozi wa Nchi kisa eti kuwabembeleza wafanyabiashara.

Bila kuwa na maono mkuu wa Nchi amedai hata makusanyo yakipungua kwa miezi mitatu ama miwili halipo tatizo huku akitabiri makusanyo kupanda juu baada ya wakati huo wa mpito jambo ambalo kwa sera na uhalisia wa wafanyabiashara wetu ni vigumu kutimiza wajibu wao ki hiari.Na hapo ndipo anguko la Mwigulu Nchemba litapoanzia.

Ndugu yangu Mwigulu natambua wewe ni mtu wa fursa lakini kwa hilo anguko lijalo la makusanyo ya kodi litapelekea uangushiwe jumba BOVU huku ukilaumiwa umeshindwa kuisimamia mamlaka ya kukusanya kodi vyema na hapo utafutwa kazi.

Tafadhari,jiepushe na kikombe hicho mapema.

Kuna watu sijui waliumbwaje. Kuna watu huku walikuwa wanamtabiria utawala wa Magufuli anguko. Sasa na wewe unamtabiria mama anguko kama vile wewe si mtanzania. Si utoe ushauri tu wa kumsaidia Mwigulu jinsi ya kukusanya kodi. Acha kutabiria nchi mabaya. Wewe ni wa CCM lakini ninaona una chuki na mama kwa sababu umekosa kitumbua na kumwonea mwenzako wivu. Mtie mwenzako moyo kwa sabau hakuna kisichowezekana chini ya jua. Sheria za kodi zitafuatwa na asiyelipa kodi atabanwa tu. Si kama unavyofikiria wewe.
 
Ni dhahiri mama amekuja na muelekeo wa kujenga nchi kwa kuwategemea WAHISANI.

Aingii akilini eti hata tukiyumba kwa miezi mitatu halafu tutapanda tena as if kila kitu kitabaki constant.
mama hajasema tutawategemea wahisani. ni kodi zikusanywe kwa sheria. not by extreme force mpaka kuua biashara na kukimbiza wawekezaji.

sasa mnalaum sana? mna njia bora mbadala ya kukusanya kodi?
 
Kodi itakusanywa kihalali na kwa mujibu wa sheria.

Makusanyo yakipungua ndio uhalisia wenyewe!
kivipi mkuu, acha kuota ndoto. Fedha za mishahara, fedha za mikopo ya wanafunzi, fedha za kulipa mishahara, zitapatikana kwa njia gani? Ukinijibu hili swali basi nakuunga mkono
 
kivipi mkuu, acha kuota ndoto. Fedha za mishahara, fedha za mikopo ya wanafunzi, fedha za kulipa mishahara, zitapatikana kwa njia gani? Ukinijibu hili swali basi nakuunga mkono
Kwani kwa sasa zinapatikana kwa njia gani?

Unadhani unaweza kukusanya kodi kwa kutumia nguvu hadi lini?
 
Tanzania inaenda kushuhudia anguko kuu la makusanyo ya kodi ambalo limeruhusiwa kwa makusudi na kiongozi wa Nchi kisa eti kuwabembeleza wafanyabiashara.

Bila kuwa na maono mkuu wa Nchi amedai hata makusanyo yakipungua kwa miezi mitatu ama miwili halipo tatizo huku akitabiri makusanyo kupanda juu baada ya wakati huo wa mpito jambo ambalo kwa sera na uhalisia wa wafanyabiashara wetu ni vigumu kutimiza wajibu wao ki hiari.Na hapo ndipo anguko la Mwigulu Nchemba litapoanzia.

Ndugu yangu Mwigulu natambua wewe ni mtu wa fursa lakini kwa hilo anguko lijalo la makusanyo ya kodi litapelekea uangushiwe jumba BOVU huku ukilaumiwa umeshindwa kuisimamia mamlaka ya kukusanya kodi vyema na hapo utafutwa kazi.

Tafadhari,jiepushe na kikombe hicho mapema.

Ajiamini Kiutendaji, ila awe mwangalifu.
 
Mku sidhani kama itakuwa hivyo kwani Mzee Mwinyi aliweza kipindi hicho ambacho wafanyabiashara walikuwa wachache sana itakuwa leo ambapo nchi kibao zinategemea Tanzania kibiashara .
Mimi sio mchumi ila sijui kama itashindikana
Kwa Nini nyie mnawatetemekea Sana wachumi? Wachumi ni watu wa kawaida sana. Tena siku hizi wachumi wengi ni vilaza. Unakuta mtu hajui hata differentiation na yeye anajiita mchumi. Wengi wao wamesoma hge halafu wanajiita wachumi hata hesabu hawajui.
 
Mmachinga wameadhiri sana biashara zinazolipa Kodi, kitambulisho cha 20,000 kimegeuzwa Chaka.
Imagine njia za kuingilia madukani kwa gari hazipitiki kwa namna biashara zilivyiwekwa barabarani
Ni rahisi tu...chukueni hatua za kuwaondoa wamachinga barabarani
 
Kodi itakusanywa kihalali na kwa mujibu wa sheria.

Makusanyo yakipungua ndio uhalisia wenyewe!
Kuna uhakika wa kinachokusanywa saivi hakiko halali? Kodi inakusanywa kwa mujibu wa sheria,basi nchi hii ina wazimu!

Ukiacha swala la kesi za uhujumu uchumi ambalo kiukweli linahitaji kuangaziwa kiasi,ingawa na lenyewe linatawaliwa kisheria, kutumia task force pia si jambo jema kiukweli lakini hivi kweli hatujui vijana wa tra walivyokuwa wamebobea kwa rushwa?

Tuna ITA, Tax administration act, VAT act,Finance act za kila mwaka wa fedha n.k kweli kodi gani inakusanywa isivyo halali? Filling za returns ziko clear,
Nini kikubwa kimebadilika from 2015 kwa mzee kikwete kwenye maboresho na marekebisho ya kodi ambayo kwa sasa tunaona kodi inakusanywa isivyo halali??

Kwa mfano,, property tax ukusanyaji wake ni maajabu,,wangapi wanalipa na wangapi hawalipi?
Kwa VAT mara ngapi tunanunua vitu na mfanyabiashara anadanganya kuwa mashine ni mbovu haiwezi print receipt? Wangapi wanadai receipt baada ya manunuzi au mtu anapewa receipt yenye kiasi kidogo ya kusafirishia mzigo,, hivi lini business people asiwaze faida kubwa? Kiuhalisia hii hela si ya MFANYABIASHARA ni ya serikali maana mnunuzi ameilipa lakini mfanyabiashara anainyonga! AJABU SANA HILI TAIFA

What about Tanzanian employees??? wao ndio waelemewe siku zote?

Hapa ni kujilisha upepo tu,,watu waje na mabadiliko kwenye sheria yaliyotokea since 2015 si yapo,,tuchambue hizi zinazolalamikiwa...

Tax personel nchi hii ni wa AJABU sana..
 
Kodi itakusanywa kihalali na kwa mujibu wa sheria.

Makusanyo yakipungua ndio uhalisia wenyewe!
Well said. Unajua kuna watu bado wako katika usingizi wa pono, hawataki kubadilika lakini wakati utawabadilisha tu. Umesema vizuri na kweli kabisa, kama makusanyo yatapungua, lakini ni makusanyo halali kwa mujibu wa sheria, na hakuna vitisho mpaka vya watu kufunga biashara zao, basi hayo ndio yatakuwa makusanyo halali yasiyo ya dhuluma. Hoja ya Rais Samia iko clear kabisa katika hili. kwamba TRA wafanye kazi zao kiweledi, kwa maana ya kukusanya kodi katika utaratibu ambao utawafanya hata kesho waikusanye kodi wanayoikusanya leo. Wafanye kazi zao kibiashara na sio kibabe, watengeneze mahusiano na wafanyabiashara, waongeze vyanzo vya kodi, nakadhalika. Kama mazingira yatafanywa kuwa rafiki, kwanini wafanya biashara wasilipe kodi? Kwanza, kama TRA wakisimamia kwa haki ile sheria inayotaka mfanyabiashara ili apate leseni msimu unaofuata lazima awe na Tax clearance, wafanyabishara watakwepaje kodi? Tatizo ni uadilifu wa maofisa wa TRA, ni mambo ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi!
 
Siku akili zikikaa sawa atakuja gundua

Gharama za mishahara kwa mwezi ni
700 billion

Debt interest ni 800 billion kwa mwezi

Miradi mikubwa inayoendelea serikali inatakiwa ichangie 400 bn kwa mwezi

Not long atabaini, makusanyo ya kodi ayatoshi ku cover budgeting plan.

Akitaka kukopa mabeberu yanamwambia nope. Magufuli alikuwa anakopeshwa kirahisi kwa sababu wanajua anaweza lipa na hela yao kwa asilimia kubwa inafika kwenye intended project. Amuulize JK kama kukopesheka ni rahisi.

Wafanyakazi na wanafunzi ambao sasa hivi washaanza kusahau habari ya mishahara na boom kuchelewa soon vilio vitaanza.

Ala kumbe kazi yenyewe ya uraisi ni ngumu kuliko.

Mama hayuko serious ☝️it’s coming make no mistake.
 
Back
Top Bottom