Elections 2015 Mwigulu Nchemba: Huu Unyama Una baraka zote za Dr. Slaa na genge lake

Nchhemba vipi hiyo bisibisi uliyotumia ni zaidi ya mabomu ya Arusha. nakuonea huruma una miaka miwili ya kupumua katika nchi hii, ngoja lowasa aje akuonyeshe kazi na huyo kijana wa bwana mkubwa wamasemi tela
 
Bora al-shabab kuliko chadema

Laiti ungejua mipango ya sisiemu ilivyo usinge thubutu kuandika haya.......in short sisiemu wamejiandaa kuua watu hapa siongei kishabiki Mungu anaona haya ninayo andika hapa ila Mungu ata dili na nyie perpendicularly mpaka mnyooke
 
Kumuita binadamu mwezio kinyago, kisa tu amemwagiwa tindikali na CHADEMA ni uzandiki usiosemeka!

Tena wewe unaonekana unaelewa vizuri hila zote zinazofanywa na sisiemu nakuhakikishia Mungu alie umba hii dunia hatokaa kimya
 
Tumuelewe vp huyu binadamu mwenzetu!,Huyu aliyekatiwa ADABU(musa) na vijana wake amezunguka nae peke yake kwenye chaguzi mbalimbali hajaambulia kitu ndo kwaanza watu wanamkimbia!,Akaona sio inshu! Akatangaza zabuni kwa wahuni wake! tena awamu hii wakamkamata mtu wao tena nakumtia ADABU as usually! Wakamtia bisibisi ya jicho duuuh! Wakampelekea tena! Sasa wapo wawili anazunguka nao huko kalenga! Ofu yangu akishindwa tena kama Arumeru na sehemu nyingine ataongeza mwingine! Ndioo! Kwani si anawatangazia zabuni tu wahuni wake walewale wanaingia mzigoni! Ili aongezewe mwingine aende nae Chalinze! Sijui huyu atatiwaje ADABU! Tusipomkemea huyu kiumbe nahiso ataendelea na mradi wake huu na hatimaye siku moja tutakuja kumshuhudia anatembea na fuso ya vilema na kuzunguka nao kila sehemu! Ndioo! Badala ya kuzunguka na Ilani ya chama chake! Yeye ameamua kubeba vilema ambao chanzo cha ulemavu wao ni kizungumkuti! Labda mi kama binadamu mwenzao niwashauri tu hawa vijana wa "KIJANI GUARD" kuwa waangaliane inawezekana kuna A na B.Wasavimbi na Wan..pe.Siinajulikana hawa hawakai chungu kimoja!? Sivyo watatafunana wenyewe hadi mutabaki vilema karibu wote! Huku mukiendelea na kulaghaiwa kuwa jirani yenu ndie mchawi kumbe wenyewe huko ndani.Hivi kama kweli ingelikuwa munafanyiwa ubaya huo na hao munaoaminishwa kila siku vyombo vya dola vingeshindwa kuwakamata?,Kuna tofauti gani kati ya wauaji na wauzaji wa meno ya tembo wanaofahamika ila hawakamatwi na ikitokea kukamatwa ni feki! Na hao wahalifu wanaowapa vilema nyie na hawakamatwi na ikitokea kukamatwa ni feki? kuna tofauti gani kati ya nyie wenzenu wanaouwawa au kupata vilema ktk mikutano ya cdm? "MUANGALIENI ANAYELIA SANA MSIBANI KULIKO MFIWA" Hivi kweli nyie munaamini kabisa kuwa savimbi anahisi uchungu sana zidi ya ulemavu wenu kuliko nyie wenyewe?!.Kusoma hamujui hata picha hamuoni? Tuambieni tu basi kama mumejitolea kuuza utu au viungo vyenu ili kukidhi njaa yenu tujue! Hivi nyie Kijani guard labda niwaulize ndg,jamaa na marafiki zenu wote wapo kwenye chama chenu tu? Hivi nikweli amuna ndg,jamaa na marafiki zenu kwenye vyama vingine? Hivi huko majumbani kwenu munakoishi mtu wa chama tofauti na chenu akipatwa na tatizo,kuugua au kifo amuzikani? Ndioo! Sasa badala ya kuyajibu hayo niwakumbushe muulizeni savimbi kwanini alikimbia pale Arusha bila hata kwenda kuwapa pole waathorika wa mabomu pale sow..to? Wakati kila siku anasimama mbele yenu na kuhubiri kuwa siasa si uadui bali ni kushindanisha sera! Hivi hiyo ya kutowapa hata pole wale waathirika na wafiwa pale sow..to ndo miongoni mwa sera iliyomo kwenye ilani ya chama chake?.Mwisho kabisa kabla sijasahau niwakumbushe Shonzo na Mwampambe kuwa sasahv ili wauzike kwenye jukwaa atakalohutubia savimbi wanatakiwa eidha wajigonge wenyewe nyundo hata kwenye meno au wakishindwa wawatafute wale wahuni wa savimbi wawatwange hadi meno hasa ya mbele yang'oke! Na baada ya hapo nawahakikishia mutaitwa na mutatumiwa ticket za ndege faster hata kesho asubuhi muende kwenye kampeni Kalenga! Ila mukikaa hivyo kama baba au bibi harusi hamutakaribia kwenye jukwaa la savimbi tena kamwee!.Mara nikaamka.
 
Kwa unyama walioufanya na wanaoendelea kuufanya Mh. Mbowe na Dr. Slaa, siku ya hukumu Mungu atawatengea moto maalumu kwaajili yao.
Uzuri wa MUNGU ni kwamba anasema kwa HAKI atahukumu wanadamu.Na hata Mwigulu atahukumiwa kwa haki kama anasema Uongo Maana angekuwa mkweli na mpenda Mungu na Mpenda haki Angeeleza na kifo cha DAUD MWANGOSI kauawa na Serikali yake.
 
Ha ha ha ha ha CCM walichelewa kuzindua kampeni zao kumbe walikuwa hawajakamilisha maandalizi ya kuwaandaa misukule yao ya kuzunguka nayo kwenye kampeni.Wakawachukue na wale mabinti wa kingereza waliomwagiwa tindikali Zanzibar pamoja na mapadri wote na mashekhe waliomwagiwa tindikali wazunguke nao kwenye kampeni waendelee kusema kuwa walimwagiwa tindikali na CHADEMA.

Hawa ccm ndio mafya hata Dr Ulimboka walimpiga wao leo hii hata huduma za afya zimekufa nchini mbona hawajamkamata yoyote apelekwe mahakamani wananchi fanyeni mageuzi mali za nchi zinaibwa hadi Ulaya wanatuonea huruma
 
Wapeni Ccm waendele kupora mali za nchi hali wananchj wameachwa kwenyd umasikini mkubwa.hata gesi ya Mtwara hakuna ufafanuzi mkubwa umetolewa chadema toeni ufafanuzi kuhusu mali za taifa zitawasaidiaje wananchi
 
1622176_673540786041329_124503048_n.jpg
1780655_673540839374657_1516800168_n.jpg
1902026_673540866041321_296530695_n.jpg

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Ifakara wakati wa Mkutano wa Kufungua Kampeni uliofanyika Jana Tar.27/02/2014.Hapa akiwa na Wahanga wa siasa chafu zinazodaiwa Kufanywa na Chadema kupitia Vijana wake wa Redbrigade.Mwenye T-shirt ya Njano ni Mzee Alphonce John ambaye alitopolewa Macho kwa dispisi wakati wa Uchaguzi wa Udiwani huko Kahama Mwezi uliopita.

Mwigine mwenye Shati la Kijana ni Kijana Musa Tesha ambaye alimwagiwa Tindikali na Vijana wanaodaiwa Kuwa wa Chadema huko Igunga wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo.Mh:Mwigulu Nchemba jana amesisitiza Wananchi wa Kalenga kuwa makini na siasa Chafu za Chadema zinazofanywa sehemu mbalimbali hasa kwenye nyakati kama hizi za Uchaguzi.Amesisitiza kuwa kwenye Chaguzi zozote Vyama vya siasa vinashindanisha Sera na hoja kuhusu Maendeleo ya Wananchi wa eleo hilo,Mkataba wa CCM na Wananchi ni Maendeleo katika Taifa hili,Umoja na Mshikamano ndio ngao ya MwanaCCM yeyote.

Mwigulu Nchemba amesema dhambi ya Mauaji na Unyama unaoendelea kwenye mikutano ya siasa na maeneo mbalimbali haitamwacha Dr.slaa Salama kutokana na yeye kuwa kiongozi anayebariki Siasa chafu hizo.

Chanzo:Kalenga

Heri ya waliofanziwa na chadema maana wangali wanatembea na kuwa maonyesho,kuliko walio fanziwa na ccm,wa igunga mmoja ,morogoro mjini kwa kitu chenye ncha kali ,Arumeru wameondoa kabisa shingo ya mwanachadema ,na kuendelea .hi inanikumbusha hadith moja ,kuna jamaa walikuwa wanasafiri na gari .wakawa wanamshangilia sana dereva akimbize gari .mara gari ikapinduka .kati yao walikuwa 6 watatu wakawa wamelala chini wamekufa ,dereva hakuumia akaja kuwaangalia abiria wake .na mara polisi wakawa wamefika kwenye tukio .moja wa wale majeruhi akawa analia akilalamika dereva amewaua kwa speed zake kali .dereva kwa mshtoka .ili polisi wasisikia madai hayo .akamkeme yule majeru .akamwambia .wewe mjinga nini ? Wenzako unawaona hapo .wamekufa lakini wamenyamaza .wewe umekatika kidole unapigakelelee .nyamaza .ndio hiki kisa cha chadema walewaliokufa na ccm wale majerui .sina hakika kama huu mtindo wa Nape anaufanya akiwa na akili timamu .ama pengine anawaona wa tz kama wajinga au ni amewadharau !!??
 
Hivi kilewo akiona picha za TESHA anajisikiaje? huu unyama umepitiliza, CHADEMA ubinadamu kwenu umekwisha!
 
Last edited by a moderator:
Ina maana CCM wamebaki na sera za kuzunguka na hao waathirika wa ujasusi wao?Wameishiwa na mbinu kabisa za kushinda uchaguzi kwa njia za kuelezea mazuri yao!Amakweli sasa ni muflis wa kisiasa,waanze maandalizi ya kujiunga na Kambi rasmi ya upunzani chaguzi zijazo.
 
Back
Top Bottom