johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,125
- 142,223
Mbona Zanzibar walitaja ongezeko juzi!Habari .
Wazo la kwanza kabisa kuhusu kupinga kutaja idadi ya wagonjwa wapya wa virus vya Corona wanaongezeka kila siku lilitolewa na mbunge wa Iramba Dr Mwigulu Lameck Nchemba.
Nchemba alijenga hoja kwamba kutaja kila siku wagonjwa wapya wa Corona kunawaongezea hofu wananchi, pia mataifa mbalimbali yaliingia kwenye mashindano ya nani ana wagonjwa wengi wa Corona badala ya kujikita kwenye kutoa elimu na kutafuta dawa ya ugonjwa!.
Kama ilivyo kwa kila wazo jipya kupokewa kwa hisia tofauti, ndivyo ilivyokuwa kwa hoja ya Dr Mwigulu, wengi ya watu ambao kwao mawazo ambayo yako beyond average huwatesa sana kuelewa ( chadema) waliponda sana wazo hilo, walisema sasa Nchemba amekwisha kisiasa na kifikra. Kitu cha ajabu kabisa hata msomi Prof Kitila Mkumbo aliingia kwenye anga za chadema akaona hilo kama ngazi ya kupanda kisiasa akaanza kumchafua Nchemba kwa wapiga kura wake kupitia twita!
Naam ,leo ni wiki ya pili sasa tangu Nchemba atoe hilo wazo na hakuna wagonjwa wapya tuliotangaziwa kuongezeka badala yake tunatangaziwa waliopona.
Je hii ina maana gani kwa Chadema?
Au ndiyo inamaanisha ushauri wa Dr Nchemba umefuatwa na wizara ya afya hivyo kuwaacha uchi chadema na Kitila Mkumbo wao?
Yetu macho.
Sent using Jamii Forums mobile app