Dakika 10 za moto hotuba ya Mwigulu Nchemba bungeni

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
214
229
Baada ya kupata futari yangu safi kwa mama mmoja wa Kitanga anayefanya taaluma ya upishi kuwa ni mojawapo ya sanaa maana anafanya mapishi yaonekane ni jambo jepesi. Nilivyofika pale nikala tende zangu kisha nakujichukulia take way ili nikapatie futari kwangu kuepukana na msongamano wa watu. Ile futari baada ya kuwa imeishafika mahala pake nikaachia ini, kongosho na figo vifanye kazi yake. Tayari simu yangu ina bando la kutosha tayari kwa kujua yaliyojiri mjini. Nikaona siyo mbaya huku nikiendelea kuperuzi mtandaoni na nishushie bilauri la maji.

Wakati wa kutaka kujua kilichotokea huko bungeni mahala ambapo huwa tunawapa ridhaa wawakilishe mawazo yetu watanzania tulio wengi. Maana haiwezekani wote tukaenda kule kila mtu kutoa mawazo huwa inatupasa tuchague wachache wanaoweza kuwakilisha mawazo yetu. Nikakutana na hotuba nyingi za wapinzani wakijitahidi kuwakatisha tamaa watanzania dhidi ya ugonjwa wa corona na kuwaaminisha kuwa serikali imeshindwa kuratibu zoezi la kupambana na corona. Nilisikitika lakini baada ya kukutana na maneno mazuri yanayoeleweka na kupangiliwa vizuri na yenye afya kwa mtanzania yeyote nikapata kufarijika. Naamini tunapoelekea kwenye uchaguzi lazima tuhakikishe tunapata watu wenye ueledi wa hali ya juu kama kama wa Dr Mwigulu Nchemba.

Utaniuliza kwanini hotuba ya Dr mwigulu? Nitakachokujibu ni kuwa katika hali ya sasa wapotoshaji ni wengi na wanazidi kuwatia hofu watu dhidi ya hili gonjwa kwa maslahi yao binfasi na tamaa za kupata madaraka. Ni suala la heri na neema kwamba nchi yetu takribani tarafa zote zina vituo vya afya. Leo hii watanzania wote wanapata huduma za afya karibu na makazi yao tofauti na zamani. Kingine zaidi kwa utawala wa awamu ya tano chini ya Rais Dr Magufuli tumeanza kutoa huduma ambazo zilikuwa hazifanyiki kama matatizo ya moyo, figo na ubongo, lakini kwa sasa hizi huduma zinafanyika hapa nchini. Dr mwigulu aliongezea kuwa serikali ilikuwa inatumia zaidi ya milioni 100 kwa mgonjwa mmoja kumsafirisha nje kwa ajili ya matibabu wakati sasa huduma zinafanyikia nchini kwetu. Uone ni namna gani taifa linakuwa linapoteza hela nyingi kuwapeleka watu ughaibuni.

Rais wetu ana jicho la kinabii, miaka ya nyuma watu walikuwa wanategemea kupata matibabu nchi za wenzetu. Lakini sasa nchi zote zimezuia watu kusafiri na kupokea wageni na viwanja vya ndege vimefungwa. Je laiti kama Rais asingetoa kipaumbele kwenye huduma za kiafya leo tungekimbilia wapi na tungekuwa mgeni wa nani?. Habari nzuri ni kuwa watu wanaendelea kupatiwa matibabu na tumeona wataalamu wetu wanatuambia zaidi ya watu mia tano wanapimwa kwa siku. Hospitali ya kisasa Mloganzila inaendelea kuwahudumia wagonjwa na idadi ya watu wengi wanapona. Sasa mtu mwingine anaanzia wapi kuilaumu serikali hii? Na siyo Mloganzila pekee na hospitali zote zilizotengwa kwa ajili ya kutoa huduma ya ugonjwa huu. Jicho la kinabii kwamba ameweza kuona mbali na siku zote kiongozi lazima uwe na maono ya mbali.

Watanzania tubadili tabia, hapa Dr Mwigulu alipaeleza vizuri na hapa ndio jambo la msingi. Watu baada ya kubadili tabia wao wanakalia kujadili mambo ambayo hayasaidii jamii zetu. Watanzania tumezoea kushirikiana na kuwa pamoja lakini kwa sasa lazima watu tuepuke mikusanyiko ya watu wengi ndio maana hata suala la misiba watu wachache wanatosha kusitiri miili ya wenzetu. Tunapozidi kuwaaminisha watu kuwa serikali inaficha taarifa za watu wanaokufa haina maana yeyote na wala serikali haipati faida yeyote. Hii ni vita lazima tuache mazoea na tubadilishe taratibu ii tuweze kupambana na huu ugonjwa. Ni muhimu watu wakapata taarifa muhimu juu ya corona. Mh Mwigulu alizungumzia watu sasahivi wanaenda kununua barakoa unakuta mtu anaanza kujijaribisha na kujipima sasa huwezi jua huyo anayejaribisha kama kabeba virusi vya Corona. Ni muhimu kwa sasa tupate taarifa sahihi za ugonjwa huu.

Janga halina taarifa, watu wengi hawajui maana ya janga na corona siyo janga la nchi bali ni janga la dunia nzima. Serikali inatumia nguvu zote kupambana na hili gonjwa watu wanazidi kubeza kuwa Rais kakimbia. Sasa nani kakuambia Rais ni nesi lazima awahudumie wagonjwa. Unapoona kila kitu kinafanyika lazima ujue Rais anafanya kazi yake maana yeye ndio Amri jeshi mkuu wa nchi. Sasa hivi tunaona namna Waziri Mkuu pamoja na kushirikiana na wizara ya afya wanavyopambana kulikomesha hili janga la corona. Cha kuchekesha zaidi wale ambao wametumwa wawakilishe watu wao ndio wamekimbia wanashinda kwenye mitandao ya jamii kuikosoa serikali. Ndio maana Rais kila kitu anatusisitiza tuendelee kuwa pamoja na kumuomba Mwenyezimungu atuondolee hili janga.

Uzalendo wa Mwigulu Nchemba, siku zote amekuwa ni mzalendo na shujaa kwa nchi yake. Nakumbuka mwanafalsafa Shaaban Robert katika kitabu chake cha kusadikika anaelezea maana ya shujaa kuwa kwa nchi ni ngao kwa taifa ni hisani. Leo hii namuona Mwigulu kama hisani kwa taifa letu. Itakuwa ni fedheha sana kwa mtanzania unayejiita mzalendo na kuisemea nchi yako vibaya. Mwishoni akasisitiza kwa wale wanaobeza nchi yetu basi wakimbilie hizo nchi wakapate hayo matibabu ila hapa watanzania wataendelea kupata huduma nzuri na kwa uwezo wa Mungu watapona.

Naweza kumalizia kwa kusema hapa ndio tunapoona umuhimu wa kuwakilishwa na watu wanaojitambua. Natamani tuwe na watu wa kariba ya Mwigulu siyo kwa ajili ya elimu zao tu bali hata kwa uzalendo wa nchi yao. Kuna watu wanakimbilia kusema kuwa eti hajatoa suluhisho kwenye hotuba yake. Hapa ndio tunaona udaktari wake wa kifalsafa nadhani la muhimu ni kubadili tabia. Jiulize ndani ya nafsi yako kuwa unapenda kuishi? Je unawapenda na watu wanaokuzunguka familia na marafiki? Je upo tayari kuwalinda? Nadhani tukijiuliza hayo maswali kila mtu atabadilisha tabia yake na kujihadhari na kuwa mlinzi kwa mwenzako.

Ningependa wote tutumie hashtag mpya ya #tubadilitabia.
 
Hii inaleta matumaini, kama nchi ilitupasa tuwe na lugha moja kutokana na haya Magufuli aliyoyafanya kwa taifa lake, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, jamaa ni nabii kiukweli.

Whenever they want to kill our prophet we must stand strongly like a concrete to defend him with everything we have.
 
Mkuu.
Mimi hua nashangaa eti qanaodai mtu amekufa kwa corona kisa eti anazikwa na wachache..

Yani shida yao Wanao Fariki now kwa magonjwa yoyote yale wazikwe na wengi !!!?..
Hapo pia watasema hawafwati kanuni ya kutojumuika..
Sometimes huu uanaSiasa uchwara uishe..
Sio kila mtu anayezikwa na wachache kafa kwa Corona,
Serikali inafanya hivi ili kuzuia mikusanyiko isiyokua na Lazima..
So mwigulu kasema kweli..
Kingine kila mtu akifuat kanuni na Taratibu ni nani Ataupata.nauliza ni nani!?

Hebu watazame wauuguzi na waganga tena wenyewe ndio wapo mbele kabisa kwani wanahudimia wagonjwa Directly..lakini hebu tujifunze kwao..

Fuateni utaratibu uliowekwa yani hata Biashara na Shughuri zingine zikiendelea lakini kama unagufuatataratibu zote ni vigumu sana kuupata..

Acheni kulaumu,
Yani kama wewe ulivaa barakoa vizuri,ulijiepusha na misongamano,Ulinawa vizuri na Ulifuata taratibu zote zilizosemwa Utaupataje ugonjwa..

Ila kama wafanya mzaha na kulaumu watu huku hata kanuni ufuati aisee.

Na mnatumia janga hili kwa faida za kisiasa duuh..

Wengine wanatumia kwaajili ya kujiongezea umaarufu..

Hebu fuateni kanuni na taratibu..
Tusiwe wajuaji,wachambuzi,wabobezi wa vitu tusivyo vifahamu..
 
RIP Dr Mahinga.
Hata hilo bunge kukutana kwa sasa ni uzembe wa hali ya juu katika mapambano ya kujikinga na kumkinga mwingine dhidi ya corona.
Mwigulu ulipaswa kuonyesha mfano kwa kubakia nyumbani badala ya kusubiri serikali ukuambie bakia nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hao wanaozika wamevaaa Barakoa .Protective clothes alafu wana nyunyuzia na madawa

Acha ujinga soma na verbal expression tu utaelewa kila kitu
Mkuu.
Mimi hua nashangaa eti qanaodai mtu amekufa kwa corona kisa eti anazikwa na wachache..

Yani shida yao Wanao Fariki now kwa magonjwa yoyote yale wazikwe na wengi !!!?..
Hapo pia watasema hawafwati kanuni ya kutojumuika..
Sometimes huu uanaSiasa uchwara uishe..
Sio kila mtu anayezikwa na wachache kafa kwa Corona,
Serikali inafanya hivi ili kuzuia mikusanyiko isiyokua na Lazima..
So mwigulu kasema kweli..
Kingine kila mtu akifuat kanuni na Taratibu ni nani Ataupata.nauliza ni nani!?

Hebu watazame wauuguzi na waganga tena wenyewe ndio wapo mbele kabisa kwani wanahudimia wagonjwa Directly..lakini hebu tujifunze kwao..

Fuateni utaratibu uliowekwa yani hata Biashara na Shughuri zingine zikiendelea lakini kama unagufuatataratibu zote ni vigumu sana kuupata..

Acheni kulaumu,
Yani kama wewe ulivaa barakoa vizuri,ulijiepusha na misongamano,Ulinawa vizuri na Ulifuata taratibu zote zilizosemwa Utaupataje ugonjwa..

Ila kama wafanya mzaha na kulaumu watu huku hata kanuni ufuati aisee.

Na mnatumia janga hili kwa faida za kisiasa duuh..

Wengine wanatumia kwaajili ya kujiongezea umaarufu..

Hebu fuateni kanuni na taratibu..
Tusiwe wajuaji,wachambuzi,wabobezi wa vitu tusivyo vifahamu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom