Mwigulu Nchemba ashauri Serikali iache kutangaza wagonjwa wapya wa Corona, itangaze wanaopona na wanaokufa

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,832
Mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba ameishauri Serikali kuacha kutangaza visa vipya vya wagonjwa wanaogundulika kuwa na corona, badala yake itangaze kama ugonjwa bado upo ama la, idadi ya watu wanaopona na idadi ya wanaofariki.

Pia Mwigulu amewashangaa wapinzani kuhusu kutahadharisha kuhusu ugonjwa huu na kuhoji kwani wao ni Mungu? Kama Mungu ameshatulinda kwanini wao watie watu hofu.

 
No wonder IMF wametutosa!!

Kama hata wanaomshauri Raisi watakuwa na mitazamo kama hii,basi tujiandae kwa mengine mengi.

Politcs, sometimes and especially here in Tanzania, is about making fun or a fool of yourself in order to make a living!
 
Mh.Mwigulu anabifi afahamu kidogo umuhimu wa kuweka idadi ya visa ,mfano

1.inasaidia jamii kuongeza umakini zaidi hivyo kupunguza maambukizi kwa jamii kwani watu wanapoambiwa idadi halisi wana chukua tahadhari zaidi.


2.kuna takwimu zinatunzwa na shirika la afya ambazo zinaweza kutumika baade kama reference

3.baada ya ugonjwa kuisha kutakuwa na misaa toka monetary institutions, sasa tusipotangaza inaonekana hatuna wagonjwa,hivyo itakapofika wakati wa kupewa fedha za kuinua uchumi ulioharibiwa na korona sisi hatutapewa ili khali ugonjwa na wagonjwa wako.nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio uchumi wako uliosomea mchumi mwigulu? Dunia nzima wanatanga cases mpya ili kuwapa watu umakini na mwamko wa kujilinda wewe ni nani hadi ufiche hadi wagonjwa wa COVID 19?? Mshazoea kila kitu kuficha ficha sasa ndio madhara yake mnadhani na hili litafichika
 
Back
Top Bottom