Mwigulu Nchemba usiwaadhibu wananchi wa kawaida kwa tozo lukuki, tueleze hali ya uchumi wa nchi ikoje?

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,398
Kwa kifupi serikali ya sasa imerudisha mambo yote yasofaa ambayo mwenzao hayati Magufuli aliyaongelea kuwa ndiyo yalorudisha nyuma nchi hii.

Kwa utafiti mdogo ambao mtu yeyote aweza kuufanya hadi sasa ni kwamba;

1. Wafanyabiashara wote wakubwa na walipa kodi wakubwa wote wamesamehewa kulipa kodi hadi watakaporejesha fedha walizokuwa wakilipa kodi inavyostahiki chini ya serikali ya awamu ya tano.

Ushahidi wa hii ni serikali na TRA kukaa kimya kuhusu mapato ya kodi ya kila mwezi ambayo yalikuwa yanafika trilioni 3.

2. Utoaji stakabadhi kwa biashara nyingi sasa haupo na hata vituo vingi vya kuuza mafuta havitumii mashine zilizoleta migogoro kipindi cha awamu ya tano.

Hali ni hiyo kwenye sehemu za mahoteli na migahawa hakuna stakabadhi.

3. Sekta ya utalii imeanguka muanguko mkuu kwani bado Tanzania imewekwa kwenye orodha ya nchi ambazo bado zinaaminika kuwa ugonjwa wa UVUKO -19 bado wasumbua na hakuna taarifa rasmi za vifo, wagonjwa na wale waloambukizwa.

Hivyo Tanzania kuwepo kwenye RED LIST kunawafanya watalii wengi kukwepa kuja kwenye RED LISTED country na kwenda kwenye nchi zilizo kwenye Green na Amber listed countries.

Hiyo namba mbili haihitaji nguvu nyingi kuibaini waweza kwenda kwenye duka lolote lile au mgahawa na ukapata mwanga.

Sera ya uchumi ya sasa ambayo twaweza kuiita ni fiscal Policy inayolinganisha ukusanyaji wa kodi na matumizi ya serikali ni mbaya kwani inaumiza ukuaji (growth) wa biashara, mitaji ya biashara hizo, ukuaji wa soko la ajira, uwekezaji, mgawanyo wa rasilimali na mapato kwa mwananchi wa kawaida.

Huku tukiwa tumekumbwa na dhoruba la ugonjwa wa UVIKO-19, serikali ilipaswa kusitisha matumizi makubwa ya kodi hizohizo kwenye shughuli kama za kukimbiza Mwenge na matumizi ya ndege.

Lakini hatua za kukabiliana na matokeo ya janga la UVIKO-19 zisiwe ni kuumiza wananchi au watu wachache na zikubalike na jamii nzima ya watanzania badala ya kuamua na kulazimisha.

Kufanya hivyo bado kunaonyesha kuwa serikali hii haijali matokeo ya maamuzi yake huko mbele ya safari.

Mpaka sasa watanzania hatufahamu deni halisi la taifa, mapato halisi ya serikali kwa mwezi na pia mgawanyo wa faida wa kila mwezi utaratibu ambao uliwekwa na serikali ya awau ya tano.

Je kwa mfano, Airtel wanaendelea kutoa mgao wao kwa TTCL na serikali?

Je, vipi mgao wa TWIGA, NMB, CRDB na wengine?

Ningependa kumshauri waziri wa fedha mheshimiwa Mwigulu Nchemba kwamba aangalie sera hii ya serikali ya sasa kutaka kutoza huduma za mitandao.

Nchi yetu ilishuhudia uchumi wetu ukikua kiasi cha kuingia kwenye uchumi wa kati yaani kuna ukuaji wa uchumi wetu (growth).

Uchumi ukiwa unakuwa kisha serikali ikawa yafanya matumizi makubwa (expenditure), na mabadiliko ya mara kwa mara ya kodi ama kuuongeza au kubadili aina za kodi kunapelekea kuongeza deni la taifa.

Sasa sidhani kama wananchi wana uelewa wa hii au hapa ndipo serikali inapotumia elimu duni kuwarubuni wananchi wake.

Hizi kodi lukuki zina athari ya kuongeza mfumuko wa bei jambo linalopelekea kuuyumbisha uwiano wa uchumi yaani "emergences of damaging imbalances of economy".

Mheshimiwa Nchemba akumbuke kuwa serikali ya awamu ya tano iliweka ada ya wamiliki wa mitandao ya 100,000 kwa wenye blogs, ada ya 1,000,000 ya kila mwaka ya leseni.

Sasa, kuongeza tozo zaidi kwenye mitandao kwa maana matumizi ya apps huo ni uporaji wa haki ya kupata habari kwani wengi wataacha kutumia mitandao hiyo kwa kuogopa makato ya tozo.

Je, hizi kodi zina uwiano wowote yaani proportionate kwamba kila mlipa kodi au mtumiaji pekee wa mitandao ndiye ataelipa hiyo tozo?

Je, ipi ni mipango ya muda mrefu kuhusu uchumi khasa kuhusu soko la ajira?

Je, kulikuwepo mipango yoyote ya kikabiliana na athari za ugonjwa wa UVIKO-19 kiuchumi?

Bila kujiuliza haya sisi watanzania wote tunaonekana ni kituko kwenye majukwaa ya kimataifa kwani tayari waliona impact ya serikali ilopita (kwenye kukusanya kodi na kutupandisha daraja kuwa uchumi wa kati) na sasa wanaona kama kuna janga (disaster|) kwa yanayoendelea sasa.

Kwa sababu Benki ya Dunia na shirika la fedha Duniani (IMF) wasingweza kufikia uamuzi huo kuwa nchi yetu ipande uchumi wake endapo wangepewa taarifa za uongo.

Na hiyo pia ni kutokana na kuwepo kwa mwakilishi wao mkazi nchini.

Hivyo serikali iwe wazi ieleze hali ya uchumi kwa sasa na wapi tunaelekea na imejiandaa vipi na hali inokuja huko mbele khasa kwa upande wa sekta ya Utalii ambayo imelala chali.

Over to you Mr Mwigulu Nchemba, uloyaeleza kwenye runinga ni vigumu kuyaelewa na pale ulipangwa muda maalum.

Tuelimishane maana umo humu JF.
 
1. Mapato ya kila mwezi yanatangazwa sema wewe sio mfuatiliaji, msemaji mkuu wa serikali amekua akitoa takwimu kila mwezi ya mapato nenda kachunguze usikae tu na kulakamika

2. Swala la stakabadhi inabdi utaje na kituo maana kituo nilichopo kinatoa, pia mwezi uliopita vituo kadhaa baada ya kugundulika vilipigwa faini, pia ata wakati wa magufuli sio maduka yote yalikua yanatoa risiti usipotoshe mfano kisesa mwanza maduka wakati wa magufuli yalikua hayatoi risiti

Deni la taifa linafahamika na Benki kuu inatoa takwimi kila mwezi, wewwe sio mfuatiliaji unaandika kutokana na maneno mtaani, nenda kwenye tovuti

NMB wametoa.mgao mwezi wa 6, nimekuambia fuatilia na penda kudadisi
 
1. Mapato ya kila mwezi yanatangazwa sema wewe sio mfuatiliaji, msemaji mkuu wa serikali amekua akitoa takwimu kila mwezi ya mapato nenda kachunguze usikae tu na kulakamika

2. Swala la stakabadhi inabdi utaje na kituo maana kituo nilichopo kinatoa, pia mwezi uliopita vituo kadhaa baada ya kugundulika vilipigwa faini, pia ata wakati wa magufuli sio maduka yote yalikua yanatoa risiti usipotoshe mfano kisesa mwanza maduka wakati wa magufuli yalikua hayatoi risiti

Deni la taifa linafahamika na Benki kuu inatoa takwimi kila mwezi, wewwe sio mfuatiliaji unaandika kutokana na maneno mtaani, nenda kwenye tovuti

NMB wametoa.mgao mwezi wa 6, nimekuambia fuatilia na penda kudadisi
Hehehehehehe
 
Hawa Instagram, Facebook wao je wanatulipa Nini? Unalia lia tozo wakati nao wanatakiwa watupe kakitu, na sisi Mb zetu tunatoa kakitu
 
Safi sana mtoa mada kwa udadavuzi murua, uchumi umeparaganyika na badala ya kutumia akili kubwa wanakimbilia kwenye tozo......stimulus plan kutokana na athari za UVIKO haijawahi kuwepo na serikali imeingia kwenye janja janja ya kunyang'anya wanyonge vipesa vyao vya madafu, hopeless!
 
Safi sana mtoa mada kwa udadavuzi murua, uchumi umeparaganyika na badala ya kutumia akili kubwa wanakimbilia kwenye tozo......stimulus plan kutokana na athari za UVIKO haijawahi kuwepo na serikali imeingia kwenye janja janja ya kunyang'anya wanyonge vipesa vyao vya madafu, hopeless!
Aibu kubwa sn
 
Ndugu abiria mbele yangu Mwigulu anavuka Barabara nifanyeje?
 
Back
Top Bottom