Uteuzi wa Dkt. Mwigulu Nchemba: Siasa, Dini na Gonjwa la Corona

Mnambua

JF-Expert Member
Jan 6, 2020
246
233
Siku tu Dkt Mwigulu alipodai kesi mpya za wagonjwa wa corona zisitangazwe na akashambuliwa sana mitandaoni basi nikajua Dkt. Mwigulu anakijua atendacho. Nikakumbuka ndugu mmoja aliyenidokeza kuhusu Dkt. Mwigulu tangu akisoma Sekondari Mazengo alivyokuwa akitaka cheo ni lazima akipate, atatumia kila namna na hata kuwa puppet wa walimu ilimradi tu cheo ni lazima akipate - tena kile anachokitaka yeye.

Ukweli ni kwamba Dkt. Mwigulu huyu anautaka URais na inawezekana kama hatakuja kuupata atakuja kuwa kama Lowasa alivyofanyiwa - mtakuja kunitafuta humu - may be corona initoe labda. Mwaka huu wa Uchaguzi Jimbo la Iramba kunaweza kutokea maafa - Dkt. Mwigulu hayupo tena popular kama alivyokuwa mwanzo. Tangu juzi nimezungukia zaidi ya vijiji saba Iramba na sijaona kama uteuzi wa sasa wa Dkt. Mwigulu umewafurahisha watu. Wapiga kura hawajafurahi - hawajafurahi kwa sababu hawaendani na alichoongea Dkt. Mamba Mwigulu bungeni.

Hivi karibuni Dkt. Mwigulu aliandika wazi wazi kuwa ni "hatari kumfuata mamba kwenye kina kirefu" na kweli inaonekana ameshafanya mkakati wa kuwaumiza wapinzani wake hapa jimboni. Jana MwanaCCM mwenzetu mmoja anadai Dkt. Mwigulu alimtuma mtu wake kuwa karibu na Dkt. Kitila Mkumbo na bila kujijua Prof. Kitila Mkumbo akaropoka mambo mengi kuhusu Dkt. Mwigulu na mwisho wa siku Dkt. Mwigulu alipopata hiyo clip akashtaki chamani na kuweka ushahidi huo maskini Prof. Kitila na uropokaji wake tayari akaonekana mtu asiyefaa kabisa pamoja akili mingi zake.

Siasa ni mchezo mchafu - tena mchafu sana sa. Dkt. Mwigulu maisha yake yote anategemea siasa - hana hata hofu ya Mungu inapokuja suala la survival yake. Anazicheza siasa na zinamlipa. Upinzani wanagomea bunge lkn wanaonekana wabaya - Kingu Elibariki - huyu homeboy wetu naye anatetea bunge liendelee - huu ni ulaji kwa wabunge wa CCM. Wasipoendelea na bunge na posho zikasimamishwa watatimizaje malengo yao, hasa katika kujiandaa kuelekea kwenye Uchaguzi? Huu ugonjwa ni mtego mkubwa kwa wanasiasa, fedha wazitaka, corona waiogopa. Walioamua kuachana na fedha nao hawapo na msimamo sawa - mgogoro kati pia yao tayari umejitokeza. Kwa kweli maslahi ya kifedha na sio ya kisiasa ndiyo yanakimbiza show! Hata kwenye dini ni hivyo hivyo.

Viongozi wengi wa kidini, isipokuwa wale Maaskofu wawili kule Kagera, nao wapo maslahi sadaka. Wala hamna cha kudanganyana. Hawa wamefupisha sana muda wa ibada - wengine wamefanya muda wa ibada kufanyika ndani ya saa moja na nusu - yaani katika muda huo sana sana kinachofanyika ni ukusanyaji wa sadaka na kuziombea tu basi ibada inafungwa. Kama kweli viongozi hawa hawaogopi corona mbona ibada wamezifupisha sana. Kwanini pia katika hizo ibada fupi hawajaachana na waumini kuleta sadaka. Ninajua wanajua fika kuwa kipindi hiki ni kigumu kwa utafutaji - kwa nini wasipunguze idadi ya sadaka au waachane kabisa na kukusanya sadaka. Ukweli kanisa ni kama limeshindwa kujisimamia - hamna tena uponyaji kutoka kwa viongozi wa dini kama ulivyokuwa uponyaji mwingine dhidi ya corona. Hatujaona mgonjwa wa corona kaenda kwa kiongozi wa kidini akapona, hakuna mafuta, sijui keki, sijui kitambaa, wala nini sijui. Mambo yote ni barakoa na sanitizer na social distancing. Hata TB Joshua naye hasikikii. Viongozi wa dini hapa mmefeli kabisa - baada ya corona sijui waumini wenu tutawatafsiri vipi? Najiuliza sana!

Corona sio mchezo. Ipo kwenye papai, mbuzi, fenesi na hata hapo ulipokaa pengine. Corona ipo hata kwenye mambo ya sheria. Si unaona Dkt. Mamba Mwigulu amepewa jukumu la kufanya ufuatiliaji wa vifaa vile wkt yeye ni Waziri anayehusika na mambo ya kisheria?! Corona imempaisha Dkt. Mamba Mwigulu na inamdondosha Prof. Kitila hivi hivi. Corona wewe Covid 19 ni hatari sana! Haya Dkt. Mamba Mwigulu pole na safari ya Chato na endelea kufanyia kazi maelekezo ya Mkulu ili kupambana na corona! Utakaporudi jimboni usisahau kutuletea barakoa na sanitizer!
 
Mkuu Munambua mimi nimefurahi.... bado siajona ujasiri na mpango madhubuti toka kwa prof. kitila katika kuipigania Iramba.
Msingi wangu wa kuamini Mwigulu bado ni bora uko hapo, labda aje mwingine.
 
Mkuu Munambua mimi nimefurahi.... bado siajona ujasiri na mpango madhubuti toka kwa prof. kitila katika kuipigania Iramba.
Msingi wangu wa kuamini Mwigulu bado ni bora uko hapo, labda aje mwingine.
Mwenyewe nimekuwa nikifikir aje mwingine zaidi ya Dkt. Mwigulu kwani Dkt. Mwigulu kwa siasa za jimbo kwa sasa hana tena jipya!
 
Mimi namshangaa zaidi aliyemteua Mwigulu tena kwa mara ya pili. Hii inadhihirisha wazi wazi jinsi ambavyo kiongozi anavyotoa madaraka kama zawadi kwa wale awapendao. Kwanza tumeona upendeleo mkubwa kutoka kabila lake, upendeleo usio na aibu kabisa kama vile kuchaguliwa kwa matatibu wakuu wawili kwa mpigo wote wakitokea kabila lake. Mawaziri wengi mno wanatokea kabila lake. Ni kiongozi anayemchagua mtu kwa ajili ya faida binafsi. Sijawahi ona mambo ya hovyo kama awamu hii imekuwa aibu sana.
 
Mwenyewe nimekuwa nikifikir aje mwingine zaidi ya Dkt. Mwigulu kwani Dkt. Mwigulu kwa siasa za jimbo kwa sasa hana tena jipya!
Bado anayo nafasi, haya yaliofanyika katika miaka ya karibuni si haba. Kuna wabunge wangapi wamepita Iramba kazi kubwa waliofanya ni kununua pombe vilabuni tu. Na ndio maana wengi waliishia miaka mitano. Huyu kafanya tofauti, bado anaweza kuwa na msaada kwa maendeleo ya jimbo na hata mkoa.
Angalia hata push ya maendeleo Iramba na Singida ilivyosimama baada ya Huyu mjomba kuondoka katika nafasi ya uwaziri. Nchi hii inahitaji wanasiasa wenye influence level za juu kuweza kupisha hata bomba tu la maji au umeme wa REA. Vinginevyo hayo mtaendelea kuyasikia kwa jirani tu.
 
Mimi namshangaa zaidi aliyemteua Mwigulu tena kwa mara ya pili. Hii inadhihirisha wazi wazi jinsi ambavyo kiongozi anavyotoa madaraka kama zawadi kwa wale awapendao. Kwanza tumeona upendeleo mkubwa kutoka kabila lake, upendeleo usio na aibu kabisa kama vile kuchaguliwa kwa matatibu wakuu wawili kwa mpigo wote wakitokea kabila lake. Mawaziri wengi mno wanatokea kabila lake. Ni kiongozi anayemchagua mtu kwa ajili ya faida binafsi. Sijawahi ona mambo ya hovyo kama awamu hii imekuwa aibu sana.
Ungewataja na majina ingenoga sana!
 
Bado anayo nafasi, haya yaliofanyika katika miaka ya karibuni si haba. Kuna wabunge wangapi wamepita Iramba kazi kubwa waliofanya ni kununua pombe vilabuni tu. Na ndio maana wengi waliishia miaka mitano. Huyu kafanya tofauti, bado anaweza kuwa na msaada kwa maendeleo ya jimbo na hata mkoa.
Angalia hata push ya maendeleo Iramba na Singida ilivyosimama baada ya Huyu mjomba kuondoka katika nafasi ya uwaziri. Nchi hii inahitaji wanasiasa wenye influence level za juu kuweza kupisha hata bomba tu la maji au umeme wa REA. Vinginevyo hayo mtaendelea kuyasikia kwa jirani tu.
Push gani ilisimama? Au unaongelea Singida United?
 
Z
Push gani ilisimama? Au unaongelea Singida United?
Ziko Kadhaa, angalia kwa mfano REA, unaona nini kinaendelea??? MAendeleo wakti mwingine yanahitaji tu harakati na uhamasishaji ili watu wajitume katika kujiletea kipato. Binafsi niliona Iramba na singida ikiwa imehamasika mno kipindi kile na naona hali ile ikirudi.
Kwa sasa Singida ilikuwa imepoa mnooooo kwa kila kitu. Mwigulu ni hamasa ya watu kujituma Singida yote.
 
Back
Top Bottom