Mwigulu Nchemba ashauri Serikali iache kutangaza wagonjwa wapya wa Corona, itangaze wanaopona na wanaokufa

Shaabash!
P.oor.H.andling D.isorder
Kuwa msomi sana huwa inachanganya mtu....hata kuchanganya sherehe za harusi kuwa ni vipaumbele vya Taifa.
...I am just an observer.
 
Ni wapi nimesema Wangwe alikufa sababu ya kuhoji ?Huwa siandiki vitu nisivyokuwa na evidence navyo. Again,nimesema hivi Wangwe alisimamishwa umakamu mwenyekiti sababu ya kuhoji mambo kadhaa ndani ya chama. Alisimamishwa au hakusimamishwa ?Shule za kata zinawafanya muwe na upeo mdogo wa kuelewa. Kajipange upya.
Nimekuelewa bush school graduate.
 
Mnaomponda Mwigulu hajawahi kuwa wanasiasa wala kufikiria kugombea ubunge
Ukifuatilia bunge kwa sasa utagundua kuwa kauli nyingi ni za kujipendekeza kwa kulenga uchaguzi 2020
 
Hapana. Tulianzisha sisi kwaajili ya kumrudisha Obote madarakani.

Nakumbuka Mwalimu alipokuja pale UDSM, Prof. Shivji alimwuliza Mwalimu kama ifuatavyo:

"Mwalimu, tunajua kuwa tuliamua kumwondoa Amin madarakani ili kumrudisha rafiki yako Milton Obote madarakani na siyo kwa sababu Amin alituvamia. Hatuwezi kulaumu, labda inawezekana kwa kumrudisha Obote, EAC ingefufuka na kuwa imara, na ama Waganda wangeweza kuwa na uhuru zaidi. Tukaingia vitani, tukafanikiwa kumwondoa Amin. Tukaunda serikali ya muda iliyoongozwa na Prof. Yusuf Lule, lakini akaanza kufanya mambo ambayo hatukuyataka, akataka kujiimarisha, tukamwondoa. Tukamweka Godfrey Binaisa. Naye hakumudu, akaondolewa. Baadaye kabisa tukafanikiwa kumweka aliyekusudiwa, Milton Obote. Obote akawa Rais, akajitangaza pia ni Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Fedha. Kwa kupitia Uwaziri wa Ulinzi, aliwaua wapinzani wake kuliko alivyoua Idd Amin. Kwa kupitia Uwaziri wa Fedha, akaiba hela ya Waganda kwa kiaso ambacho hakuna anayejua. Hatimaye Waganda wakaungana, wakamwondoa Obote, akakimbilia Zambia. Watanzania tumepoteza vijana wetu, tumepoteza fedha zetu, Wewe ukiwa Rafiki wa Obote, una nini la kusema?"

Mwalimu, tofauti kabisa tulivyotegemea, aliinama chini, kisha akasema, "TUMWOMBEE KWA MUNGU". Sote tuliduwaa maana aliyokuwa akiyasema Shivji yalikuwa mageni kwa sisi sote.

Kwa hiyo, naamini ni kweli kuwa kuna mengi tunayoambiwa, hayana uhalisia. Akina Mwigulu wamekulia kwenye hii mifumo ya kusema uwongo. Ndiyo maana kwao kuusema ukweli ni dhambi kubwa.
Duh.! kumbe, hivi kumbe Nyerere watu walikuwa wanaweza kumchallenge hadharani namna hiyo? halafu Nyerere pia alikuwa akiunga mkono waasi wa Biafra huko Nigeria, sababu nayo ni nini, ni nyerere pia alisuka mpango wa mapinduzi huko Zanzibar?
 
Nchi yetu imepita katika majanga mengi ya maradhi.

Kwa mtazamo wangu corona siyo ugonjwa tishio kabisa kwa Africa hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara, sema huu ugonjwa huu umekuwa overrated na western media kwa kuwa umewadhuru sana wao ukilinganisha na Africa.

Ukiangalia takwimu wengi wanapona huu ugonjwa. Mwigulu nchemba alitoa wazo zuri.

Sioni umuhimu wa kutangaza idadi ya maambukizi ili kupunguza hofu katika jamii kwani hofu peke yake inaweza kusababisha vifo vingi kuliko hata corona yenyewe. Wote tunajua magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza yalivyo sababisha maelefu ya watu nchini.

Mfano Kipindu pindu kuna wakati ulitokea mlipuko walikuwa wanazikwa watu 50 kwa siku. Vilevile, Ukimwi wakati watu hawajapata elimu ya afya vifo vilikuwa vingi sana.

Ugonjwa wa corona ka ugonjwa cha kawaida tu ila kutokana na taharuki iliyojengwa na vyombo vya habari vya Mabeberu jamii ilikuwa na woga sana

Kwa jinsi ninavyojua Mtanzania hutembea na malaria bila kujua na kupona bila kujijua

Naamini corona haitaleta madhara yeyote kwa Watanzania kwani mpaka sasa imesababisha digit moja tu ya vifo

Wakati Tunaendelea kupambana na corona tusisahau kuwa Ukimwi upo na una ua Ndugu zangu Watanzania Tuendelee kujihadhari.

Fuata maelekezo unayopewa na viongozi wako ili uwe salama

Tuipende Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwigulu nchemba alitoa wazo zuri sana

Kutangaza idadi ya maambukizi haisadii kitu zaidi ya kuleta hofu kwenye Jamii

Zaidi serkali ijikite katika kuboresha na kuongeza vipimo ili wanaogundulika wamethirika wakae hospitalini hadi wapone

Corona sio hatari kwa Nchi za kusini mwa jangwa la Sahara
Tushasema sana lakini ndo hivyo viongozi wameziba masikio huu ugonjwa sio tishio kwetu kama ilivyo ngozi nyeupe. Sisi tunafuata tu upepo,ya nini kutangaza tangaza idadi ya walioambukizwa?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna familia naifahamu toka mambo ya corona yaanze kutangazwa haitoki Ndani imejifungia tu wamefunga biashara yao kwa wiki mbili sasa

Serkali ibadilishe utaratibu wa ku dili na huu mlipuko wa corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna familia naifahamu toka mambo ya corona yaanze kutangazwa haitoki Ndani imejifungia tu wamefunga biashara yao kwa wiki mbili sasa

Serkali ibadilishe utaratibu wa ku dili na huu mlipuko wa corona

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayakuhusu acha kuingilia maisha ya watu binafsi! Pambana na hali yako dogo
 
Mwigulu nchemba alitoa wazo zuri sana

Kutangaza idadi ya maambukizi haisadii kitu zaidi ya kuleta hofu kwenye Jamii

Zaidi serkali ijikite katika kuboresha na kuongeza vipimo ili wanaogundulika wamethirika wakae hospitalini hadi wapone

Corona sio hatari kwa Nchi za kusini mwa jangwa la Sahara

Sent using Jamii Forums mobile app
Dogo hizi bangi unazovuta sio za nchi hii, jitahidi utulize mzuka tafadhali
 
Back
Top Bottom