Mwigulu Nchemba anashangaa Waziri kufua nguo Ulaya hajui kuwa mabeki tatu walikuwa wanatumwa buchani SA kununua kitoweo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,965
141,968
Namfahamu mwanasiasa mmoja ambaye alikuwa akimtuma house girl kwenda kununua nyama buchani/ supermarket Afrika ya Kusini kila wiki.

Hili la kufua nguo Ulaya, Nairobi au Pretoria ni la kawaida sana kwa viongozi na wengi wao wanakwepa dry cleaners za hapa nyumbani kwa kuhofia kulogwa kupitia nguo zao.

Yawezekana Mwigullu Nchemba alimlenga mtemi Chenge au Nyalandu lakini kiukweli wenye mapene wote walifua nguo zao nje ya nchi, ndio hawa akina Adam, Ngelejela, Maigae nk nk.

Hiyo ilikuwa kawaida sana kwa waishio mjini.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nyalandu katumikia uwaziri kwa miezi michache tu,,kama mapene anayo ni yake
 
Waliotajwa na mwana-CCM Kindakindaki wote ni wana-CCM, tena waliowahi kuhudumia ngazi za juu kabisa serikalini!

Kama ndivyo, hatimae mwana-CCM Kindakindaki unatuthibitishia kwamba CCM na Viongozi wanaotokana na CCM ni kansa kubwa kwa taifa!

Mosi, inaonekana kwamba CCM na Viongozi wanaotokana na CCM ni watu waliotopewa na ujinga vichwani mwao manake ikiwa mtu unaogopa eti kulogwa kupitia nguo, huo ni ujinga kuliko hata ujinga wenyewe!

Pili, inaonekana kwamba CCM na Viongozi wanaotokana na CCM hawaziamini biashara za Kitanzania kwa sababu ikiwa wanaamini wanaweza kurogwa kupitia nguo walizopeleka dry cleaners, ina maana hawaamini HATA PUNJE ya weledi wa KAMPUNI ZOTE za dry cleaners za TZ

Tatu, kama nguo tu wanapeleka nje ya nchi kwa kuogopwa kulogwa kupitia nguo; je walikuwa wanakula mchele wetu wa Mbeya hawa?! Walikuwa wanatumia nyanya zetu za Lushoto hawa? Walikuwa wanatumia maji yetu ya Uhai, Kilimanjaro, and the like hawa?!

Ni ujinga wa wana-CCM na Viongozi wanaotokana na CCM au ni kutaka kuwakoga wananchi maskini wanaowapatia huo uongozi?!
 
Mimi ukinipa mbeleko, huwa nabeba hata watoto wachanga (0-3 yrs) mgongoni. Huwa ninaweza hata kutembea nikiwa nimebeba mtoto mgongoni, napita naye mtaani naenda sokoni kununua nyaya!
 
Waliotajwa na mwana-CCM Kindakindaki wote ni wana-CCM, tena waliowahi kuhudumia ngazi za juu kabisa serikalini!

Kama ndivyo, hatimae mwana-CCM Kindakindaki unatuthibitishia kwamba CCM na Viongozi wanaotokana na CCM ni kansa kubwa kwa taifa!

Mosi, inaonekana kwamba CCM na Viongozi wanaotokana na CCM ni watu walioptopewa na ujinga vichwani manake ikiwa mtu unaogopa kurogwa kupitia nguo, huo ni ujinga kuliko hata ujinga wenyewe!

Pili, inaonekana kwamba CCM na Viongozi wanaotokana na CCM hawaziamini biashara za Kutanzania kwa sababu ikiwa wanaamini wanaweza kurogwa kupitia nguo walizopeleka dry cleaners, ina maana hawaamini HATA PUNJE ya weledi wa KAMPUNI ZOTE za dry cleaners za TZ

Tatu, kama nguo tu wanapeleka nje ya nchi kwa kuogopwa kurogwa kupitia nguo; je walikuwa wanakula mchele wetu wa Mbeya hawa?! Walikuwa wanatumia nyanya zetu za Lushoto hawa? Walikuwa wanatumia maji yetu ya Uhai, Kilimanjaro, and the like hawa?!

Ni ujinga wa wana-CCM na Viongozi wanaotokana na CCM au ni kutaka kuwakoga wananchi maskini wanaowapatia huo uongozi?!
Nyalandu ni CCM?

Uchawi umezungumzwa hadi kwenye Biblia takatifu bwashee!
 
Ajenge hoja zenye mashiko, kwenda kufua nguo ulaya ni kipato Cha mtu kikiruhusu siyo vibaya, na exposure ni muhimu kwa kila mtu ili kufunguka ki fikira, mtu aliyekulia kijijini bila kutoka huwezi kumlinganisha na mtu aliyefika hata Dar, tuacheni kushabikia kutokupata exposure na kwanini yeye haishi muda wote huko kijijini anashinda Dar.
 
Nyalandu ni CCM?

Uchawi umezungumzwa hadi kwenye Biblia takatifu bwashee!
Team uliyoitaja wengi ni CCM! Na hiyo inaonesha ni CCM ndiko yaliko mambo ya kulogana logana kwa sababu hata enzi zile wakati watu wanawekeana "unga" kule bungeni, suala lile liliwahusisha wana-CCM!

Hivyo basi, kuna uwezekano mkubwa hata huyo Nyalandu alikuwa anafanya hayo wakati yupo CCM na hivi sasa itakuwa ameshaacha baada ya kuwa ameshatoka kwenye genge la wachawi!

Lakini hata kama itakuwa bado anaendelea, ni kwa sababu tu tayari alishaaribiwa na CCM!!
 
Back
Top Bottom