Mwigulu Nchemba ameleta maendeleo jimboni kwake

Mwigulu Nchemba ameleta maendeleo jimboni kwake

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
3,098
Reaction score
631
10568911_289961367872765_5012020053667875809_n.jpg

Mh:Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr.Kone wakati wakukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Maabara za Kisasa Katika Shule za Jimbo la Iramba,Hapa ni Shule ya Kijiji cha Usule.Kufikia Tar.31/09/2014 Mkuu wa Mkoa anategemea Kumkabidhi Mh:Rais Jakaya Kikwete Maabara zote za Shule za Sekondari zikiwa zimekamilika ndani ya Mkoa wa SIngida kuendana na Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
10615609_289962554539313_2503796252753281458_n.jpg

Mkutano unaendelea huku Mh:Mwigulu nchemba akiwafafanulia mambo mbalimbali ya maendeleo wanakijiji wa Usule,Kubwa ni Usambazaji wa maji hapo Kijijini ambao tayari umekwisha anza,Pia amesisitiza Kusuka nyaya za Umeme wakati huu Umeme unapowekwa kwenye nguzo,Ukiingiza Umeme wakati huu mafundi wakiwa wanasambaza nyaya ni Bei nafuu 27000/= tu.

10426171_289961904539378_3950919716198159061_n.jpg

Ilikukamilisha Ujenzi wa Maabara ya Shule ya Usule Mh:Mwigulu amechangia Mifuko 100 ya Sementi na ameagiza kwenye Upungufu wowote Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi atoe taarifa.Hivyo hivyo amesaidia Uchimbaji wa Bwawa la maji kama Mpango wa Muda mfupi wakati Bomba za Maji zikiendelea Kusambazwa kijiji chote cha Usule.
10406533_289961871206048_3320458004636324388_n.jpg

14959_289962514539317_6866443170765152599_n.jpg

10635799_289962491205986_8076544293195350125_n.jpg

Mh:Mwigulu Nchemba akikabidhi Mchango wake wa bati 70 kwa Diwani wa kata ya Mbelekesye kwaajili ya kuezeka Madarasa ya shule ya Mbelekesye yaliyoongezwa.Pia amechangia Mifuko 100 na Mbao kwaajili ya kupau madarasa hayo.
Wakati hili likifanyika katika kijiji cha Kibaya,Mh:Mwigulu Nchemba jana alikabidhi Mabati 320 kijiji cha Misuna kwaajili ya Ujenzi wa Zahanati.
10557464_289962551205980_4116640334007969904_n.jpg
 
Huu ndio uzuri wa kuichagua CCM na Wabunge wake, Mnakuwa na uhakika wa maendeleo...

"CCM = Maendeleo kwanza"
 
'welcome 2015' hio inaitwa, hichi ndo kipindi cha kukamua wallet zetu kwa wananchi kujiimarisha na mbio za mwakani!!
 
Haa haa, hiyo pesa mwigulu ni yake? Acheni uwongo na propaganda ya wazi hapa!
 
Unamuongelea Mwigulu huyu gaidi au mwingine?
 
Haa haa, hiyo pesa mwigulu ni yake? Acheni uwongo na propaganda ya wazi hapa!

hii 1% ya zile milion 10 za maendeleo ya jimbo anazopewa kila mwezi...99% ya fedha zilizobaki ametia mfukoni mwake. fisadi mkubwa!
 
aaaaah aaaaaah!!! Maaabara singida nzima ni ndoto ya mchana kweupe peee!!! Kilimanjaro imeshindwa ni singida aaaah aaaaah

Alafu taifa hili kwa kuwa na watu wasiofikiri ni shida sana. Kabla ya kuchepuka kwe mambo mengine mimi nimekuwa mwaalimu kwa miaka saba. Nimekuwa mtaaluma, makamu wa shule na nimekaimu shule mwaka mzima.
Hii siasa ya kujenga maabara si ya leo nenda mijini majengo ya maabara yapo. Maabara siyo jengo peke yake ninafahamu shule zimejengwa miaka mitatu iliyopita hadi leo wanafanya alternative papers.
Nikiwa academic ilituchukua mwaka na nusu kujenga jengo lakini ilichukua miaka mitatu kuweza kufanya practical paper mitihani ya taifa. Vifaa vya maabara ndio maabara maana ukiwa navyo hata darasa unawezalifanya maabara. Tuliomba ufadhili sehemu mbalimbali na baada ya miaka miwili ndipo mamlaka ya hifadhi ngorongoro ilijitokeza kununua sehemu ya vifaa ambavyo pia iliwachukua mwaka kukamilasha. Bado hadi naaga ajira ya serikali kwenda kwenye taasisi nyingine maabara ilikuwa na mapungufu mengi japo kwa kuungaunga inafanikisha lengo. Maabara kwa maana ya ccm ni jengo ila mahali pengi mimepita maabara zimegeuzwa madarasa maana hamna vifaa. Vifaa vya maabara ni expensive sana ulizia bei tu ya test tube maana ni ndogo sana utashangaa sembuse chemicals kuna kikopo tu gram 500 kinauzwa laki moja. Kwahiyo kisiasa maabara zinaweza kujengwa lakini zikawa nyumba za popo maana hamna sera ya elimu nchi hii. Elimu inaamuliwa na matakwa ya siasa inataka nini kwa minajili ya umaarufu.

Mambo yanatakiwa kufanyika kitaalamu siyo kisiasa kwahiyo hizi maabara zinazopigiwa kelele fanyeni utafiti mje na majibu sahihi siyo jengo la milion 20 ukazani kazi imeisha. Mifumo ya maji safi na taka, ya nishati na kumanage pollution haipo. Hakuna vifaa karibu million mia na tunajipongeza tuna maabara. Jengo ni theluthi moja tu ya gharama za vifaa. So kama hamna plan tukubaliane mnajenga madarasa tu. Sehemu nyingi fanya utafiti uone mmejenga madarasa badala ya maabara maana kitu huwa kamilifu kinapofanya kazi yake. Ndio maana nikiwasikia mkibwabwaja humu huwa nacheka sana!! ccm bwana kwa hadaa mmezidi.
 
aaaaah aaaaaah!!! Maaabara singida nzima ni ndoto ya mchana kweupe peee!!! Kilimanjaro imeshindwa ni singida aaaah aaaaah

alafu taifa hili kwa kuwa na watu wasiofikiri ni shida sana. Kabla ya kuchepuka kwe mambo mengine mimi nimekuwa mwaalimu kwa miaka saba. Nimekuwa mtaaluma, makamu wa shule na nimekaimu shule mwaka mzima.
Hii siasa ya kujenga maabara si ya leo nenda mijini majengo ya maabara yapo. Maabara siyo jengo peke yake ninafahamu shule zimejengwa miaka mitatu iliyopita hadi leo wanafanya alternative papers.
Nikiwa academic ilituchukua mwaka na nusu kujenga jengo lakini ilichukua miaka mitatu kuweza kufanya practical paper mitihani ya taifa. Vifaa vya maabara ndio maabara maana ukiwa navyo hata darasa unawezalifanya maabara. Tuliomba ufadhili sehemu mbalimbali na baada ya miaka miwili ndipo mamlaka ya hifadhi ngorongoro ilijitokeza kununua sehemi ya vifaa ambavyo pia iliwachukua mwaka kikamilosha. Bado hadi naaga ajira ya serikali kwenda kwenye taasisi nyingine maabara ilikuwa na mapungufu mengi japo kwa kuunga unguunga inafanikisha leongo. Maabara kwa maana ya ccm ni jengo ila mahali pengi mimepita maabara zimegeuzwa madarasa maana hamna vifaa. Vifaa vya maabara ni expensive sana ulizia bei tu ya test tube maana ni ndogo sana utashangaa sembuse chemicals kuna kikopo tu gram 500 kinauzwa laki moja. Kwahiyo kisiasa maabara zinaweza kujengwa lakini zikawa nyumba za popo maana hamna sera ya elimu nchi hii. Elimu inaamuliwa na matakwa ya siasa inataka nini kwa minajili ya umaarufu.

Mambo yanatakiwa kufanyika kitaalamu siyo kisiasa kwahiyo hizi maabara zinazopigiwa kelele fanyeni utafiti mje na majibu sahihi siyo jengo la milion 20 ukazani kazi imeisha. Mifumo ya maji safi na taka, ya nishati na kumanage pollusion haipo. Hakuna vifaa karibu million mia na tunajipongeza tuna maabara. Jingo ni theluthi moja ya gharama za vifaa. So kama hamna plan mnajenga madarasa. Sehemu nyingi fanya utafiti uone mmejenga madarasa badala ya maabara.

asante sana kwa uchambuzi wa kina .
 
aaaaah aaaaaah!!! Maaabara singida nzima ni ndoto ya mchana kweupe peee!!! Kilimanjaro imeshindwa ni singida aaaah aaaaah

Alafu taifa hili kwa kuwa na watu wasiofikiri ni shida sana. Kabla ya kuchepuka kwe mambo mengine mimi nimekuwa mwaalimu kwa miaka saba. Nimekuwa mtaaluma, makamu wa shule na nimekaimu shule mwaka mzima.
Hii siasa ya kujenga maabara si ya leo nenda mijini majengo ya maabara yapo. Maabara siyo jengo peke yake ninafahamu shule zimejengwa miaka mitatu iliyopita hadi leo wanafanya alternative papers.
Nikiwa academic ilituchukua mwaka na nusu kujenga jengo lakini ilichukua miaka mitatu kuweza kufanya practical paper mitihani ya taifa. Vifaa vya maabara ndio maabara maana ukiwa navyo hata darasa unawezalifanya maabara. Tuliomba ufadhili sehemu mbalimbali na baada ya miaka miwili ndipo mamlaka ya hifadhi ngorongoro ilijitokeza kununua sehemu ya vifaa ambavyo pia iliwachukua mwaka kukamilasha. Bado hadi naaga ajira ya serikali kwenda kwenye taasisi nyingine maabara ilikuwa na mapungufu mengi japo kwa kuungaunga inafanikisha lengo. Maabara kwa maana ya ccm ni jengo ila mahali pengi mimepita maabara zimegeuzwa madarasa maana hamna vifaa. Vifaa vya maabara ni expensive sana ulizia bei tu ya test tube maana ni ndogo sana utashangaa sembuse chemicals kuna kikopo tu gram 500 kinauzwa laki moja. Kwahiyo kisiasa maabara zinaweza kujengwa lakini zikawa nyumba za popo maana hamna sera ya elimu nchi hii. Elimu inaamuliwa na matakwa ya siasa inataka nini kwa minajili ya umaarufu.

Mambo yanatakiwa kufanyika kitaalamu siyo kisiasa kwahiyo hizi maabara zinazopigiwa kelele fanyeni utafiti mje na majibu sahihi siyo jengo la milion 20 ukazani kazi imeisha. Mifumo ya maji safi na taka, ya nishati na kumanage pollution haipo. Hakuna vifaa karibu million mia na tunajipongeza tuna maabara. Jengo ni theluthi moja tu ya gharama za vifaa. So kama hamna plan tukubaliane mnajenga madarasa tu. Sehemu nyingi fanya utafiti uone mmejenga madarasa badala ya maabara maana kitu huwa kamilifu kinapofanya kazi yake. Ndio maana nikiwasikia mkibwabwaja humu huwa nacheka sana!! ccm bwana kwa hadaa mmezidi.
 
NAONA ULIKUWA HAUJALIPWA MUDA MREFU SANA NA LEO ANGALAU AMEKUKUMBUKA KWA KUKUJAZIA TUMBO NDO UKAKUMBUKA KURUDI JF. HIZO MAABARA ANAJENGA KWA HELA IPI? UNAFIKIRI KILA KICHWA NI CHA KUDANGANYWA? KULIKUWA NA UMUHIMU GANI WA KUHANGAIKA NA BARABARA ILE YA KIFISADI BADALA YA MAENDELEO YA WANANCHI? HAHAHAHAAA KWANI 2015 MBALI BHANA. FURAHIENI MIPIRA YA MIGUU NA UKISHINDA UNAPEWA NG'OMBE MMOJA KISHA MNACHINJA NA KUGAWANA WATU MIA MOJA WAKATI MAENDELEO HAKUNA. FURAHIA SANA KWANI AKILI NDOGO HAIWEZI GUNDUA FIKRA PEVU NA ZA MBELE KIMAENDELEO. KIMSINGI ANAHANGAIKA KWA SASA KWA AJILI YA WATU KAMA NINYI MNAODANGANYIKA KIRAHISI MWAKANI MKUMBUSHWE KWAMBA MLIPEWA NYAMA MKALA. WENYE UPEO HATUONI. NJAA ITAWAUWA NINYI KINA jr.
 
MANDAL JR ANAFIKIRI SCIENCE KIT MOJA YA MAABARA INAUZWA BUKU SABA ALOZOEA KULIPWA AKILETA UZUSHI HUMU. NJOO TUKUPE BEI. LABDA MWIGULU ATOE HELA ZOTE KWENYE AKAUNTI YAKE ALIZOPATA WAKATI WA UTUMISHI USIOTUKUKA BENKI HELA ZETU ZILIPO EPA, PIA ATOE ZOTE ALIZOPATA WAKATI WA UHAZINI LUMUMBA Ndo maabara zitajengwa. Otherwise usilete uongo humu
 
Back
Top Bottom