Shine
JF-Expert Member
- Feb 5, 2011
- 11,481
- 1,371
Ndugu yangu Mwigullu ..Mdogo wangu...
Naomba nenda pale Chuo kikuu ajiri Political Scientist akufanyie tathmini.....ya siasa Zako ...
Tathmini ya haraka haraka ya kina kabisa inaonesha kuwa aina ya siasa unazofanya zinakiumiza Chama cha mapinduzi..kuliko kusaidia ...Kwa kiasi kikubwa unashindwa Kusoma mazingira ya hadhira...Umezidisha Propaganda...Zaidi kuliko kuongelea kwa lugha nyepesi na ya kueleweka Sera za Chama
Wananchi wa Leo wanahitaji Zaidi kusikiliza sera kuliko porojo...,uwongo au propaganda....
Uchaguzi wa mwaka 2015 utaamuliwa na vijana...ili CCM ishinde ni lazima ihangaike na agenda za vijana ambao kwa sasa...wanao uelewa ...na aina ya siasa unazofanya hazita kuwa na tija ........Ongelea namna ya kutengeneza Ajira..kupitia Kilimo,viwanda..ufundi .....,ufugaji etc...
Siasa Zako zinaonekana ni za uchonanishi na utangano.....hazikujengi wewe Kama Statesman...yaaani mwana siasa ambayo atafikiri mbali ya upeo wa Chama Chake ....na kujenga Utaifa Zaidi .....,Ukitazama miaka mitatu ijayo Kama hutabadili aina ya siasa Zako na kujielekeza kwenye Issues na kuwacha propaganda......naona utakuwa na nafasi finyu ...Sana yakuendele kuwa kwenye nafasi kubwa kwenye Chama au serikali.....ukijilinganisha na wana siasa wengine vijana ndani ya CCM ......Kama January Makamba...,Maselle ( tazama Jana ulipomaliza kumwaga propaganda bungeni...Massele alisimama akajielekeza kwenye hoja )...Emmanuel Nchimbi......,Hussein Mwinyi..,Lazaro Nyalandu...,Deo Fulikunjombe..,etc
Kama kijana ni muhimu kufanya siasa za sasa na wakati ujao.....,ili kujijengea uhalali Kitaifa ni lazima ukubalike na vijana wote ndani ya Chama na hata tena hasa nje ya chama.....,Watu wanakulinganisha na Hawa Ghasia...kwa kuongea bila kufikiri.
Ni lazima uangalie beyond ....2015....,vijana wenzako ndani ya CCM wamejingea heshima ndani na nje ya CCM........ukiamua kubadili aina ya siasa unazofanya kwa sasa unayo nafasi...ya kuwa kiongozi wa wakati ujao wa CCM ...
Tatizo la huyu kiburi na unafiki umemjaa na wenzake ccm ndo wanaomdanganya afanye propaganda za kuihujumu CDM nae pasipokufikiri anatekeleza pasipokujua anapotea kisiasa na akishapotea asitegemee ccm watamgeukia ama kuwa nae tena la hasha watamtupilia mbali kama toilet pepa isiyokuwa na thamani baada ya kutumika