Mwigulu Nchemba akana kauli yake

Mwigulu Nchemba akana kauli yake

Hakuna cha unyonge ila hakukuwepo na mapepo ya kukemea. Nimeongea kwa lugha ya mazungumzo sio ya kukemea mapepo ya bungeni


Ndugu yangu Mwigullu ..Mdogo wangu...

Naomba nenda pale Chuo kikuu ajiri Political Scientist akufanyie tathmini.....ya siasa Zako ...



Tathmini ya haraka haraka ya kina kabisa inaonesha kuwa aina ya siasa unazofanya zinakiumiza Chama cha mapinduzi..kuliko kusaidia ...Kwa kiasi kikubwa unashindwa Kusoma mazingira ya hadhira...Umezidisha Propaganda...Zaidi kuliko kuongelea kwa lugha nyepesi na ya kueleweka Sera za Chama
Wananchi wa Leo wanahitaji Zaidi kusikiliza sera kuliko porojo...,uwongo au propaganda....
Uchaguzi wa mwaka 2015 utaamuliwa na vijana...ili CCM ishinde ni lazima ihangaike na agenda za vijana ambao kwa sasa...wanao uelewa ...na aina ya siasa unazofanya hazita kuwa na tija ........Ongelea namna ya kutengeneza Ajira..kupitia Kilimo,viwanda..ufundi .....,ufugaji etc...

Siasa Zako zinaonekana ni za uchonanishi na utangano.....hazikujengi wewe Kama Statesman...yaaani mwana siasa ambayo atafikiri mbali ya upeo wa Chama Chake ....na kujenga Utaifa Zaidi .....,Ukitazama miaka mitatu ijayo Kama hutabadili aina ya siasa Zako na kujielekeza kwenye Issues na kuwacha propaganda......naona utakuwa na nafasi finyu ...Sana yakuendele kuwa kwenye nafasi kubwa kwenye Chama au serikali.....ukijilinganisha na wana siasa wengine vijana ndani ya CCM ......Kama January Makamba...,Maselle ( tazama Jana ulipomaliza kumwaga propaganda bungeni...Massele alisimama akajielekeza kwenye hoja )...Emmanuel Nchimbi......,Hussein Mwinyi..,Lazaro Nyalandu...,Deo Fulikunjombe..,etc
Kama kijana ni muhimu kufanya siasa za sasa na wakati ujao.....,ili kujijengea uhalali Kitaifa ni lazima ukubalike na vijana wote ndani ya Chama na hata tena hasa nje ya chama.....,Watu wanakulinganisha na Hawa Ghasia...kwa kuongea bila kufikiri.

Ni lazima uangalie beyond ....2015....,vijana wenzako ndani ya CCM wamejingea heshima ndani na nje ya CCM........ukiamua kubadili aina ya siasa unazofanya kwa sasa unayo nafasi...ya kuwa kiongozi wa wakati ujao wa CCM ...
 
Hakuna cha unyonge ila hakukuwepo na mapepo ya kukemea. Nimeongea kwa lugha ya mazungumzo sio ya kukemea mapepo ya bungeni

Ndg yangu kama ccm nashauri tukae kitako, tujadiliane na tuje na suluhisho. tuzihurumie damu na roho za ndugu zetu ili tusije tukadaiwa kwa kumwaga damu yao kwasababu ya madaraka. naamini mwigulu kuna siku utakufa na kama kuna damu imemwagika kwasababu yako utaikuta mbele za Mungu ikikusubiri uipe haki yake ya kuishi wakati hutakuwa na uwezo huo

amani ya nchi ipo mikononi mwako na ccm, tusipokaa kitako tujue nchi hii haitatufaa ss wala watoto wala wajukuu zetu kuishi

najua utatumia busara kuyapima na kuyaona haya
 
Hakuna cha unyonge ila hakukuwepo na mapepo ya kukemea. Nimeongea kwa lugha ya mazungumzo sio ya kukemea mapepo ya bungeni

Mkuu wewe kweli Mbunge au Muwakilishi wa watu Bungeni? Watu wanatoa hoja wewe unaongelea Mapepo, who nis pepo by the way? Na mashaka na wadhifa ulonao otherwise am done.
 
tabu ya wadudu wa Unga a.k.a watu wa Njia ya vumbi mkishaingia mjini 'MNAPITILIZA',Ndugu kapime akili yako naona Ipo spidi zaidi hata ya 'NEWTON LAW'

Mkuu ni law gani ya newton inayoongelea speed? simtetei Njemba lkn kuhusu hiyo Njia ya Vumbi, all tanzanian their roads are VUMBI's..wewe unakaa Tanzania ipi barabara sio ya vumbi?
 
Hakuna cha unyonge ila hakukuwepo na mapepo ya kukemea. Nimeongea kwa lugha ya mazungumzo sio ya kukemea mapepo ya bungeni
Wewe ni wa Baba yako ibilisi shetani maana tamaa zake ndizo upendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuwaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo. (yoh 8:44) mtu wa jinsi hii hana uwezo wa kutoa pepo.
 
Hakuna cha unyonge ila hakukuwepo na mapepo ya kukemea. Nimeongea kwa lugha ya mazungumzo sio ya kukemea mapepo ya bungeni

damu ya uliowaua/ mauaji uliyoratibu yatakuandama for the rest of your life....... nakuhakikishia hutaweza kulala usingizi mzuri kwa maisha yako yaliyosalia.
 
Bwana alisema "Mtawatambua kwa matunda yao. je! watu huchuma zabibu katika miiba?..... Mathayo 7:16, Wewe Mwigulu huna hata Chembe ya Roho ya Mungu ndani yako (Wagalatia 5:19-23) Tubu Uovu wako la sivyo unakwenda Jehanamu ya Moto kwa Uovu Wako. Bwana Yesu Amekuona Leo (Mithali 28:13)
 
Hakuna cha unyonge ila hakukuwepo na mapepo ya kukemea. Nimeongea kwa lugha ya mazungumzo sio ya kukemea mapepo ya bungeni

Hivi kweli ndugu unayo akili timamu? Au uliwahi kuugua Kichaa? Mbona wewe umekua ni mtu wa ajabu sana!?

Mwenyewe wewe ni PEPO sasa utakemeaje pepo wenzio? Unachokifanya mdogo wangu haimpendezi hata Mungu. Kweli damu za watu zimemwagika lakini bado unaleta Siasa ktk maisha ya watu?
Ole wako maana Damu isiyo na hatia iliyomwagika aidha kwa wewe kuhusika ktk mipango ya kukatiza maisha ya viumbe vya MUNGU,au kwa njama zako za kupandikiza chuki kwa wana wa Mungu ili tu wewe na wenzio muendelee kuishi ktk Anasa na dhuluma,Maana MUNGU NI WA HAKI!!

Haijalishi ni lini Mungu atajibu lakini sina Shaka kwamba Mungu atajibu na sio kwa haraka lakini polepole kwa USAHIHI.!....Umekua Kinara wa kupanga mipango ya uovu dhidi ya watu wa Itikadi moja na nyingine,lakini Kama MUNGU ANAISHI hataacha kukujibu iwe leo kesho au hata keshokutwa lakini lazima utajibiwa.

Laana hii unayoichuma itaitafuna kizazi chako na kizazi cha watoto wako. Ni muda wako sasa wa kufikiri na kuamua kutubu kwani yeye Mungu ni wa Rehema na kwamba ukitubu ktk Roho na kweli,basi atakusamehe.
Binafsi nimekuwa nikikukosoa sana kwa Siasa zako Chafu na za hila na kutafuta MISIFA huku ukiwagombanisha Watanzania kwa maslahi yako na wenzio.

Wewe ni mkiristo na Biblia inasema wazi kuwa Neno kubwa alilotuachia bwana wetu YESU KRISTO NI UPENDO.! Umepata wapi wewe uwezo wa kupandikiza Chuki kwa watu wa Mungu??

Nikuombe ukae chini utafakari je haya yote unayoyafanya ni kwa "UTUKUFU" wa MUNGU au Wanadamu(CCM)? Ikiwa ndio ni kwa Utukufu wa Mungu basi uendelee,lakini kama sio basi uache na Utubu pamoja na kutotumia tena nafasi na cheo kuwagombanisha wana wa MUNGU.

MUNGU yeye ni wa Rehema na pamoja na wewe kumkosea kwa mambo mengi ikiwemo kusema utatoa ushahidi hadi Mbinguni ukihitajika! Huku ukijua yote unayo yasema ni uwongo, naamini bado atakusamehe!

Nakuombea kwa BABA MUNGU akupe maisha marefu ili siku moja uje ushuhudie haya unayo wafanyia wenzio ukifanyiwa wewe au wanao au wana wa wanao,ikiwa hutabadilika.
Kumbuka kwamba kila Enzi na Zama zake! Hakuna mtu atakae ishi milele kwani hapa hatuna mji udumuo bali tunautafuta ule ujao! Mungu wetu na bwana wetu YESU KRISTO akupe Ufahamu na Ujielewe na kufanya mambo yanayo mtukuza MUNGU na sio shetani.
Mungu akusamehe kwa yote uliyoyafanya unayo yafanya na utakayo yafanya na siku moja uwe mwalimu wa kufundisha na kuhubiri Amani na kuacha kubeza Watu waliopoteza maisha kwa kuwaona kana kwamba wao hawakua na haki ya kuishi ila wewe tu ndie mwenye haki kuishi.

Maisha ni safari na hujui maisha yako ni ya muda gani hapa duniani na hadi hata ufikie kuwa na KIBURI na KUJIAMINI kupita kasi.

Kumbuka MWISHO WA UBAYA SIKU ZOTE NI AIBU.
 
Hakuna cha unyonge ila hakukuwepo na mapepo ya kukemea. Nimeongea kwa lugha ya mazungumzo sio ya kukemea mapepo ya bungeni

Ni vema kufanya siasa kwa manufaa ya watanzania wote,kuliko sifa za kijinga kufurahisha watu wachache co kila unaloagizwa lazima ufanye fikiri kwanza.
 
Kumjadili huyu jamaa ni kupoteza muda, siku zake zinahesabika Mungu hazihakiwi
 
Siku hizi CCM inategemea kuongozwa na Wendawazimu tu.
Hakuna mwenye akili hata mmoja ndani ya CCM anafungua mdomo wake kukemea.
 
ana nja mbya sana ,kifadulo ,mawaya,kichwa cha panzi ,akili ndogo ,watoto hawaendi chooni,baba yake haendi chooni,mama yake haendi chooni ,dada yake pia tu.,sahangazi yake pia tu.
 
Hakuna cha unyonge ila hakukuwepo na mapepo ya kukemea. Nimeongea kwa lugha ya mazungumzo sio ya kukemea mapepo ya bungeni
Wewe Mwigulu Nchemba ni kichwa maji kabisa.
Umekariri kuropoka ujinga mtupu kila mahali. Rudia kusoma ulichokiandika hapo.
Mapepo yamefuata nini hapa?

Ni sisi hapa JF tuliona video hiyo ukitamka maneno kuwa ''Arusha wasipoichagua CCM watakufa'' Njoo na facts kukanusha na sio kuja kuropoka hapa JF
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ni law gani ya newton inayoongelea speed? simtetei Njemba lkn kuhusu hiyo Njia ya Vumbi, all tanzanian their roads are VUMBI's..wewe unakaa Tanzania ipi barabara sio ya vumbi?
Hii dhana potofu ya kudhani Kuwa ukizaliwa Dsm tayari una Phd ya Ujanja na Elimu Dunia itakwisha lini?Kumbuka wamiliki wa Nyumba Masaki Mikocheni mbezi nk kwa 90%si wazaliwa wa Dar
 
Back
Top Bottom