utaifakwanza
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 14,193
- 2,815
MH>MWIGULU LAMECK NCHEMBA AMVAA DR.SLAA NA CHADEMA YAKE,AMUSIHI DR.SLAA AREJEE KUCHUNGA KONDOO WA BWANA KWA SABABU MUNGU ANASEMA HATAKAMA DHAMBI ZAKO NI NYEKUNDU KAMA DAMU,ATAZITAKASA NA KUWA NYEUPE KAMA THERUJI.
AFANIKISHA HARAMBEE YA TSH.MILIONI 19,AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI KWAKE IRAMBA MAGHARIBI.
Naibu katibu mkuu wa CCM na mbunge wa jimbo la Iramba magharibi ameshiriki kikamilifu kwenye harambee ya ujenzi wa kanisa wilaya ya singida Vijijini,kata ya Kijota Usharika wa Mijuhu jimbo la Mashariki Dayosisi ya kati KKKT.
Mbunge huyo amefanikisha upatikanaji wa Tsh.Milioni 19 na laki tisa na themanini.Pia amefakisha upatikanaji wa viti 500 vya plastic kama hatua ya awali katika kufanikisha ujenzi wa kanisa hilo.
Ikumbukwe Mbunge huyo anayevuma kwenye medani za siasa yawezekana kuliko mbunge yeyote kwa sasa hapa nchini,yupo jimboni kwake kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.Jana alianza kwa kufanya vikao vya ndani na madiwani na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.
Pia siku ya jana alitumia kuhamasisha michezo jimboni kwake na wilaya mpya ya Mkalama ambapo Mbunge huyo alishiriki kucheza mechi ya mpira wa miguu akiwa upande wa madiwani.
Kwenye harambee ya leo mbunge huyo Mh.Mwigulu Lameck nchemba madelu alitumia nafasi kuongea na washarika na wananchi wa kata ya kijota,kijiji cha Ikuwi kuwaomba kuachana na tabia ya kulishwa maneno na wanasiasa na viongozi mbalimbali kuhusu serikali yao eti haifanyi kazi.
Amesisitiza kuwa endapo wananchi na viongozi wa vyama vya siasa wangemrudia mungu,wangejikita kusaidia ujenzi wa nyumba za ibada,kushiriki kwenye huduma za kiroho leo hii Tanzania tusingekuwa na aina hii ya viongozi wa vyama vya siasa hasa upinzani wenye uroho wa madaraka,wanaomwaga damu za watanzania ili tu wapate madaraka ndani ya nchi hii.
Mh.Mwigulu nchemba amekwenda mbali zaidi kwa kulaani vikali kauli ya kiongozi wa CHADEMA Dr.slaa yakuwambia viongozi wa dini waache kuombea amani ya nchi.Amesema viongozi kama hao ni wakupuuzwa kabisa kabisa,na niwazi Dr.slaa na chama chake hana nia njema kwa nchi yetu.Ni kwasababu aliachana na misingi ya dini na kiroho ndio maana uwezo wake wa kufikiri kuhusu amani ya nchi ni hafifu kupita kiasi.
Leo Mh.Mwigulu Nchemba ametembelea ujenzi wa barabara mbali mbali ndani ya jimbo lake.Akiwa ameambatana na DC na Mkurugenzi wa wilaya,Mh.Mwigulu Nchemba ameona ujenzi wa barabara kata ya Kidalu barabara inayounganisha wananchi na makao makuu ya wilaya.
Ni barabara inayojengwa na TANROAD kwa kiwango cha changalawe.Pia amezungukia sehemu kadhaa za barabara zinazotajwa kuwa ni korofi kipindi cha masika,lengo likiwa ni kujenga miundombinu safi kabla masika hayajaanza.
Katika kuonesha mshikamano wa kiutendaji uliopo ndani ya jimbo la Iramba,Mbunge huyo aliambatana na madiwani wa kata na makatibu wake pamoja na viongozi wa serikali + Injinia wa wilaya ilikushauriana namna ya kufanikisha ujenzi imara na bora wa miundombinu ya barabara ndani ya jimbo la Iramba.