Mwigulu nae analalamika kwanini usichukue hatua juu ya wauza unga? Inamaana kwani hamuwajui?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AKUTANA NA MAMA MZAZI WA CHID BENZI.
Nimekutana na kufanya mazungumzo na mama wa msanii Rashid Makwilo "Chid Benz" ambaye kwasasa amepatwa na tatizo la Dawa za kulevya.Inasikitisha na haivumiliki kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea huku wauzaji wakinufaika kwa pesa haramu.Ifahamike wazi vita ya serikali dhidi ya magenge, wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya imeongezeka hasa katika awamu hii ya tano chini ya Mh.Rais J.P.Magufuli,hivyo anayejihusisha kwa namna yoyote ni vema akaamua kuachana nayo kabla hajakutwa na mkono wa dola.
Mbali ya vyanzo vya taarifa tulivyonavyo,ni wajibu wa kila aliye RAIA MWEMA kutoa taarifa zitakazo saidia kuangamiza biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Naishukuru familia ya Chid Benz kwa jitihada wanazozifanya kuhakikisha kijana mwenzetu anarejea katika hali yake ya kawaida.
Unaweza kuimba,unaweza kufanikiwa,unaweza kutatua matatizo yako bila kutumia madawa ya kulevya.
 
Mwigulu Nchemba kwa nafasi yake anatakiwa ajipambanue kwa "solutions". Mh. ameaminiwa na uzuri vyombo kama sio chombo cha Usalama wa Raia na mali zao kiko/viko ndani ya mamlaka yake. Akisikia chidi chidi chidbeeenz yuko nganda, jukumu lake ni kufumua kwa UHAKIKA walio nyuma ya madhira. Najua anaweza na mimi nimemkumbusha shujaa huyu wa siasa zijazo. Go Mwigulu, you can.
 
Chid nae aamue moja kwa moja toka moyon kuyaacha watanzania wengi wanamuonea huruma sana
 
Kitwanga alianza na kasi kutaka kubana hao jamaa, naona Mwigulu yupo kimya.
Kama wasingempiga zengwe Kitwanga alishaanza kufanikiwa. Mwigulu naona anawaogopa wasije mfanyia zengwe kama la mwenzie. Lakini kwangu mimi ni bora awamalize hata wakifanya zengwe historia itamkumbuka. Vijana wanateketea jamani.
 
Sidhani kama mwigulu ana hizo guts, huyu wangempeleka wizara yenye mambo ya sera kama alivyokuwa kilimo, kule alikuwa anaft, ila hapo hawezi perform to convincing levels.
 
WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AKUTANA NA MAMA MZAZI WA CHID BENZI.
Nimekutana na kufanya mazungumzo na mama wa msanii Rashid Makwilo "Chid Benz" ambaye kwasasa amepatwa na tatizo la Dawa za kulevya.Inasikitisha na haivumiliki kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea huku wauzaji wakinufaika kwa pesa haramu.Ifahamike wazi vita ya serikali dhidi ya magenge, wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya imeongezeka hasa katika awamu hii ya tano chini ya Mh.Rais J.P.Magufuli,hivyo anayejihusisha kwa namna yoyote ni vema akaamua kuachana nayo kabla hajakutwa na mkono wa dola.
Mbali ya vyanzo vya taarifa tulivyonavyo,ni wajibu wa kila aliye RAIA MWEMA kutoa taarifa zitakazo saidia kuangamiza biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Naishukuru familia ya Chid Benz kwa jitihada wanazozifanya kuhakikisha kijana mwenzetu anarejea katika hali yake ya kawaida.
Unaweza kuimba,unaweza kufanikiwa,unaweza kutatua matatizo yako bila kutumia madawa ya kulevya.
wapi amelalamika wazee wa kupinga kila jambo?
 
Hii kazi namuomba namuomba JPM ampe waziri mkuu anaweza kuwaangamiza Mara moja.lakini wengjne wanaogooana.mungu tusaidie 2017 iwe ni agenda kuu,optn tokomeza madawa ya kulevya.
 
Hii nchi ni ya kipuuzi kweli!!!! Waziri mzima una deal na individual case? Hili baraza la mawaziri la mheshimiwa halina ubunifu kabisa!!! Asilimia kubwa ya mawaziri wake sio wabunifu hata kidogo!!! Kuanzia kinara wao hadi yule wa mwisho kwa umuhimu wote ni kutafuta kiki na kutembea na waandishi Wa habari kama wanaenda kwenye uzinduzi wa miradi!!!!!! Ukienda viwanda hovyo ukija maliasili hoi ukienda nishati sifa tu hamna cha maana ukienda mambo ya ndani ndio hayo mtu anahangaika kushona magwanda utadhani yeye polisi, ukienda afya ndio kichekesho kabisa, ukienda utumishi ndio hata hajui anahangaika na nini! Kutoka tulipo tunahitaji watu wabunifu na watu wenye vision sio hawa wapenda kiki za ovyo!!!!
 
Ubavu wa kuwakamata anautoa wap?kaka mkubwa aliepita alikua na majina yooote pale mjengoni kaondoka nayo yako kwenye mfuko wa shati nadhani unajua kua hakuna aliye tayari kukidhuru kiungo chake cha mwili yeye mwenyewe.
 
kama huyu wazir. mwenye dhamana anakuja na hadithi hizo hizo toka enzi za jk eti tufichue wahalifu ina maana nyinyi na usalama wa tai.. hamuwajui au mnatung'ong'a
nb:mnachoweza ni kudeal na upinzani na wote wanaogusa maslai yenu
 
Back
Top Bottom