Kauli ya Zitto Kabwe kumuunga mkono Mwigulu Nchemba endapo atapitishwa kugombea uraisi na chama chake ni kauli ya kizalendo.
Hapa Zitto alikuwa anaonyesha umuhimu wa vijana kupata nafasi za juu za uongozi wa nchi.
Kauli angeitoa pia Kama angekuwa kwenye mahojiano na Hamis Kigwangala au January Makamba.
Hapa Zitto anaonyesha sasa ni wakati wa vijana kuaminiwa na ndiyo maana Hata yeye alitangaza kugombea uraisi mwaka 2015 endapo katiba ingemruhusu.
Naamini Kama Ukawa itampa nafasi kijana kupeperusha bendera za umoja huo mzalendo Zitto atamuunga mkono moja kwa moja kwa asilimia Mia moja.
2015 ni wakati wa vijana na ni wakati wa mabadiliko ni muhimu kupeleka vijana wengi bungeni Kama itashindikana Ikulu.
View attachment 223292