Mwigulu kujipendekeza to the Maximum, amfate Chalamila

fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
2,165
3,655
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba umeleta taharuki kubwa sana ndani na nje ya nchi, kufuatia kauli yako ya Jana kumsifu kinafiki Rais Mstaafu Jakaya Kikwete. Kwa kauli hii nathubutu kusema haina tofauti na kauli ya aliyekua RC wa Mwanza Mr. Albert Chalamila ambaye uteuzi wake umetenguliwa ukichagizwa na kauli yake ya watu waandikie mabango hata ya matusi ktk kumlaki Rais ziarani Mwanza.

Ni wazi amefanya makusudi kuonyesha kwamba:

1. Mama Samia Suluhu siye anayengoza nchi kama wasemavyo watumiaji wa mitandaoni na hata minong'ono ya baadhi ya wananchi bali ni JK.

Kwamba JK ndio ameshika mpini kwa sasa.

2. Pili kujipendekeza kisiasa kuliko pitiliza baada ya kusoma alama za nyakati huku akitazama Bawa la mama limeelemea upande upi kiuongozi.

3. Muendelezo wa kusifu na kuabudu kama ilivyo ada yake, mtakumbuka enzi za Mwendazake hakuna sifa aliacha toa huku akiitetea serikali iliyopo madarakani hata baada ya uteuzi wake wa waziri wa mambo ya ndani kutenguliwa kabla ya kuja kurudishwa tena

4. Bado ana ndoto ya Urais, na hapa ndo panapomtoaga akili kabisa hivyo yupo tayari kufanya lolote ili tu safari yake isijeishia njiani hivyo anaendelea kuvuta attention.

Maoni yangu, Huyu bwana Mwigulu utawala uchoke sasa kumbeba na kumuonea aibu ikiwezekana atumbuliwe kabisa.

Kwanza IQ yake ndogo sana kiuongozi ktk wizara wizara ya fedha inayohitaji mtu mwenye uwezo wa Hali ya juu.

Pili ni mnafiki wa kiwango cha lami, Hata mama ikitokea bahati mbaya hayupo leo basi ni wazi ataendelea kucheza na fursa tu(KINYONGA) kulingana na mazingira ilimradi aendelee kuteuliwa na kula mema ya nchi hii.

NI BORA CHEO CHA UWAZIRI WA FEDHA KUBAKI WAZI KULIKO KUENDELEA KUWA NA MWIGULU, HAAMINIKI KABISA HUYU MTU.
 
Na Maza ndio kampa wizara ya fedha.Kati ya watu hakufaa,hafai ni huyu Mwigulu...ni chawa ndani ya Sufi

Na kati ya makosa ya awamu hii ni kuendelea kutumia watu kama Mwigulu,ashukuru serikali inababaikia MTU akishajiita Dr

Mwigulu is smart that is the reason he had to invoke Kikwete in his speech as a way of putting his house close to power!!! He is a dangerous dude!!!
 
Anatumia fursa,kutukuza kwake kunamlipa.Alimsifia jiwe kesho akapewa teuzi.
Aliwajibu wapinzani eti mnataka raisi atoke Chato aje mjini kupambana na corona kwani raisi ni nesi.Kesho tu akapewa teuzi.
Kwa hiyo akivaa skafu weye unajisikia uchungu?Hebu acheni upukunusi.😂😂😂😂
 
Mwigulu is smart that is the reason he had to invoke Kikwete in his speech as a way of putting his house close to power!!! He is a dangerous dude!!!

Mwigulu ni mroho wa madaraka na mnafiki pia.

He knows how to play mind games so as those in power to see him for appointments, he is a sycophant of higher grade, he can self humiliate for posts.
 
Na Maza ndio kampa wizara ya fedha.Kati ya watu hakufaa,hafai ni huyu Mwigulu...ni chawa ndani ya Sufi

Na kati ya makosa ya awamu hii ni kuendelea kutumia watu kama Mwigulu,ashukuru serikali inababaikia MTU akishajiita Dr
Hafai kabisa hata hyo wizara kwake ni mbingu na ardhi
 
Back
Top Bottom