Kwa imani ya dini yangu, nimefundishwa kwamba sitakiwi kulipa kisasi! Si vizuri kufunga ili umuombe Mungu amwadhibu binadamu mwingine. Hakuna mkamilifu chini ya jua, hivyo ni vizuri tukaombeana mema.
Tunatakiwa kufunga na kusali Mungu awape huruma wale walio kwenye mateso! Awape ujasiri na uwezo wa kupambana na magumu yanayowasibu.
Pia, tumuombe Mungu abadili moyo wa Bwana Mkubwa uliyemtaja kuhusika na mateso ya hao vijana. Awe na moyo wa ubinadamu na huruma. Chuki, kisasi na tamaa ya madaraka viondoke katika moyo wake.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Wewe,
Pharao alikuw na roho ngumu ya kutokuamini na kumtii Mungu, aliendelea kuwafuatilia Israel hadi alipopoteza jeshi lake lote. Waliangamia kwa ajli ya utii wako kwa farao aliyekuwa akinyanyasa Israel. Farao asiyemjua Yusuph, ccm isiyokuwa na uchungu wa taifa la Tanzania.
Nabii Elijah alipokuwa kwenye kilima, mfalme Ahabu alituma majeshi ili wamkamate, Elia aliagiza moto ukashuka na kuwateketeza wale majeshi ya Ahabu. Ahabu alitumikia miungu ya Baali.
Nabii Elisha alipokuwa amebaki baada ya kupaa kwa Elijah, wale wana wa manabii walimdhihaki wakisema "paa wewe mwenye upaa", Elisha aliagiza dubu wakawamaliza.
Yesu na yule mwenye pepo ziitwazo :legion" sijui kama nimeandika sahihi ama "jeshi" aliruhusu zile pepo ziingie kwa nguruwe na wale nguruwe na pepoe zao wakaishia majini.
MUNGU HANA KANUNI MOJA YA KUTETEA WATU WANAOTESWA. Kama mtu anaendelea kufuga roho chafu katika moyo wake, na anaendelea kumtumikia shetani huku akinyanyasa watu wa Mungu, Mungu halazimishwi kumtenganisha na hiyo roho. Wala hana kanuni moja.
IMANI YETU IMEJENGWA JUU YA MITUME NA MANABII. TUTAMWOMBA MUNGU NA NAMNA ATAKAVYOSHUGHULIKA NA AKINA NCHEMBA NA SYNDICATE YAKE YOTE, ANAJUA YEYE. SISI HATUWEZI KUMCHAGULIA. TUNACHOTAKA UDHALIMU HUU UKOME MARA MOJA NA MILELE.
SASA NI MUDA WA WACHAWI WOTE, WASHIRIKINA, WENYE VIBURI, FITINA, UWONGO NA HILA ZA KILA NAMNA, KUMTAMBUA NA KUKIRI KWAMBA, KWELI YUKO MUNGU ANAYEISHI NAYE NI MUNGU WAA MILELE WALA HAKUNA MWINGINE.
SAWA NA PHARAOH ALIVYO KIRI KWAMBA "GOD OF MOSES IS GOD"
THIS IS REAL, LET THE CHURCH SAY "ENOUGH IS ENOUGH, WE ARE NOW TAKING OUR POSITIONS IN THE SPIRITUAL REALM".
GOD BLESS TANZANIA.