Mwigulu, CCM hili mnalijua kweli?

Mwigulu, CCM hili mnalijua kweli?

Fisadidagaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
962
Reaction score
235
Ndugu wana jamvi,
Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia siasa zetu,na matukio yanayojitokeza kila siku nchini,hasa kwa vyama hivi viwili, TAWALA(ccm) na UPINZANI(Chadema),

Sasa hivi kuna matukio yanafanyika mpaka unajiuliza kuwa kuna SERIKALI Kweli katika nchi hii,na kama ipo mbona kimya? Watu wana uwawa, wanatekwa na kuteswa, mikataba hovyo, ardhi inauzwa kwa kisingizio cha uwekezaji, Rasilimali kama madini, mafuta na gesi wanajimilikisha wachache, Elimu bomu, hospitali hakuna kama ipo madawa hakuna ,wanyama wanaisha, deni la taifa linakua kila uchwao na hakuna wakusema pesa zimeenda wapi, maofisa wa Ikulu nao wanapiga dili safari za rais na mengine mengi, ila serikalini hakuna anayefanya tendo la kuthubutu hata kumfunga paka kengele.

Hapa sasa ndiyo nikasema niipitie kidogo katiba ya Chama tawala nione labda kuna kipengele kinachoruhusu yote hayo na mengine mengi.

Lakini sasa chakushangaza hata kabla ya kufika mbali na kuisoma kwangu nakutana na haya.

KATIBA YA CCM.
SEHEMU YA KWANZA.
Aya 4;CCM Inaamini kuwa.
1;BINADAMU WOTE NI SAWA.
2;KILA MTU ANASTAHILI HESHIMA NA KUTAMBULIWA NA KUTHAMINIWA UTU WAKE.
3;UJAMAA NA KUJITEGEMEA NDIYO NJIA PEKEE YA KUJENGA JAMII YA WATU WALIO SAWA NA HURU.

Unaweza kuisoma katiba hii ya ccm Sehemu ya kwanza tu kuanzia namba 1 hadi 19, na ukahisi kuwa viongozi wa serikali hawajui katiba ya chama chao,maana wangekuwa wanaijua naamini wangeisimamia kama siyo kuilinda.

Labda niwakumbushe Mwigulu na CCM kuwa, katiba hiyo hiyo,

NYONGEZA "A"
AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI(CCM).
1;Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.
2;Nitatumikia nchi yangu na watu wake wote.
3;Nitajitolea nafsi yangu kuondoa UMASKINI,UJINGA,MAGONJWA na DHULUMA.
4;RUSHWA ni adui wa HAKI,sitopokea wala kutoa RUSHWA.
5;Cheo ni dhamana,sitatumia cheo changu,wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
6;Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.
7;Nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.
8;Nitasema UKWELI DAIMA,FITINA kwangu MWIKO.
9;Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na Raia mwema wa Tanzanania na Afrika.

Mimi.
Kama kweli sijakosea haya maandishi yanatoka kwenye katiba ya CCM, mbona hawayasimamii? Au hawajui kama yapo? Au wanajisahaulisha?

NB.
Ni mara ya kwanza kwangu kuweka mada jamvini, ushauri kukosoa maoni kwa wenye mapenzi mema na nchi hii, nawasilisha.
 
Ukiwaona akina Kwigulu povu linawatoka ni kwa ajili ya hiyo ndg yangu.Wamehama kabisa nje ya mwelekeo wa chama chao na hawana namna ya kujitetea ila kuanza kusingizia video za kigaidi ili kuhamisha maswala muhimu ya nchi yetu tubakie kujibizana huku jamvini habari za ugaidi.Yeye mwenyewe Mwigulu wakati wa EPA alikuwa benki kuu sina hakika kama hakuwa part&parcel of the whole EPA scandal.Utawaona watakavyotujia juu humu jamvini.
 
wanaotoboa macho,kutoa kucha,kubana mbavu na kuvunja,kung'oa meno na nk ni wanausalama wa chadema ambao slaa anadai wako makini kuliko tiss.kwa sababu tiss tulikuwa nao tangu zamani na hayamambo hayakuwepo yameanza pale rwakatale alipo teuliwa
 
Hawatatokea hapa kwani wao wako huku jamvini kushambulia cdm na wamenunuliwa wengi sana.
 
Hayo unayajua wewe na wengine lakini ccm walisha badili kabisa mwelekeo
 
Wanachama wengi ni wale waliopatikana kwa njia ya Vodafaster. Unategemea hao wasome Katiba saa ngapi?
 
nape na mwigulu hawajui hata ccm inakatiba..wao wanazo zakwao kichwani....
 
Ukiwaona akina Kwigulu povu linawatoka ni kwa ajili ya hiyo ndg yangu.Wamehama kabisa nje ya mwelekeo wa chama chao na hawana namna ya kujitetea ila kuanza kusingizia video za kigaidi ili kuhamisha maswala muhimu ya nchi yetu tubakie kujibizana huku jamvini habari za ugaidi.Yeye mwenyewe Mwigulu wakati wa EPA alikuwa benki kuu sina hakika kama hakuwa part&parcel of the whole EPA scandal.Utawaona watakavyotujia juu humu jamvini.

Kwanza nimesikia malalamishi juu ya huyu mwingulu mchemba kwa wabunge na watu wa kawaida kwamba huyu jamaa ananuka mdomo, so huenda akipiga mswaki hasugui ulimi, au ana tatizo la kunuka mdomo.so ajipime mwenyewe ajirekebishe.
 
wanaotoboa macho,kutoa kucha,kubana mbavu na kuvunja,kung'oa meno na nk ni wanausalama wa chadema ambao slaa anadai wako makini kuliko tiss.kwa sababu tiss tulikuwa nao tangu zamani na hayamambo hayakuwepo yameanza pale rwakatale alipo teuliwa

Hapa una 7, 000 yako saafi....
 
AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI(CCM).
1;Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.
2;Nitatumikia nchi yangu na watu wake wote.
3;Nitajitolea nafsi yangu kuondoa UMASKINI,UJINGA,MAGONJWA na DHULUMA.
4;RUSHWA ni adui wa HAKI,sitopokea wala kutoa RUSHWA.
5;Cheo ni dhamana,sitatumia cheo changu,wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
6;Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.
7;Nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.
8;Nitasema UKWELI DAIMA,FITINA kwangu MWIKO.
9;Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na Raia mwema wa Tanzanania na Afrika.

.
Hizi zilikuwa ahadi za mwana TANU under the late Mwalimu. Kwa sasa ni umafia-mafia, undava - undava - survive for your own fitness, huwezi umeumia.
 
wanaotoboa macho,kutoa kucha,kubana mbavu na kuvunja,kung'oa meno na nk ni wanausalama wa chadema ambao slaa anadai wako makini kuliko tiss.kwa sababu tiss tulikuwa nao tangu zamani na hayamambo hayakuwepo yameanza pale rwakatale alipo teuliwa
hayakuwepo au ulikuwa hujui!?
kama ni siasa nadhani umeanza juzi tu lakini unadhani unafahamu kila kitu..punguza spidi mdogo wangu hii nchi ina mengi mazito na wewe ni mtoto kuweza kutambua, jiulize kwanini ccm ilisaidia ukombozi nchi nyingine za afrika na waliwezaje? Unadhani hawatumii mbinu hizo kujilinda wanapohisi hali inakuwa ngumu kwao? Ni mbinu gani hizo?
kalagabaho!
 
Nafikiri hizo ahadi ziko katika toleo la kwanza enzi za Mwalimu. Naomba mwenye Azimio la Zanzibar atuwekee hapa tuone kama bado zinakubalika.
 
Kwenye hiyo katiba yao mbona hakuna kile kipengele kinachosema ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI WA CCM?
 
Hapa una 7, 000 yako saafi....

saiv nadhan watakuwa wameongezewa posho sio chin ya elfu 20 ukitoa overtime maana wana juhud sana humu ndan...kama bado hawajaongezewa wanajioverwork
 
wanaotoboa macho,kutoa kucha,kubana mbavu na kuvunja,kung'oa meno na nk ni wanausalama wa chadema ambao slaa anadai wako makini kuliko tiss.kwa sababu tiss tulikuwa nao tangu zamani na hayamambo hayakuwepo yameanza pale rwakatale alipo teuliwa

Mkuu.

Kwenye mnakasha wa moto kama huu usitegemee kuwakuta wale jamaa kina Ritz. Wao wameambia "Nendeni JF mkajibu mapigo" hivyo vifungu vya katiba wao hawavijui.
 
Last edited by a moderator:
Fisadidagaa.....jina lako linaoonekana kuwa baadae utageuka kuwa fisadipapa.
 
Mkuu umejisahau, CCM unayoisema wewe alikufa nayo Mwalimu Nyerere.Hawa waliobaki wanaimba chukua chako mapema!
 
Ndugu wana jamvi,
Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia siasa zetu,na matukio yanayojitokeza kila siku nchini,hasa kwa vyama hivi viwili, TAWALA(ccm) na UPINZANI(Chadema),

Sasa hivi kuna matukio yanafanyika mpaka unajiuliza kuwa kuna SERIKALI Kweli katika nchi hii,na kama ipo mbona kimya? Watu wana uwawa, wanatekwa na kuteswa, mikataba hovyo, ardhi inauzwa kwa kisingizio cha uwekezaji, Rasilimali kama madini, mafuta na gesi wanajimilikisha wachache, Elimu bomu, hospitali hakuna kama ipo madawa hakuna ,wanyama wanaisha, deni la taifa linakua kila uchwao na hakuna wakusema pesa zimeenda wapi, maofisa wa Ikulu nao wanapiga dili safari za rais na mengine mengi, ila serikalini hakuna anayefanya tendo la kuthubutu hata kumfunga paka kengele.

Hapa sasa ndiyo nikasema niipitie kidogo katiba ya Chama tawala nione labda kuna kipengele kinachoruhusu yote hayo na mengine mengi.

Lakini sasa chakushangaza hata kabla ya kufika mbali na kuisoma kwangu nakutana na haya.

KATIBA YA CCM.
SEHEMU YA KWANZA.
Aya 4;CCM Inaamini kuwa.
1;BINADAMU WOTE NI SAWA.
2;KILA MTU ANASTAHILI HESHIMA NA KUTAMBULIWA NA KUTHAMINIWA UTU WAKE.
3;UJAMAA NA KUJITEGEMEA NDIYO NJIA PEKEE YA KUJENGA JAMII YA WATU WALIO SAWA NA HURU.

Unaweza kuisoma katiba hii ya ccm Sehemu ya kwanza tu kuanzia namba 1 hadi 19, na ukahisi kuwa viongozi wa serikali hawajui katiba ya chama chao,maana wangekuwa wanaijua naamini wangeisimamia kama siyo kuilinda.

Labda niwakumbushe Mwigulu na CCM kuwa, katiba hiyo hiyo,

NYONGEZA "A"
AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI(CCM).
1;Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.
2;Nitatumikia nchi yangu na watu wake wote.
3;Nitajitolea nafsi yangu kuondoa UMASKINI,UJINGA,MAGONJWA na DHULUMA.
4;RUSHWA ni adui wa HAKI,sitopokea wala kutoa RUSHWA.
5;Cheo ni dhamana,sitatumia cheo changu,wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
6;Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.
7;Nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.
8;Nitasema UKWELI DAIMA,FITINA kwangu MWIKO.
9;Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na Raia mwema wa Tanzanania na Afrika.

Mimi.
Kama kweli sijakosea haya maandishi yanatoka kwenye katiba ya CCM, mbona hawayasimamii? Au hawajui kama yapo? Au wanajisahaulisha?

NB.
Ni mara ya kwanza kwangu kuweka mada jamvini, ushauri kukosoa maoni kwa wenye mapenzi mema na nchi hii, nawasilisha.

hizo kanuni 9 hakika ukiwaeleza wana ccm utangombana nao maana wao walisharekebisha na kuwa na kanuni zifuatazo
1. uongo 2. ufisadi 3. matusi 4. kupanga kudhuru watanzania wenzao haswa wanaoingilia maslahi yao 5. kunyanyasa wanachi kwenye maeneo yao kwa kuwamilikisha wageni ardhi 6. kuteteana hata kwenye mambo ya kipuuzi ya siyo leta maendeleo kwa taifa (elimu sio muhimu kwa taifa) 7. kupenda kusifia nchi za magharibi na kuweka hela nje ya nchi bila kusahahu kusafiri kila kukicha 8. kuingia mikataba isiyo na faida kwa taifa bali kwa viongozi tu na kundi ndogo la wafuasi 9. kuziba masikio na kuendelea kuamini watakuwa kwenye dola milele na milele.
 
Back
Top Bottom