Ndugu wana jamvi,
Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia siasa zetu,na matukio yanayojitokeza kila siku nchini,hasa kwa vyama hivi viwili, TAWALA(ccm) na UPINZANI(Chadema),
Sasa hivi kuna matukio yanafanyika mpaka unajiuliza kuwa kuna SERIKALI Kweli katika nchi hii,na kama ipo mbona kimya? Watu wana uwawa, wanatekwa na kuteswa, mikataba hovyo, ardhi inauzwa kwa kisingizio cha uwekezaji, Rasilimali kama madini, mafuta na gesi wanajimilikisha wachache, Elimu bomu, hospitali hakuna kama ipo madawa hakuna ,wanyama wanaisha, deni la taifa linakua kila uchwao na hakuna wakusema pesa zimeenda wapi, maofisa wa Ikulu nao wanapiga dili safari za rais na mengine mengi, ila serikalini hakuna anayefanya tendo la kuthubutu hata kumfunga paka kengele.
Hapa sasa ndiyo nikasema niipitie kidogo katiba ya Chama tawala nione labda kuna kipengele kinachoruhusu yote hayo na mengine mengi.
Lakini sasa chakushangaza hata kabla ya kufika mbali na kuisoma kwangu nakutana na haya.
KATIBA YA CCM.
SEHEMU YA KWANZA.
Aya 4;CCM Inaamini kuwa.
1;BINADAMU WOTE NI SAWA.
2;KILA MTU ANASTAHILI HESHIMA NA KUTAMBULIWA NA KUTHAMINIWA UTU WAKE.
3;UJAMAA NA KUJITEGEMEA NDIYO NJIA PEKEE YA KUJENGA JAMII YA WATU WALIO SAWA NA HURU.
Unaweza kuisoma katiba hii ya ccm Sehemu ya kwanza tu kuanzia namba 1 hadi 19, na ukahisi kuwa viongozi wa serikali hawajui katiba ya chama chao,maana wangekuwa wanaijua naamini wangeisimamia kama siyo kuilinda.
Labda niwakumbushe Mwigulu na CCM kuwa, katiba hiyo hiyo,
NYONGEZA "A"
AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI(CCM).
1;Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.
2;Nitatumikia nchi yangu na watu wake wote.
3;Nitajitolea nafsi yangu kuondoa UMASKINI,UJINGA,MAGONJWA na DHULUMA.
4;RUSHWA ni adui wa HAKI,sitopokea wala kutoa RUSHWA.
5;Cheo ni dhamana,sitatumia cheo changu,wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
6;Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.
7;Nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.
8;Nitasema UKWELI DAIMA,FITINA kwangu MWIKO.
9;Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na Raia mwema wa Tanzanania na Afrika.
Mimi.
Kama kweli sijakosea haya maandishi yanatoka kwenye katiba ya CCM, mbona hawayasimamii? Au hawajui kama yapo? Au wanajisahaulisha?
NB.
Ni mara ya kwanza kwangu kuweka mada jamvini, ushauri kukosoa maoni kwa wenye mapenzi mema na nchi hii, nawasilisha.
LAZIMA TUJILAUMU WATANZANIA KAMA TUNGEKUWA MAKINI CCM ISINGETUFIKISHA HAPA TULIPO.SISI WATZ PAMOJA NA MIMI LAZIMA TUBADILI FIKRA ZETU ILI TUONDOKANE NA KERO HIZI ZA KUDUMU.
NI MTANZANIA GANI ASIYEJUA HAYA YANAYOTUTESHA KILA SIKU huku mafisadi wakipiga makofi tu kupitisha mambo haya haya kila siku.???????????????
1.HALI NGUMU YA MAISHA nauli/kodi juu wakati kipato ni kile kile
2.HUDUMA ZA AFYA MBAYA.DAWA hakuna zikiwepo zaenda kwa hospital binafsi.
3.UBINAFSI WA VIONGOZI WETU -Kujilimbikizia mali kila mahali.Kufa kufaana
4.UFISADI -Dowans na Richmond
5.MIKATABA MIBOVU.Idara za madini na mali asili
6.KULINDANA KUNAKOLETA VIONGOZI WABOVU.Watoto wa vigogo kila penye idara nyeti nenda TRA,BOTn.k
7.UTAPANYAJI WA MALI NA RASILIMALI ZA UMMA.Magari ya umma kwa issue binafsi
8.KUONGEZEKA KWA TABAKA LA WALIONACHO NA WASIONACHO.Tajiri na masikini
9.KUTUMIA RASILIMALI ZA NCHI KUENEZA PROPAGANDA NA CHUKI.
10.UKOSEFU WA AJIRA.64% ya wahitimu ni jobless
11.VIWANDA VINGI KUFA NA KUFANYWA MAGOFU.
12.UKOSEFU WA HAKI KWENYE VYOMBO VYA MAAMUZI MFANO MAHAKAMA.
13.MIGOGORO KILA KONA HASA YA ARDHI ,WAWEKEZAJI KWANZA MZAWA BAADAYE..loliondo,kiteto n.k
14.MIFUMO MIBOVU YA UONGOZI HIVYO KUSABABISHA MZIGO MKUBWA KWA SERIKALI mfano vyeo vya ajabu tu kila
kona.
15.SIASA CHAFU HASA KWENYE MASUALA YA MSINGI MFANO MAJI AMBAYO NI ISSUE MUHIMU TEMBELEA SHY
TOWN,NZEGA,TABORA YOTE,SIMIYU,MPANDA KWA PINDA,DODOMA,DSM,MANYARA,GEITA ,BUNDA,N.K HAKUNA MAJI.
16.UJAMBAZI ULIKITHIRI WA RASILIMALI ZA TAIFA MFANO WANYAMA KUTOROSHWA.
17MASHULE KIBAO ,VITENDEA KAZI HAKUNA.