hakuna jipya. inasikitisha sana. yaani unazunguka nchi nzima unazungumzia mshikamano leo? tanzania inamatatizo yanayohitaji viongozi wenye utashi wa kuyatatua na si kuomba mshikamano kwani bado hauwasaidii wananchi hata kidogo. hebu viongozi wetu mnaopewa dhamana ya uongozi jaribuni kujifunza dhana kamili ya uongozi kwa maana pana zaidi na kuwaongoza watz katika haki, kweli, sheria bila upendeleo na ushirikishi wa pamoja kwa uwazi katika kupanga, kusimamia, kutekeleza na kupitia upya mara kwa mara miradi ya maendeleo ya jamii husika. iwe ni ya elimu, afya, uchukuzi, maji na uzalishaji mali kwa kutumia rasilimali tulizonazo kwa faida ya watz. tuache siasa za zamani.