Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,768
- 3,621
Nimefanya ziara ya siku moja kukagua mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa ya ranchi ya Taifa ya Ruvu.Ujenzi wa ranchi hii ulianza mwaka 2010 hadi hii leo haujakamilika kutokana na uzembe,kukosa uzalendo kwa baadhi ya watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia mali hii ya Umma.
Kutokana na usimamizi,ushauri na kutoa kujali thamani hii ya mali ya umma ya Watanzania nimechukua hatua za awali:
Kwanza, nimewasimamisha kazi wakurugenzi wote wa bodi ya (NARCO) kampuni ya usimamizi wa ranchi za Taifa kwa kushindwa ama kwa maksudi au vinginevyo kusimamia ujenzi wa machinjio haya ya kisasa.Bodi hii imesababisha Taifa lipoteze Billion 5.7 zilizotolewa kwaajili ya ujenzi wa hatua za awali za machinjio haya.
Pili,nimesitisha kuendelea kwa kazi kwa mkurugenzi wa ranchi za Taifa kwa kushindwa kusimamia mradi huu ulioliingizia Taifa hasara ya Bilion 5.7
Tatu, nimeagiza ndani ya siku 7 kupitia wataalam wa wizara wahakikishe inaletwa ripoti ya thamani ya fedha inayohitajika kumalizia ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa
Mwisho, kupitia vyombo vya sheria, nimeagiza wahusika wote walioshiriki kuliingizia Taifa hasara hii wanafikishwa mahali stahiki kwaajili ya hatua za kinidhamu.
Rai yangu kwa watumishi wote wanaopewa dhamana ya kusimamia mali ya umma, wasimamie kwa uzalendo na kwa ufanisi ili kuisaidia nchi yetu kusonga mbele.