Mwigulu apigilia msumari agizo la Rais Magufuli kuhusu mimba shuleni na Ushoga

"...hii dunia Licha ya ubaya ama uzuri wa jambo wote hatuwezi kuwa sawa.... "
 
Waziri Nchemba amesema kama kuna taasisi yoyote imesajiliwa nchini na inafanya kampeni za haki za ushoga basi atafuta usajili huo na watu wake kukamata na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Wanaotaka haki za ushoga watafute tu nchi yao nyingine ambayo inaruhusu mambo hayo wakakae huko, kama ni taasisi imesajiliwa kwenye nchi yetu tukaigundua inafanya kampeni ya haki hizo na bahati nzuri zinasajiliwa Wizara ya Mambo ya Ndani nitazifutia usajili wao…

…..na kama ni raia wa Tanzania anaendesha kampeni hizo tutamkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria, na kama si raia amekuja kwenye nchi yetu kuja kuendesha haki hizo tutampa amri ya kuondoka ndani ya nchi yetu hatapata fursa hata ya kuchomoa chaji ya simu kwenye soketi ya umeme” amesema Nchemba.

Kwa upande mwingine Waziri Nchemba amemuunga mkono kauli ya Rais Magufuli dhidi ya wanafunzi ambao watapata ujauzito wakiwa shuleni na kusema watu wanaopinga jambo hilo wasitumie nguvu kubwa kupinga bali wajenge shule zao wao watoe hiyo haki ya kusomesha wanafunzi wajawazito au wale ambao tayari wamejifungua na siyo kulazimisha serikali kufanya hayo.
.
HON. MWIGULU, GOOD ENDS MAY NEVER JUSTIFY EVIL MEANS....

Kanisa Katoliki lilipoona limeshindwa kutetea uhalali na usahihi wa hoja kwamba "kila tendo la ngono linapaswa kuheshimu haki ya kila spematozoa kuingia katika tumbo la uzazi la mwanamke ili kurutubisha ovamu inayoweza kuwepo huko ndani (Humanae Vitae of 25 July 1968, No.11)," likaamua kufanya propaganda hasi kwa yeyote anayepinga fundisho hilo.

Kwa sababu hii likadai kwamba mapenzi ya mdomo, mapenzi ya vidole, mapenzi ya mapajani, punyeto, ni mapenzi yaliyo kundi moja na mapenzi ya rektamu (anal sex). Yaani ni matendo yanayovunja haki ya spematozoa kuingia katika tumbo la uzazi la mwanamke ili kurutubisha ovamu inayoweza kuwepo huko ndani!

Hivyo, likajenga hoja kuwa, yeyote anayepinga fundisho lake anauunga mkono ushoga au ni shoga. Likatumia kanuni ya propaganda hasi yenye msingi wake katika "fallacy of association" kueneza kwa mabavu mafundisho yake batili. Huu ni umachiavelli na ni UOVU.

Na kwa sababu hii, likasahau kujipanga kwa ajili ya kuandaa "a theology of people with disability," wakiwemo the lame, blind, deaf, cripples, albinos, she-male catholics, hermaphrodite catholics, blind catholics, deaf catholics, etc. Hapa Tanzania wapo wengi, na tatizo lao sio la kipolisi kama Rais Magufuli, Mwigulu, Kigwangala na Ummy Mwalimu wanavyofikiri.

Wakiambiwa kuwa, "kwa vile Mungu ni muumba wa vitu vyote, na kwa vile walemavu wa kizaliwa ni wengi, basi Mungu huyo hakumuumba mwanamke na mwanamume pekee, bali na hawa walemavu pia", wanashikwa na kigugumizi.

Nina tatizo na wanateolojia wa Kiafrika pia. Wamebaki kuwa Kasuku wa maneno ya wamisionari waliokuja Tanzania miaka 150 iliyopita--"Male and female created he them (Gen 5:2)," no less no more! Hata kusoma soma Biblia tena ili waweze hata kubuni teolojia ya ulemavu ili uwe mchango wao wa kiteolojia mbali ya ule ulioletwa na Wazungu, wapi! Wanaishia kumpa jukwa Mwigulu alichafue Kanisa...

Sasa Kanisa Katoliki limewafundisha JPM na Mwigulu kutumia mbinu ile ile. Wanalazimisha watu wakubali marufuku dhidi ya wanafunzi wazazi na wanafunzi wenye mimba. Ukipinga unaambiwa unaunga mkono ngono za utotoni au unaunga mkono ushoga au ni shoga. Wanasahau kwamba Tanzania ya leo sio ile ya "ndio mzee." Nimeanza kupata mashaka kuhusu umakini wa Rais Magufuli, ambaye kimsingi ni msomi wa ngazi ya juu kabisa--PHD holder...
 
Back
Top Bottom