Mwigulu apigilia msumari agizo la Rais Magufuli kuhusu mimba shuleni na Ushoga

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,315
2,000
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amezionya taasisi zisizo za Serikali zinazohamasisha kudai haki ya mtoto anayepata mimba kurejeshwa shuleni kuacha mara moja na zikiendelea atazifutia usajili.

Mwigulu ameyasema hayo leo, Jumapili wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Parokia ya Kisasa Mjini hapa.

Amesema Serikali haitaomba ushauri wala maoni kwa sababu maelezo yaliyotolewa na Rais, John Magufuli ni maagizo ya Serikali.
Waziri huyo amesema Serikali imetoa haki ya kila mtoto kupata elimu kwa kuifanya kuwa bure kwa hiyo atakayeikosa asitafute kisingizio.

pic%2Bmwigulu.jpg

"Rais ametoa haki hiyo sasa hivi elimu ni bure, halipi tuition wala nini, atakayeamua kuachana na haki hiyo asitafute kisingizio, asipeleke lawama kwa Serikali, "amesema.

=====

HOTUNA YA MWIGULU NCHEMBA AKIZUNGUMZA WAKATI WA HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA KANISA KATOLIKI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YESU, PAROKIA YA KISASA MJINI DODOMA 25 juni 2017
“Maoni ya watu tofauti tofauti, wengine wanasema mbona Rais sasa anakuwa mkali? Father (Padre) na wewe leo utatwambia. Hivi kumeishabadilika siku hizi kiasi kwamba mapepo yanakemewa kwa upole, kwamba “shetani toka basi, toka basi.” Shetani anakemewa kwa ukali tena kwa mamlaka.

“Niliona hata juzi hivi, Rais alipokuwa katika ziara, bahati nzuri MC wetu nilimwona kwa macho yangu kule Bagamoyo, wakati Rais anaongelea mimba kwa wanafunzi. Watanzania kwa vile tunapenda debate (mjadala), hilo nalo tumeanza kuona kwamba ni debate (mjadala). Yaani, hata maelekezo tunadhania kwamba nayo ni debate.

“Na wengine wanaosema hivyo ni waumini. Na wengine wanao… wanaopigia kampeni mimba za wanafunzi nao ni waumini. Mimi ninatafuta sana Biblia gani wanayoisoma, ambayo imeisharuhusu wanafunzi wapate mimba. Kwa imani yangu, na kwa mujibu wa maandiko yote ninayoyapitia, kwanza yanazuia mimba nje ya ndoa. Na yote yanazuia ndoa za utotoni. Waumini wenzetu ambao wanatokea na wanaona mimba zihalaishwe tu katika rika la wanafunzi, wanasoma kitabu kipi?

“Na wengine ni akina mama. Hayo malezi ambayo tunataka kuruhusu wanafunzi wafanye tu mambo hayo, msingi wakeo uko… unatokana na nini? Kwa hiyo, mimi namuunga mkono Mhe. Rais kwa asilimia 100 zote. Ameongelea mambo makubwa mawili.

“Moja likiwa hilo la mimba, lakini la pili likiwa la mambo ya ushoga. Hili la mimba linaletwa kwa ka-kivuli hako hako ka haki, na la ushoga linaletwa kwa ka-kivuli hako hako ka haki.

“Wanaotaka haki za ushoga wakatafute hiyo nchi ambayo wanaruhusu mambo hayo, basi wakakae huko. Kama ni taasisi imesajiliwa kwenye nchi yetu, tukaigundua inafanya kampeni ya haki hizo, na bahati nzuri zinasajiliwa Wizara ya mambo ya ndani, nitazifutia usajili wao.

“Na kama ni raia wa Tanzania anaendesha kampeni hiyo tutamkamata na tutamfikisha kwenye vyombo vya sheria. Kama si raia, amekuja kwenye nchi yetu kuja kuendesha kampeni ya haki hizo, kama kwao wanaabudu hayo mambo ya ushoga, akaamua kuja kuendesha kampeni ya haki hizo, tutampa amri ya kuondoka ndani ya nchi yetu. Hatapata fursa hata ya kuchomoa charger (chaja) kwenye soketi ya umeme. Hatutaruhusu hayo.

“Na mheshimiwa Rais ameelekeza vizuri, kama kuna watu wanatumia kigezo hicho cha haki, badala ya kutumia nguvu kubwa kuilazimisha serikali, wao na wajenge shule zao, watoe hiyo haki.

“Lakini, serikali haiwezi ikaruhusu utaratibu huo. Mwalimu anakwenda darasani anakuta wanafunzi wote wako maternity leave (likizo ya uzazi). Kwa mimi ninayesimamia idara ya utekelezaji wa maelekezo, nizionye taasisi zote zilizokuwa zinafanya kampeni hizi. Watafute shughuli zingine za kufanya.

“Kama watadhania kuwa maelekezo ya Mhe. Rais yalikuwa ni public hearing (jukwaa la kupokea maoni ya umma), ni ajenda ya kuzua mjadala, nitazifutia usajili taasisi zote hizo. Haya ni maelekezo, aliyotoa Mhe. Rais ni maelekezo, sio ajenda ya mjadala. Sio debate (mjadala). Na kwenye hilo hatukusanyi ushauri wala hatukusanyi maoni.

“Huo ndio msimamo wa serikali. Hakuna ushoga. Hakuna mimba kwa wanafunzi. Hakuna maternity leave (likizo ya uzazi) kwa wanafunzi. Na wanaosema haki ya elimu kwa kila mtoto, serikali tayari imetoa haki ya elimu kwa kila mtoto. Ndio maana Mhe. Rais anasomesha watoto bure, ili haki hiyo kila mtoto apate.”
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,744
2,000
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amezionya taasisi zisizo za Serikali zinazohamasisha kudai haki ya mtoto anayepata mimba kurejeshwa shuleni kuacha mara moja na zikiendelea atazifutia usajili.

Mwigulu ameyasema hayo leo, Jumapili wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Parokia ya Kisasa Mjini hapa.

Amesema Serikali haitaomba ushauri wala maoni kwa sababu maelezo yaliyotolewa na Rais, John Magufuli ni maagizo ya Serikali.
Waziri huyo amesema Serikali imetoa haki ya kila mtoto kupata elimu kwa kuifanya kuwa bure kwa hiyo atakayeikosa asitafute kisingizio.

View attachment 530362
"Rais ametoa haki hiyo sasa hivi elimu ni bure, halipi tuition wala nini, atakayeamua kuachana na haki hiyo asitafute kisingizio, asipeleke lawama kwa Serikali, "amesema.
Sawa kabisa badala yake NGO hizo zihamasishe wanaume kutotembea na wanafunzi ili mabinti wetu wawe Salama wasipate mimba au ukimwi
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,130
2,000
Moja ya watu ambao hawakutakiwa kumtetea JPM kwenye hili suala ni huyu Mwigulu Nchemba!!!

Huyu si mwenyewe ameshawahi kusema mara kadhaa kwamba wakati yupo darasa la nne aliacha shule na kwenda kuchunga ng'ombe!! Hata hivyo, alivyorejea alipewa second chance!!!

Sasa na yeye angenyimwa second chance angekuwa hapo alipo?!

Mwigulu Nchemba huyu hapa:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu.
Popote ulipo Mwigulu... look at yourself! Uliacha shule mara mbili tena bila sababu za msingi lakini bado ulipewa second and third chance!

Leo hii hawa watoto ambao ni victim wa mababa watu wazima unashabikia wasipewe second chance??!!!
 
The Invincible

JF-Expert Member
May 6, 2006
5,982
2,000
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amezionya taasisi zisizo za Serikali zinazohamasisha kudai haki ya mtoto anayepata mimba kurejeshwa shuleni kuacha mara moja na zikiendelea atazifutia usajili.

Mwigulu ameyasema hayo leo, Jumapili wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Parokia ya Kisasa Mjini hapa.

Amesema Serikali haitaomba ushauri wala maoni kwa sababu maelezo yaliyotolewa na Rais, John Magufuli ni maagizo ya Serikali.
Waziri huyo amesema Serikali imetoa haki ya kila mtoto kupata elimu kwa kuifanya kuwa bure kwa hiyo atakayeikosa asitafute kisingizio.

View attachment 530362
"Rais ametoa haki hiyo sasa hivi elimu ni bure, halipi tuition wala nini, atakayeamua kuachana na haki hiyo asitafute kisingizio, asipeleke lawama kwa Serikali, "amesema.

Mwigulu ni kijana asiyejitambua. Asamehewe bure.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom