Mwigulu amuwashia moto Mpina, ni kuhusu kufunga biashara. Adai Mpina anafurahia watu wakiumia

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,822
Akiwa bungeni leo Juni 26, 2023, waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba wakati akihitimisha hoja ya makadirio ya bajeti amemkalia kooni mbunge mwenzeke, Luhaga Mpina kwa madai alikuwa anafungia viwanda alipokuwa waziri huku akifurahia. Mwigulu amesema Mpina alikuwa anafanya sherehe kwa kuchoma nyavu bila kuzidhibiti kuingia.

Mwigulu amesema Rais Samia anawafundisha shughuli za uzalishaji ziheshimiwe na inapotokea matatizo kuwe na utaratibu wa kiungwana wa kurekebisha na kuacha kufunga biashara.

Mwigulu amemwambia Mpina kuwa si ubingwa wala ustaarabu kupinga kila kitu hata ambavyo havistahili kupingwa.

======

Amemshauri Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuwa si ubingwa wala si ustaarabu kupinga kila kitu hata visipopaswa kupingwa, badala yake anaweza kuuliza kwa namna nzuri ili aeleweshwe. Ameyasema haya wakati akirejea hoja ya Mpina iliyokata biashara zifungiwe.

Ametolea mfano alivyokuwa anafunga viwanda, kuchoma nyavu akiwa Waziri kuwa matendo hayo hayakuwa ya kistaarabu. Watu wa Sekta binafsi sio maadui, ni washirika wa maendeleo.

Katika kufungia biashara za watu ni muhumu kuzingatia mitaji yao, uwekezaji na muda wanaotumia kuwekeza na kufanya biashara hizo. Hauwezi kukaa na mtaji wa mtu umeushikilia huku yeye akiumia.


 
Bandari kwanza, tushajua alikuwa wa ovyo inatosha
Bandari ina shida gani kukodisha, wamatumbi mmeshindwa kuendesha bandari yenu basi kaeni kwa kutulia tukodishe tupate hela nyingi ili tuwaletee maendeleo. Cha msingi ikodishwe kwa maslahi ya nchi.
Kama ni amri yangu ningekodisha hadi mwendokasi, reli, airports, atcl, tanesco mpaka ttcl zote ziwe chini ya wageni nyie kazi yenu iwe kula kulala tu.
 
Back
Top Bottom