Mwigulu aishangaa serikali kwa UFISADI na misamaha ya kodi

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
22,378
19,213
Akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara ktk ziara ya kuimarisha chama na kutangaza mafanikio ya serikali ya CCM, Dr Mwigulu Nchemba aliwaeleza wananchi masikitiko yake kuhusu UFISADI unaofanywa na baadhi ya viongozi wanaoiba mabilioni ya fedha za umma; na pia serikali inayowasamehe watu mabilioni ya fedha wakati ikikosa fedha za kuwahudumia wananchi wake.

Huku akishangiliwa sana na umati mkubwa wa wananchi waliohudhuria, Dr Mwigulu alitolea mfano wa mwizi anayeiba bilioni 200, anapelekwa mahakamani ambapo kesi huchukua miaka 10 mpaka hata thamani ya pesa alizoiba inapungua. Alipendekeza ikibainika mtu kaiba afilisiwe mali zake zote na kufungwa jela ili liwe fundisho kwa mafisadi wengine. "Kufanya hivyo kutawafanya watu waogope kuiba fedha za umma", alisema.

Akiongelea misamaha ya kodi, Dr Mwigulu alisema kwamba suala hili huikosesha serikali mapato, ambapo mwaka jana tu serikali imepoteza Tsh 1.8 bilioni.

MAONI YANGU:
Naona sasa Mwigulu ameanza rasmi kufanya kazi ya UKAWA.

Source: Star TV.
 
Huu ni ugonjwa wa akili, naoan damu za watu wasio na hatia zimeanza kumtafuna akili. hii ni mwanzo shughuri yenewe ndiyo kwanza inaanza...damu ya mtu haipiti bure!
 
Huu ndio unaitwa Usanii ambao CCM wameanza kuufanya..Na kwa raia ma bogus kabisa wa Tanzania wataichagua tena CCM...
 
Tekniki hio.. Wewe unawarushia wananchi bomu (wengi wanakufa na kujeruhika sana) , halafu unaenda umejifunga bandeji kwenye ugoko wako ulio ngani ya suti yako..... unawaonesha wanachi bandeji lako ukidai na wewe umejeruhiwa na unakuwa kifua mbele kuwahimiza wananchi mkamsake alierusha hilo bomu ambalo halijulikani liliingilia upande gani.

Unafiki unapopitiliza.. mwishowake huwa sio mzuri sana.
 
Kwani serikali ni nani? Na inaundwa na watu gani au wanaishi sayari nyingine utasikia kinana analia mara nape analia rais nae analia oo mara mwakyembe analia pinda nae yumo embu acheni usanii serikali ni nyie mmeshindwa kazi mrudi kwenu mkalime sio mnakaa kula hela za walalahoi halafu mnatupigia kelele tu hapa na move zenu zisizoisha.
 
Hii habari hata siiamini kabisa! Basi huyu jamaa haki ya nani ni mwehu na hata aliyempa nafasi ya unaibu waziri wa fedha naye ajichunguze. Maneno kama hayo hayawezi kumtoka naibu waziri hata kidogo, serikali ipi anayoilaumu ambayo yeye hayupo ndani yake? Naanza kuamini maneno ya Kakobe kuwa utawala unaoanguka utaparaganyika na kila mtu atasema lake bila hata kufikiri.
CCM hebu ijichunguze na kuona kweli bado iko makini kutawala au ijiweke pembeni ili ijpange upya? Nchi inaangamia kwa kukosa maarifa, na inavyoangamia na wao wanaangamia wakati nchi hii ni ya wote. Kuna sababu gani kuendelea kutawala halafu unakuja kuikabidhi nchi kwa wengine ikiwa hoi bin taaban? Si bora kujiengua mapema ili wenye weledi waiendeleze?
 
kwani kazi ya UKAWA ni kuongelea ufisadi? siyo kupigania katiba mpya tena?
 
hiki ni kituko!ni sawa na mchawi kuwashangaa wachawi wenzake kula nyama ya mtu!!!!!!!!akafie mbele gaidi huyu na unafki wake.

hapa ndipo wapinzani mnachanganyiwa, anapotokea mtu toka nje kuonesha kuwatetea wananchi zaidi ya mnavyowadanganya wananchi.
 
mimi nilimsikia akiongea nilibaki hoi, nikajiuliza kwani mwigulu amejiunga na chama gani cha upinzani? maana huwezi kushangaa madudu ambayo wewe mwenyewe unayasimamia. kilichonishangaza zaidi ni wananchi walivyokua wanashangilia na kumpigia makofi. OMG!!!
 
anajishangaa alivyo mchawi,aache ulaghai! Misamaha hiyo inapopitishwa anasahau kuwa wao magamba huishabikia tena kwa kejeli nyingi! Kweli maccm ni janga la Taifa
 
Back
Top Bottom