Mwigizaji JB apanga kugombea ubunge mwaka 2015...

Mwigizaji JB apanga kugombea ubunge mwaka 2015...

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,458
JB.jpg
Mwigizaji anayependwa sana na mwenye mwili wa kipekee kwenye bongo movies Jacob Steven, ama JB kama anyofahamika kwa wapenzi wake, ameongea na bongomovies.com na kuelezea mpango wake wa kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015.

Katika interview fupi iliyofanyika maeneo ya leaders jijini Dar es salaam leo, JB alisema angependa kuwakilisha wananchi kwani kupitia sanaa ameweza kujifunza matatizo mengi yaliyopo kwenye jamii na anahitaji nafasi ili ayafanyie kazi.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari hii ni kwanini amepata wazo hilo saivi JB alisema kuwa amewahi kushiriki kwenye shughuli nyingi sana za kampeni kama "manager" wa kampeni za wabunge mbalimbali na kupata uzoefu wa siasa na pia karibu wote waliweza kupita kwenye nafasi hizo na sasa anaona ni wakati wake yeye kuwawakilisha wananchi bungeni.

Na alipoulizwa kuhusu suala la chama na sehemu anayopanga kuiwakilisha JB alisema, "kwa sasa siwezi kuweka wazi kuhusu chama na sehemu nayotaka kugombea ubunge, ila wapenzi wangu wakae tayari na wajue mipango yangu kama mwigizaji na mtu anayependa mandeleo kwa jamii"
 
wazo zuri..........ila hata ukiwa mbunge bado ukipata muda hasa baadhi ya rikizo unarudi tena kwenye fani ma funs wako tuendelee kuenjoy.
 
maendeleo kwa jamii yanaletwa na ubunge?....aseme anataka fedha kupitia ubunge. ila bunge litajaa vilaza, si nasikia hata wema anataka ubunge,,,ee mungu tunusuru!
 
Hapa ndio tulipofikia,kila mtu kudhani anaweza kujaribu bahati yake kwnye siasa.Wonders will never end in ths country,Mungu tusaidie.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Aaah!JB sema bwana au unawaogopa wenye nchi watakubandalize!!tuna jua upo CDM labda wakubadili,,ila poa tu tutakuwa na waagizaji bungeni hamna uhalisia ni kuigiza tu na kuimba tu mizik bungeni km jamaa yangu
 
Ila kama yule jamaa wanamuita sugu aliyekusanya wahuni wenzake wakajiita ant virus wakaimba matusi ya aina zote aligombea na akapata ubunge basi kila mtu lazima aone anaweza kuingia mjengoni maana tunaona namna wabunge wanavyokosa adabu kwa kauli chafu ambazo hazina tija katika nyumba iliyobeba uelekeo wa nchi kuwa kama genge la wahuni ptuuu hili nchi joto hasiraa kwa kweli.
 
Hana jipya huyo, aendelee kuchezea nyonyo za vibinti vya bongo movie!
 
Kama kaweza Migulu Michenza na wenda wazimu wake.
Basi kila m2 anaweza.
Hata W.Sepe2 unaweza.
JB NI JEMBE ACHA AJARIBU.
 
Ameshindwa kuleta maendeleo nyumbani kwao (sinza mori) anategemea ng'ombe wa maziwa na bajaj, ataweza kuyaleta hayo maendeleo kwa wanannchi? (hivi alishahama kwao au bado mtoto wa mama)?
 
maendeleo kwa jamii yanaletwa na ubunge?....aseme anataka fedha kupitia ubunge. ila bunge litajaa vilaza, si nasikia hata wema anataka ubunge,,,ee mungu tunusuru!

thanks mkuu. you made my day kwa kusema ukweli. huyo anataka pesa tu hana lolote.
 
Nasubili tu bado wema nae atataka kugombea.

akigombea wema basi na mimi nagombea maana najua wabunge wa wakati huo lazima watakuwa wanapata ofa ya kile kitu kitamu toka kwa bibie wema... naomba sana itokee hata kama ni jimbo la bush kiasi gani nitagombea tu ilimradi nijue yule X wa ile njemba inasema inataka kulewa na yeye anagombea
 
View attachment 90154
Mwigizaji anayependwa sana na mwenye mwili wa kipekee kwenye bongo movies Jacob Steven, ama JB kama anyofahamika kwa wapenzi wake, ameongea na bongomovies.com na kuelezea mpango wake wa kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015.

Katika interview fupi iliyofanyika maeneo ya leaders jijini Dar es salaam leo, JB alisema angependa kuwakilisha wananchi kwani kupitia sanaa ameweza kujifunza matatizo mengi yaliyopo kwenye jamii na anahitaji nafasi ili ayafanyie kazi.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari hii ni kwanini amepata wazo hilo saivi JB alisema kuwa amewahi kushiriki kwenye shughuli nyingi sana za kampeni kama "manager" wa kampeni za wabunge mbalimbali na kupata uzoefu wa siasa na pia karibu wote waliweza kupita kwenye nafasi hizo na sasa anaona ni wakati wake yeye kuwawakilisha wananchi bungeni.

Na alipoulizwa kuhusu suala la chama na sehemu anayopanga kuiwakilisha JB alisema, "kwa sasa siwezi kuweka wazi kuhusu chama na sehemu nayotaka kugombea ubunge, ila wapenzi wangu wakae tayari na wajue mipango yangu kama mwigizaji na mtu anayependa mandeleo kwa jamii"

sasa hivi ubunge umekuwa kama jamvi la wageni au la msibani. kila mtu anautaka. na kila mtu anaufikiria. huu ni uchizi.
 
usiwasikilize hawa mazwazwa, we gombea tu jembe letu!
kwani bungeni nani hajafuata hela? we huoni tunavyokulaga mapilau yao kwenye kampeni?
bunge limejaa maprofesa na ma-dr. kibao, lakini kila siku nchi inakwenda kombo.!
hebu nyie raia wakawaida jitoseni labda twaweza leta angalau chembe ya mabadiliko..
hata wema sepetu poa tu,mbona hao maprofesa na ma-dr. ndo wanaongoza kutuibia hela zetu pale mjengoni, hakuna mchngo wowote wa kimaendeleo significant tunaouona..
acheni unafiki,,
 
Ubunge si kazi! Ukikaa kimya sawa, maadamu ujue tu kuitikia ndiooooooooooooooooooooooooooooooooooo! Unapewa posho yako ya kikao unaondoka. Maana imedhihiri kama huna hoja basi tukana.
 
Amewachoka mademu wa bongo movie na sasa kahamua kwenda kusaka mafuska kule Dodoma? Hapa naanza kumwogopa JB na siangalii tena sinema zake kuanzia leo hii kwani anatangaza rasmi kuwa anahamua kuwa mchawi na fuska. Hakuna mbunge bongo asiye mchawi ama kujihusisha tu na vitendo vya kishirikina. Mhhhh, JB, why hata kama umechoka ku act sinema imba tu bongo fleva, why ubunge....mademu si utawapata tu hapa hapa si mpaka uende Dom babake?
 
Back
Top Bottom