sakapal
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 1,804
- 1,425
Jamani wanajamvi mwenzio akinyolewa nawe tia maji...............
Hapa nilipo nimechanganyikiwa ................laiti ningejua haya yatatokea nisingekubali.........
Haya ni maneno yaliyomtoka mtoto wa dada yangu......., ilikuwa hivi,
''binti huyu wa dada yangu amemaliza form four na baada ya kumaliza form four baba yake alimlipia computer na english course asome. Alikuwa anaenda dara sani kila siku na alikuwa akichelewa kurudi nyumbani kwao kutokana na shida ya usafiri. Kumbe binti alikuwa mida ya lunch anapitia kwa mshefa wake (ambae ni mume wa mtu) na wanaenda hoteli za town na kuvunja amri ya sita kisha jioni anarudi home kimyaa. Jinsi binti alivyo mpole, mkimya, msikivu na mtaratibu hakuna aliyedhani atakuwa anafanya mambo hayo.
Kumbe hoteli walizokuwa wanenda kuvinjari na huyo mume wa mtu kuna rafiki zake na baba wa binti huyo walikuwa wakimuona akijinafasi na huyo mpenziwe. Taarifa zikamfikia baba mtu, nae alikuwa ni yule wa kujisifia mbele za watu kuwa binti yangu anaakili, mtiifu, msikivu ametulia na sifa kibao. Baba yake hakuamini hadi siku walipompa mchongo akashuhudie kwa macho yake. Siku ya tukio kwa kuwabishia rafikize kuwa huyo si bintiye na kama akiwa ni yeye nmfungisha ndoa ya mkeka hivyo alifika na mashehe maana ni muislamu. Basi wakafika hoteli husika na akamuona bintie anatoma ndani ya hoteli na mpenziwe wakiwa wameshikana mikono alipigwa na butwaa na hasira na kusema ngoja ipite nusu saa tukawagongee kwenye chumba chao kama ndo binti yangu kweli basi namfungisha ndoa. Baada ya nusu saa wakagonga mlango wa chumba kweli alikuwa bintiye na huyo mume wa mtu na waliwakuta wanakula raha ndipo wakawaamuru wavae nguo na shehe akawafungisha ndoa palepale.
Hivi ninavoongea binti kafukuzwa kwao na anaishi na huyo mwanaume(kampangia chumba maana nae anafamilia yake), mama mtu amabaye ni dada yangu hajatoka nje kwa kuumwa tangu tukio la bintiye kufungishwa ndoa ya mkeka kwani ndio alikuwa binti yao wa kwanza. Huyu binti alinifata kazini kuniomba nimuombee msamaha kwa wazazi wake arudi na aendelee na maisha kwani bado anataka kuendelea na shule na alikuwa anaongea huku analia na ameahidi kutorudia tena na anajutia makosa aliyofanya.
Mimi najiuliza hivi, ndoa ya mkeka inatambuliwa kiserikali? binti ana miaka 17 sasa nikienda kumuombea kwa wazazi arudi je ndoa itafutika? mke wa huyo mpenz wake hajui ishu. Binti ni wale watoto wanaorudi shule hawafui hawapiki wala hawafuti vumbi, nyumbani mboga nane yaani wafanyakazi kila mahali ili mtoto asome asipoteze muda kwenye shuhuli za nyumbani. Analia kwani pia hiko chumba alichopangiwa hajui kufanya kazi yoyote hata kuosha chombo hajui.
Karibuni kwa mawazo yenu na mchango tafadhali.