Bernard bakari
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 407
- 781
Maisha hayampangii mtu namna ya kujiendesha bali mtu anayapanga maisha yaendeje baada ya kukaa mda mrefu nimegundua nilikuwa mjinga sana nimechelewa mno kwa kutokuweza kuyatawala maisha lakini sasa nimejifunza nahisi sitorudia kosa.
Nilichogundua ili kufanikiwa lazima uwe bahili sana, unatakiwa ujinyime sana, kuheshimu pesa kwa kiwango cha juu, kufanya mambo ya lazima na muhimu kutotumia pesa kufanyia kitu kisicho cha lazima.
Pili ili pesa zikae jaribu kutokutafuta sifa za kijinga kama kufanya kitu kwa kutumia pesa ili uonekane unazo hapo utakuwa umepotea kabisa, ni vyema uonekane huna pesa kumbe unazo utajikuta mambo yako yanaenda vizuri.
Ogopa sana kukopa pesa zisizo na ulazima, pale unapobanwa jaribu kuvumilia changamoto unazokumbanazo
Ili kushinda yote hayo jiwekee malengo katika pesa unazopata kila mwezi au kila siku jipangie kiasi cha kuweka akiba hata kama akiba ndogo we weka na hakikisha kila mwezi unafikisha kiasi ulichojiwekea. Kama mwezi mwingine utapata na matatizo usipofikisha kile kiasi hakikisha unaongeza kiasi kwa miez ijayo ili kufidia kiasi kilichopotea.
Mafanikio yanakuja kwa kuweka akiba na kuheshimu pesa kwa kiwango cha juu, hayo yote yatawezekana ukiwa bahili wa kutupwa.