Mwenyekiti wa UVCCM Kheri James awakabidhi Vijana Jazz Bendi vifaa vya kisasa vya muziki

Sudysoko

JF-Expert Member
Aug 19, 2015
449
180
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komred Kheri James (MCC) amewaongoza viongozi na watendaji wa jumuiya hiyo ktk shughuli ya kukabidhi vifaa vipya navya kisasa kwa bendi yao ya Vijana Jazz ikiwa ni mkakati wa kuifufua na kuijengea uwezo Bendi hiyo.

Akizungumza ktk hafla hiyo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komred Kheri James amesema .

"Tumeamua kuijengea uwezo bendi yetu kwa kuipa vifaa vya kisasa ili kuiongezea ufanisi wakazi,na kuiandaa kimkakati kufanya kazi ya kuibua vipaji vipya, kuelimisha, kuhamasisha shughuli za Maendeleo, kuendeleza utamaduni,kuburudisha,kutangaza mafanikio ya nchi yetu,kueneza sera za chama chetu na kujiendesha kibiashara ili kuimarisha uchumi wa jumuiya"

Aidha amewataka wanamuziki hao kutumia vyombo hivyo katika kuhamasisha Vijana kufanya kazi kwa bidii,kuhamasisha wananchi kuiunga mkono jitihada za serikali, kuhamasisha na kuunga mkono kazi zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi, Kukemea mmomonyoko wa maadili katika jamii zetu na katika kuwatia moyo vijana wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali.

Nao watumishi wa vijana Jazz wameushukuru uongozi wa jumuiya chini ya Komred Kheri James na SG wake Komred Raymond Mangwala kwa kuwapatia vifaa vya kisasa na wameahidi kuvitunza na kuiendesha bendi kwa ufanisi ktk mwelekeo mpya uliopangwa na jumuiya kisiasa na kiuchumi.

Hafla hii imehudhuriwa na wakuu wa Idara za UVCCM taifa, wajumbe wa baraza kuu, viongozi wa CCM wilaya ya Kinondoni,Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam,viongozi wa jumuiya wa wilaya na vijana wa mkoa wa Dar es Salaam.

31a99a55980af5b2c6817b0816490030.jpg

e8d4016b993024a53c4266438de1b96c.jpg

4d8981de25a6d8925dbcb9ca4974656a.jpg
 
Back
Top Bottom