Mwenyekiti wa CHADEMA Usa River auwawa kinyama

Hivi huwa hakuna uwezekano wa kutumia maneno mengine kwenye issue kama hii ambapo mtu ameuwawa kinyama?
Mkuu J. Mushi, mwenye kuleta uhai ni Mungu na ndiye mwenye authority roho iache mwili!. Hata kama mauaji yamepangwa na shetani, shetani hana mamlaka ya uhai wala kifo hivyo bila kujalisha mtu amekufaje hata vitani, hata kwa firing squad hata kwa hukumu ya kifo inabaki Bwana Ameleta, Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe!.
 
Unyonge unamwisho,hatutokubali kuonewa na kuuwawa kama kuku tena,DAWA ni kuandaa mpango kazi kabambe kudhibiti haya matukio.VITA VITA 2.Tukilalamika bila kudhibiti wataendelea kuua na kutisha wapenda mabadiliko.
 
Sidhani kama huu ni mkono wa ccm.labda kuna jingine.anyway ngoja tuone uchunguzi utasrmaje.kuna mengine yanaerza kutokea kwa tukasingiziana kutokana na uhasimu uliopo.lakini kama ni mkono wa magamba hiyo damu haijapotea bure.malipo yake ni ghali sana
 
RIP Mbwambo!Mungu ametoa Mungu ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe!wote waliyofanya huo unyama kwasababu yoyote ile Malipo ni hapa hapa Duniani.

Jamani, imani humfanya tu awe mpuuzi! Sasa hapo Mungu amehusikaje? Tiseme walioua wasamehewe!

Nahisi ata wale vijana waliuliwa kwa style ka hii. Hapa hakuna cha kupozana kuwa Mungu katwaa si kweli. wauaji wapo.
View attachment 52883
 

CCM kama wanataka kuchinjana waseme! Walianza kuua kule Igunga baadae wakawacharaza mapanga wabunge wetu kule Mwanza na leo tena wameua kiongozi wetu! Sierra Leone walianza hivi hivi. Kama wanataka watufikishe huko, sisi tutawafikisha zaidi ya hapo maana umafya kwetu ni zaidi ya siasa. Tunawapa muda waendelee na ujinga wao, siku tukianza kulipiza kisasi nchi haitatawalika.

Una uhakika gani kuwa CCM wamehusika?Acha kukurupuka ndugu!
 
Ni huzuni kubwa sana kwa kitendo hiki cha kinyama. Sipendi kusema watu walipize kwa kitendo hicho kwa sababu najua watu wana hasira. Cha maana sana na cha msingi, watu tuingie katika maombi kwa Mwenyezi Mungu ili hao watu wakamatwe tuweze kujua kwa nini walifanya kitendo hicho na ndipo tutajua adui yetu ni nani. WAna wa Arumeru, kuweni wastaarabu kama mlivyofanya kwenye uchaguzi. Chadema msikubali kulipiza kwa damu kwa kuwa damu itadai damu na anayeuwa kwa upanga adhabu yake aijua Mwenyezi Mungu.

Chadema nawaomba sana tujifanye wajinga wala tusianzishe fujo bali tuwe wanyenyekevu LAKINI werefu. Tuwe wapole kama njiwa lakini werevu kama nyoka. Vijana wa boda boda najua mna hasira mwenzenu ameondolewa kinyama, vumilieni na kuweni na uvumilivu. Simu hiyo itajulikana tu ni ya nani, ilipigwa toka wapi na mwenye simu pia lazima atajulikana. Nasikitika sana kama mtu anaweza kutumi simu kufanya mauaji wakati satellite zipo zinanasa kila kitu.

Mwenyezi Mungu awape ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wanachama wote wa chadema uvumilivu na utulivu mkuu wakati huu wa majonzi.

Wanaomtaka Mwenyekiti wa chama kutoa tamko la kulipiza naomba ushushe jazba kidogo kwani ikiwa ni kulipiza basi tutaingia kwenye machafuko makubwa.

Naomba kuwasilisha

MWana-CDM
 
Binadamu tunafanya mambo yanayogharimu vizazi vyetu. yaani nimeona picha kwenye taarifa ya habari inasikitisha sana.
mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi
 
Duh! It's such a shocking news!imenifanya nikumbuke maneno ya mwanamapinduzi Che Guevara,maneno yake ya mwisho "I know you've come to kill me. Shoot, you are only going to kill a man." These reportedly, were his last words, to Sergeant Jaime Terán..Kamanda Mbwambo,kama wamekuua kwa ajili ya itikadi,jua kua wameua mwili tu,tutayaenzi na kuyakumbuka yale yote uliyokua ukiyaamini,ipo siku damu yako itazaa matunda! R.I.P...salamu za rambirambi kwa familia yake na wanaChadema kwa ujumla, alluta Continua!
 
Poleni sana. Tukio hili inabidi lisiusishwe na siasa. Chamuhimu ni uchunguzi wa kina ufanywe.

R.I.P Mbwambo!
wanao fanya huo uchunguzi si ni magamba hao hao? siku zenu zina hesabika
 
Mkuu J. Mushi, mwenye kuleta uhai ni Mungu na ndiye mwenye authority roho iache mwili!. Hata kama mauaji yamepangwa na shetani, shetani hana mamlaka ya uhai wala kifo hivyo bila kujalisha mtu amekufaje hata vitani, hata kwa firing squad hata kwa hukumu ya kifo inabaki Bwana Ameleta, Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe!.
Asante mkuu Pasco kwa taarifa hii, sikuwa na habari kuwa shetani anauwezo wa kupanga mauaji na Mungu akayatekeleza bila huruma!
 
R.I.P Mbwambo, wanafikiri kwa kuwaua viongozi wa Cdm wenye ushawishi na kukubalika kwa jamii ndio Cdm itashindwa? Hata kama watuchinje sote, Mungu yu upande wetu. M4C FOREVER...
 
this is too much for the party! tafadhali cdm taifa semeni neno maana mkikaa kimya kesho mtachinjwa nyie wenyewe;samaki tumkunje angali mbichi.
 
Hebu tuache jazba...akili yenye hasira kamwe haiko sawa...tusubiri uchunguzi wa mamlaka zinazohusika hili ni jambo zito lisiposimamiwa vyema halitakuwa na mustakabali mzuri kwa taifa letu
 
Back
Top Bottom