Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Tawi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kisutu, limeandika barua ya kutaka maelezo kutoka kwa mwanachama wake, Henry Kilewo, likimtuhumu kwa usaliti, kuhujumu shughuli halali za chama, na kuendesha kampeni za kuwashawishi wanachama kuhama chama chao.
Katika barua hiyo iliyotiwa saini na Katibu wa Tawi hilo, Anaely Sarakikya, tarehe 11 Mei 2025, Kilewo ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa kichama Kinondoni, anatakiwa kujieleza kwa maandishi ndani ya siku 14 juu ya tuhuma zinazomkabili.
Pia, Soma: Patrick Assenga avuliwa Uanachama CHADEMA
Tawi la Kisutu linamlaumu Kilewo kwa kuwa kinara wa "usambazaji wa mabango ya mikutano ya waandishi wa habari inayoratibiwa kwa nia ovu ya kushawishi wanachama na viongozi wa CHADEMA kuhama chama chao."
"Tumeona kupitia vyombo vya habari mbalimbali na mitandao ya kijamii (whatsap group) za chama, wewe pamoja na mwenzako mkitoa lugha chafu na tuhuma dhidi ya chama na viongozi wake wa kitaifa", inaeleza barua hiyo.
Mbali na hilo, Kilewo anadaiwa kuhusika moja kwa moja katika uandishi na usambazaji wa waraka maarufu wa "G55". Waraka huo, kwa mujibu wa tawi hilo, "ulibeba maudhui ya kubeza na kupinga programu za chama ikiwemo ya No Reform, No Election."
Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, matawi ya chama yana mamlaka ya kusimamia na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanachama wanaokiuka maelekezo, sheria, au programu za chama.
Kilewo ametakiwa kuwasilisha utetezi wake kwa maandishi kwa tawi hilo ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya barua, vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.