Mwenyekiti wa CHADEMA Kibaha ajiunga CCM

Mwenyekiti wa CHADEMA Kibaha ajiunga CCM

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
56,901
Reaction score
46,425
Wanabodi.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini, Abdallah Ngajulage ametanganza kukihama chama na kujiunga na CCM.

Ngajulage amejitoa Chadema kwa sababu ya kutawaliwa na ubinafsi na ukabila.

Amechoshwa vitendo vya Chadema nyadhifa kuu za kitaifa kushikwa na watu wale wale kila chaguzi na uchoyo wa maslahi unaowabana viongozi wa chini.

SOURCE: MWANANCHI JANUARI 22, 2013.
 
Mkuu Molemo
Haya habari za mwananchi hizi umezisoma?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA katika halmashauri ya wilaya ya kibaha vijijini, ABDALLAH NGAJULAGE ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM.

Ngajulage alitangaz hatua hiyo juzi katika kijiji cha boko wilaya ya kibaha vijijini.

Alisema sababu zilizomfanya kujitoa chama hicho ni pamoja na kutoridhishwa na uendeshaji wa mambo ndani ya chama hicho na kutawaliwa na ubinafsi,kukandamiza walio chini huku wakubwa wakijinufaisha wenyewe na suala la ukabila.

Pamoja na mwenyekiti huyo, wanachama wengine 32 wamejiunga na CCM wakitokea CHADEMA na CUF.

Mwananchi 22.01.2013
 
T2015CCM Mbona ameenda CCM maana nachojua mimi CCM ni Chama cha Familia za watu Sita au hajasoma majina ya UVCCM na Kamati Kuu..Na katika yote hayo sijasikia jina la Chagulage mimi napafahamu Kibaha sijawahi kumsikia ila sasa hivi nimemsoma hapa JF au Techniques za magamba wanajigawawia kadi alafu wanatangaza kwamba wametokea CHADEMA..Hakuna Jina kama hilo Hapa Kibaha labda kama ni Kibada
 
Last edited by a moderator:
Karudia matapishi yake?kazi kweli kweli...
 
Tunaelekea kwenye uchaguzi jamani sasa ambao wanajiona wanahitaji ulaji wanaanza kuahama mapemaKatika hiki kipindi wengi watahama vyama hasa wanaotaka madaraka ama kipato.
 
Huyu Mwenyekiti alifikiri akiingia CHADEMA atanufaika.Bora ameondoka mapema,kwa kuwa,hafai hata kuitwa baba wa familia,kwa sababu anaonekana yuko kimaslahi zaidi.
 
aliyekua kumbe sio sasa,
Wanakimbia tingatinga lazima liwasafishe mpaka 2015 tutakuwa na makamanda wa kweli..... fukuza wote mapandikizi kajiwai.

V
SENGEREMA.
 
lazima kutenganisha ngano na masuke, asante Mungu kwa kutufunulia maono haya makuu...
 
Mkuu Molemo
Haya habari za mwananchi hizi umezisoma?

Chama
Gongo la mboto DSM

Huyu jamaa muache aende kwani ukombozi sio kazi ya lele mama wengine huwa wanajionyesha upinzani ili wapewe vyeo sasa sijajua huyu jamaa ata pewa cheogani maana huko kumejaa mafisadi wa vyeo.
 
Kwanza huyu masalia amechelewa kuondoka alikuwa hana faida yeyote zaidi ya kumpa Sokwe taarifa za uongo alifikiri Chadema kuna wizi kama kwa magamba alipoona hakuna namna ndio anarudi nyumbani we masalia Chadema hakuna wizi hapa ni ukombozi mpaka kieleweke
 
aliyekua kumbe sio sasa,
Wanakimbia tingatinga lazima liwasafishe mpaka 2015 tutakuwa na makamanda wa kweli..... fukuza wote mapandikizi kajiwai.

V
SENGEREMA.

ameshajiunga ccm ndio maana umeambiwa aliyekuwa, kiswahili kigumu sana ee???
 
Huyu alifukuzwa siku nyingi Chadema kwa utapeli.

mkuu molemo, hivi ingekua balozi wa nyumba kumi wa ccm kajiunga na upinzani hizo sherehe si zingehudhuriwa na kiongozi wa kitaifa?????
 
Kwanza huyu masalia amechelewa kuondoka alikuwa hana faida yeyote zaidi ya kumpa Sokwe taarifa za uongo alifikiri Chadema kuna wizi kama kwa magamba alipoona hakuna namna ndio anarudi nyumbani we masalia Chadema hakuna wizi hapa ni ukombozi mpaka kieleweke

mkuu, watu wanasema balozi wa nyumba kumi wa ccm ni sawa na mwenyekiti wa wilaya au wa mkoa wa upinzani.
 
Back
Top Bottom