Mwenyekiti wa CHADEMA Kibaha ajiunga CCM

Mwenyekiti wa CHADEMA Kibaha ajiunga CCM

Karuka mkojo akanyage nnya...Akirudi tena CHADEMA hamna kumpokea msaliti hyo..na tukishinda Wasaliti na mafisadi wote wanyongwe mnazi mmoja..SWINE
 
Huyu mzee alikuwa m/kiti mtaa kupitia ccm na aliondoka na kuhamia cdm mei 2012, na baadhi viongozi wa cdm wilaya wakamkaimisha uwenyekiti jimbo k/vijijini, kila siku akiingia ofisini anasaini kitabu cha wageni, alihama cdm julai na sio juzi kama wasemavyo
 
Ayaaaaaa ! kadandia boti inayozama. maskini wee, hakuna haja ya kupiga mbizi kwenda kumuokoa. Wacha samaki nao wapate mlo wenye virutubisho. Kama akifanikiwa kujiokoa na kurudi nchi kavu arudi na majibu ya maswali yafuatayo:
1. Ni akina nani waliotuibia mabilion ya shilling na kuyaficha uswis?
2. Ni akina nani waliotuibia mabilion kupitia meremeta, kagoda, epa na richmond?
3. kama utapata majibu (ukiweza kuibuka) tutajie majina yao. kama utashindwa endelea kubaki ccm!
 
Wacheni ekwende zake kwenye magamba yake akapokeee rushwa zake na kuuza pembe za ndovu wetu kwenye nchi yetu pasi na akili zetu kufikiri urithi wetu na wa watoto wetu.
 
Huyu jamaa muache aende kwani ukombozi sio kazi ya lele mama wengine huwa wanajionyesha upinzani ili wapewe vyeo sasa sijajua huyu jamaa ata pewa cheogani maana huko kumejaa mafisadi wa vyeo.

Kama hoja ya cheo si tayari alishakuwa nacho?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Wanabodi;
Magamba yameanza kuweweseka na kuchanganyikiwa
Chadema haina Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini, kama CCM ilivyoigizwa kichakani na Abdallah Ngajulage, Chadema ina Uongozi wa Wilaya ya Kibaha na Uongozi wa Majimbo ya Kibaha Mjini na Kibaha Vijijini. Kama kweli Ngajulage angekuwa kiongozi wa ngazi ya Wilaya au Jimbo angejieleza kwa kuzingatia muundo wa Chama. Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kibaha ni Ndg Bumija Moses Senkondo, Mwenyekiti wa Jimbo la Kibaha Mjini na Ndg Ally Mohamedi Gandi na Mwenyekiti wa Jimbo la Kibaha Vijijini na Ndg Fatuma Halfan. Ukweli kuhusu Mzee Abdallah Ngajulage ni kuwa mwanzoni mwa mwezi mei 2012 Chadema kilifanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mpiji na kuvuna Wanachama 56 wote wakitokea CCM, miongoni mwa Wanachama hao ni Abdallah Ngajulage ambaye alikuwa ni mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Mpiji kwa tiketi ya CCM na baada ya kujinga na Chadema aliteuliwa kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Tawi la Chadema katika Kijiji cha Mpiji. Baada ya mwezi mmoja tu tokea awe Mwanachama wa Chadema alianza sarakasi za kigamba na ilipofikia tarehe 28/07/2012 alivuliwa rasmi uanachama wa Chadema. mwisho nawapa pole sana Magamba kwa kuingizwa kichakani na Mwenzao. mwenye hoja au maswali tunakaribisha na atapata majibu sahihi.
"HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE"

Asante sana Bumija kwa kuwaelewesha watu wasiojua CDM iko vipi Kibaha, kazi iliyombele yako hivi sasa ni kushughulikia yale mabaki ya vijana yaliyokuwa yanatumika na mchange hapo Kibaha, naamini vijana wenyewe unawajua fika sasa kusanya ushahidi na ukikamilisha kawamwage mto Ruvu, KWANINI WAO TU HUONEKANIKA WAKIWA WAMEJIFICHA NA WATU WA TISS???
 
Wanabodi.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini, Abdallah Ngajulage ametanganza kukihama chama na kujiunga na CCM.

Ngajulage amejitoa Chadema kwa sababu ya kutawaliwa na ubinafsi na ukabila.

Amechoshwa vitendo vya Chadema nyadhifa kuu za kitaifa kushikwa na watu wale wale kila chaguzi na uchoyo wa maslahi unaowabana viongozi wa chini.

SOURCE: MWANANCHI JANUARI 22, 2013.

Mkuu Ritz.
Baada ya kusikia ufafanuzi wa John Heche EATV unasemaje kuhusu hii habari yako?!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Safi sana kamanda BUMIJA MOSSES kwa ufafanuzi wa hoja kwa umakini sana.

Siku hizi ukiwa upinzani na ukitaka upokelewe kwa nderemo na vifijo ndani ya ccm we jipachike cheo chote tu cha uongozi uone utakavyofanyiwa sherehe ya mapokezi!

Chama cha ccm kimekuwa desperate kiasi kikubwa sana na nguvu ya Chadema kiasi kwamba wamesahau kwamba wanadaiwa na wananchi utekelezaji wa ahadi zake na kujikita katika kufanya propaganda dhidi ya Chadema!
 
Last edited by a moderator:
Wanafiki watatoka wote, watatuachia CHADEMA yetu.
 
Back
Top Bottom