Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu turudishie CCM kwenye misingi yake

Wewe ni aina ya CCM wenye akili
CCM ya Napd na Kinana ilikuwa insjibu hoja kwa hoja, CCM hii ya Shaka na mwenzie nani sijui hata nina lake wanategemea virungu vya polisi viwanyamzishe wapinzani!
Hili tutapambana nalo hadi CCM yenyewe irudi kwenye siasa zake
 
Ni lini CCM hakutuhumiwa kuiba kura? Tangia 95 kuna tuhuhuma za kuiba kura, tangia miaka hiyo wasiojulikana walikuwepo walikanda Dr. Ulimboka na wakamfyeka Daudi Mwangosi..!!

Utofauti wa CCM ya Kikwete ilikuwa dhaifu sana afadhari CCM ya Magu ilikuwa na uhakika labda kutokana na mtu aliyepo juu pale..!! Binafsi naanza kupiga kura mwaka 2015 sikupigia Magufuli kwasababu naipenda CCM ila nilikuwa na imaninae yeye kama yeye kwamba ni mtu kazi ila sijawah kumiliki kadi ya CCM mpaka leo.
Kutumia dola kubaki madarakani sio uimara wa chama
 
Siasa mchezo mchafu sana...

Inawezekana kabisa hili vuguvugu nyuma yake yuko mama, amewafinyia jicho waendelee tu.
 
Leo CCM inalaumiwa eti inaua watu, yaani mambo ya wasiojulikana. Hii haijawahi kuwa msingi wa CCM

CCM inaonekana inaogopa wapinzani, suala la kununua wapinzani. Hatuna CCM ya namna hii kwenye misingi yake

CCM inatajwa kila pahala eti inaibaga kura, uchaguzi uliopita Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu. CCM kama hii haipo Tanzania kwenye misingi ya CCM

CCM inahimiza wapinzani wafanye siasa za kisayansi na za kistaarabu, ni mara ngapi sisi CCM tumekosa ustaarabu na sayansi ya siasa, hadi tunatia kinyaa?

Yaani inakuwa mtu anayetangaza amani huku kaweka panga mfuko wa nyuma.

Waliopo ndani ya CCM hawawezi kukosoa wala kusema vibaya chama kwa kuhofia vyeo vyao. Sisi tusio na hio hofu acha tuseme. Kuanzia sasa na kuendelea na sisi CCM huru / CCM msingi tutaendeleza vuguvugu hili la kuidai CCM msingi inayoishi kwenye misingi ya 'CCM'. Tutatumia kila aina ya mitandao kuidai hii CCM.

Hatutaki CCM ionekane kama kimbilio la uteuzi, kimbilio la kuganga njaa. Wanaopigania chama usiku na mchana wanaachwa solemba na vyeo kupewa wahamiaji. Hapana. This is no more!

Ki ukweli CCM ya nyakati hizi ni CCM nyingine sio ile yenyewe hasa ya 'Jembe na Nyundo'. Hii si CCM ya kufanya mapinduzi. Vilio vya ajira kila kona ya nchi, CCM ipo kimya haina mipango inayoeleweka.

CCM ni chama cha Mapinduzi. Ni chama cha kufanya mapinduzi at any time katika kujenga nchi. Hata kabla ya vuguvugu la Katiba CCM tulipaswa kuleta katiba mpya maana CCM inaona mbali miaka 100 zaidi kuliko wapinzani. CCM sio ya kutumia nguvu bali sayansi ya siasa.

CCM ina rangi ya kijani, alama ya Jembe na Nyundo kuashiria amani, furaha, upendo, uchapakazi kwa kila mtu.

Mwenyekiti wetu, Mh. Samia tunaomba CCM yetu asili tuwakabili wapinzani squarely hoja kwa hoja.

Hatuhitaji tena msaada wa mamlaka za ki dola bali tunahitaji mamlaka ya ki chama tucheze ngoma za kisiasa na hawa jamaa zetu wa upinzani.

UVCCM kujitokeza na kusema Katiba Mpya sio muhimu nako ni kukosa kuelewa siasa za nyakati.

Wakati, wapinzani wakiendesha vuguvugu la katiba Mpya na sisi CCM msingi / CCM huru / CCM damu tunataka kuanzisha vuguvugu la kudai CCM msingi, maana CCM hii sio ile ya akina Nyerere, sio ile ya akina Kawawa, hii ni 'pure CCM JAZA TUMBO'. Hatuitaki hii CCM inayoogopa kula sahani moja na wapinzani kwenye majukwaa ya kisiasa! CCM inayosemwa ni wepesi kama pamba bila msaada wa ki polisi. Tunaanza harakati za kuitafuta CCM yetu. Tutafanikiwa tu.

Hatutaki CCM yenye kuonekana CCM haramu. Tutaipigania CCM asili na kuhama hatuhami.

CCM ndio iliyoruhusu siasa za upinzani iweje sasa tuonekane tunawaogopa?.

#VuguvuguCCMmsingi
#VuguvuguCCMmsingi
#VuguvuguCCMmsingi
#VuguvuguCCMmsingi
Leo ndiyo nimemsoma Mwana CCM ambaye anajua kwa nini TANU ilidai uhuru ili kujitawala.
Pia nimeona kuwa kuna mtu anaweza kusema ukweli daima.
Ila tu niwahakikishie wana CCM kuwa kama Viongozi wa dini zote hapa nchini ambao Mwenyezi Mungu huwa Anajibu maombi yao wakaomba Mwalimu Nyerere akafufuka akaelezwa madudu ya CCM ya sasa hata akasikia kuna mpinzani alipigwa risasi tu acha kuuawa, Nyerere ama hangekubali kuishi Tanzania au angeanza upya kupigania Uhuru! Nadhani wengi mnaelewa ninachosema na mimi sina Chama hapa nilipo ingawa nilikuwa Umoja wa Vijana wa TANu wakati tunagombea Uhuru. Huu ni wakati wa kujisahihisha tusingoje Mwenyezi Mungu aingilie kati. Na Viongozi wa dini waache unafiki na kuganga njaa. Wapiganie ukweli.
 
Leo ndiyo nimemsoma Mwana CCM ambaye anajua kwa nini TANU ilidai uhuru ili kujitawala.
Pia nimeona kuwa kuna mtu anaweza kusema ukweli daima.
Ila tu niwahakikishie wana CCM kuwa kama Viongozi wa dini zote hapa nchini ambao Mwenyezi Mungu huwa Anajibu maombi yao wakaomba Mwalimu Nyerere akafufuka akaelezwa madudu ya CCM ya sasa hata akasikia kuna mpinzani alipigwa risasi tu acha kuuawa, Nyerere ama hangekubali kuishi Tanzania au angeanza upya kupigania Uhuru! Nadhani wengi mnaelewa ninachosema na mimi sina Chama hapa nilipo ingawa nilikuwa Umoja wa Vijana wa TANu wakati tunagombea Uhuru. Huu ni wakati wa kujisahihisha tusingoje Mwenyezi Mungu aingilie kati. Na Viongozi wa dini waache unafiki na kuganga njaa. Wapiganie ukweli.
Acha tu inauma sana. CCM ilipaswa kuwa baba la Vyama vya siasa barani Afrika, lkn kwa sasa sivyo
 
Back
Top Bottom