mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,150
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amesema ana siri kubwa ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia Chadema na kupewa nafasi ya kugombea urais akiwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Aliwataka wananchi kumpuuza mgombea huyo wa Ukawa na badala yake wananchi waelekeze nguvu zao kumchagua mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli huku akisisitiza kuwa ni muda wa Kanda ya Ziwa kumtoa rais.
Matata
Aliyewahi kuwa Meya wa Jiji la Mwanza kupitia Chadema, Henry Matata naye ametoboa siri baada ya kudai alijiunga na chama hicho akiwa pandikizi kutoka CCM na kwamba alichokipata kinatosha.
"Mimi nilikuwa pandikizi wa CCM ndani ya Chadema, baada ya kuona Mbowe natekeleza Ilani ya CCM katika kipindi changu cha Uongozi wakanifukuza," alidai Matata.
Aliongeza kuwa akiwa Chadema amekaa humo na kujua matatizo na siri zote za chama hicho pamoja na matatizo yote ya Mbowe.
Hata hivyo, aliwataka wanachama wa CCM Wilaya ya Geita ambao bado wamegawanyika kutokana na makovu ya uchaguzi wa kura za maoni kuvunja makambi ili kujihakikishia ushindi katika jimbo hilo la Geita.
Source: Jambo leo
NB. Nilikuwa nalinganisha tu maneno ya Nape leo kumtuhumu Lowasa kutumia udini, je hapo kwenye bold mwenyeketi wa ccm hajatumia ukanda kumnadi mgombea wake? je hili ni sawa kwa Nape lakini la Lowasa ndio kosa? Nasema hvi kwa sababu simjamsikia kiongozi yeyyote wa ccm akimkemea msukuma. je magufuli achaguliwe kwa sababu anatoka kanda ya ziwa?