Mwenyekiti wa CCM ajiunga Chadema

Mwenyekiti wa CCM ajiunga Chadema

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
2,274
Reaction score
303
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), katika kata ya Kukirango wilayani Butiama mkoani Mara, Lucas Magweiga (43), amejiengua kwenye chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kufuatia hatua hiyo, Magwaiga aliamua kumnadi mgombea wa CHADEMA Issa Ihunyo Khazi kwa madai kuwa amechoshwa na vitendo vya ufisadi vilivyofanywa na mgombea wa kiti hicho kupitia CCM Fidelis Kisuka tangu awe diwani wa kata hiyo miaka 16 iliyopita.


Akiwa amevalia mavazi ya CCM kwenye mikutano ya CHADEMA jana, iliyofanyika katika vijiji tofauti vya Kamugegi na Kyawazaru, Magwaiga ambaye alijivua cheo cha uenyekiti na uanachama wa kawaida, alisema CCM imepoteza dira na mwalekeo kwa kumteua tena Kisuka kuwania nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka minne kutokana na fedha zake.


"Huyu mtu hakubaliki hata kidogo, lakini amepitishwa kutokana na fedha zake, CCM imepoteza mwelekeo…siwezi kuendelea kubaki kwenye chama hiki hata kwa dawa," alisema Magwaiga.


Sababu kubwa ya kumpigia debe mgombea wa CHADEMA inatokana na kutambua uwezo wake na umakini na kuwa mwenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo katika kata hiyo.


Akihutubia mamia ya wananchi wa vijiji hivyo, mwenyekiti huyo maarufu kwa jina la ‘Kichomi' aliwaomba wana CCM waungane na kumchagua mgombea wa CHADEMA kwa ajili ya kupata ukombozi mpya.


"Mimi siogopi kuulizwa wala kunyang'anywa kadi ya CCM, lakini ukweli utabaki pale pale kuwa chama hiki kimepoteza mwelekeo… ukweli unabaki pale pale kuwa CHADEMA imeleta mgombea makini ambaye ni chaguo la wana Kukirango," alisema Khazi.


Pamoja na Kisuka kuwa diwani kwa kipindi chote na kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kipindi cha miaka 10, wananchi wake wameendelea kuwa maskini wa kutupwa kutokana na kutafuta fedha nyingi za miradi mbalimbali kutoka kwa wafadhili.

Chanzo: Tanzania Daima
 
Safi sana,

Moto wa nyika unazidi kushika kasi. Kuna jamaa kanambia kuwa huko Mwanza hali ya CCM ni mbaya sana. Kwamba kwa ufupi CCM ilishakufa siku nyingi.

Watu wote wenye mapenzi na nchi hii waanze maandalizi ya kulinda kura zetu zisifanyiwe michezo ya Kivuitu!
 
source?

Najua mnajua na msiojua mjue, na wengi watazidi kujua na hata CCM WANAJUA Kuwa CHADEMA IKO JUU. Habari ndio hiyo.
 
Kazi bado, hapo october 31 ndo finali, and the mission will be complete. Kazeni buti twende jamani, tunataka na mikoa mingine waache kuogopa hawajachelewa wanaccm jiengueni haraka ili tupate ushindi wa kishindo mwaka huu.
 
kiwa amevalia mavazi ya CCM kwenye mikutano ya CHADEMA jana, iliyofanyika katika vijiji tofauti vya Kamugegi na Kyawazaru, Magwaiga ambaye alijivua cheo cha uenyekiti na uanachama wa kawaida, alisema CCM imepoteza dira na mwalekeo kwa kumteua tena Kisuka kuwania nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka minne kutokana na fedha zake.

"Huyu mtu hakubaliki hata kidogo, lakini amepitishwa kutokana na fedha zake, CCM imepoteza mwelekeo…siwezi kuendelea kubaki kwenye chama hiki hata kwa dawa," alisema Magwaiga.

Ndege njema huonekana tangu asubuhi.
 
Safi sana,ufisadi unatakiwa upingwe kwa vitendo!hii ni hatua nzuri sana!
 
another political prostitution... angekua chadema kaham ungesikia maneno... njaa inatuua
 
Source please and if possible picha!!! Maana hizo ndo zitakazo wafedhehesha wa kina MS hapa!! Duh!
 
Mwenyekiti wa kata? Ndio nini. Humu kuna wendawazimu nini" msitupotezee muda
 
Kwanza ni shangwe kubwa mwenye dhambi mmoja anapotubu.
Pili ni ujasiri mkubwa mtu kuihama CCM inayofuatilia maisha ya watu kila siku na kuhakikisha kuwa wanahujumu shughuli zao za kila siku pale wanapoonekana kukikataa chama hicho au hata kukipinga tu.

Karibu kamanda katika mchakato.
 
kuvua kidagaaa imekua sewe kuna wagombea ubunge chadema wamekimbia

japo mliwaita malaya. wamehongwa na mengine

huyu na yy mnajuaje kama si njaa au chuki zake binafsi?
 
Tangu kampeni zianze... i could conclude that transfer window net effect CCM ina positive.
 
kuvua kidagaaa imekua sewe kuna wagombea ubunge chadema wamekimbia

japo mliwaita malaya. wamehongwa na mengine

huyu na yy mnajuaje kama si njaa au chuki zake binafsi?

Mkuu mbona waongea sauti kama ya Malecela?
 
Tangu kampeni zianze... i could conclude that transfer window net effect CCM ina positive.
hao mnaoendelea kumdanganya zuzu wenu kwa kumpa kadi za wanachama feki wa upinzani waliohamia CCM
 
kwanza ni shangwe kubwa mwenye dhambi mmoja anapotubu.
Pili ni ujasiri mkubwa mtu kuihama ccm inayofuatilia maisha ya watu kila siku na kuhakikisha kuwa wanahujumu shughuli zao za kila siku pale wanapoonekana kukikataa chama hicho au hata kukipinga tu.

Karibu kamanda katika mchakato.

hakika nin shangwe kubwa mwenye dhambi mmoja akitubu.
 
Huyu sio kuwa kahama kutokana na njaa, ni kuwa amechoshwa na CCM.
 
Kwanza ni shangwe kubwa mwenye dhambi mmoja anapotubu.
Pili ni ujasiri mkubwa mtu kuihama CCM inayofuatilia maisha ya watu kila siku na kuhakikisha kuwa wanahujumu shughuli zao za kila siku pale wanapoonekana kukikataa chama hicho au hata kukipinga tu.

Karibu kamanda katika mchakato.

Afanyiwe ukombozi.
 
Back
Top Bottom