TANZIA Mwenyekiti wa BAWACHA wilaya ya Siha afariki dunia

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Mwenyekiti wa Baraza la wanawake wa Chadema (Bawacha) Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Elizabeth Mollel amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Ocean Road, iliyopo Jijini Dar es salaam.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Siha, Imma Saro amesema kiongozi huyo amefariki alasiri Aprili 18, 2025 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Ocean Road.

"Kwa masikitiko makubwa, natangaza kifo cha Mwenyekiti wa Bawacha Wilaya ya Siha, Elizabeth Mollel, kilichotokea Aprili 18, 2025 saa 9 alasiri katika Hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu," amesema mwenyekiti huyo.

Amesema kifo chake ni pigo kwa chama hicho kwa kuwa alikuwa ni kiongozi mchapakazi, mpambanaji na aliyekuwa akijituma katika kazi.

"Kifo cha Elizabeth ni pigo kwa chama, tumepoteza mpambanaji. Nilifahamu Elizabeth Mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu akiwa anajitolea katika chama, amelea wengi amefanya makubwa ndani ya chama na alikuwa ni kiongozi asiyechoka kukipenda chama," amesema Sarro.

Aidha amasema chama hicho, kitatoa taarifa zaidi baadaye kuhusu maziko ya kiongozi huyo.
1745068608027.png

Chanzo Mwananchi
 
Mwenyekiti wa Baraza la wanawake wa Chadema (Bawacha) Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Elizabeth Mollel amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Ocean Road, iliyopo Jijini Dar es salaam.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Siha, Imma Saro amesema kiongozi huyo amefariki alasiri Aprili 18, 2025 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Ocean Road.

"Kwa masikitiko makubwa, natangaza kifo cha Mwenyekiti wa Bawacha Wilaya ya Siha, Elizabeth Mollel, kilichotokea Aprili 18, 2025 saa 9 alasiri katika Hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu," amesema mwenyekiti huyo.

Amesema kifo chake ni pigo kwa chama hicho kwa kuwa alikuwa ni kiongozi mchapakazi, mpambanaji na aliyekuwa akijituma katika kazi.

"Kifo cha Elizabeth ni pigo kwa chama, tumepoteza mpambanaji. Nilifahamu Elizabeth Mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu akiwa anajitolea katika chama, amelea wengi amefanya makubwa ndani ya chama na alikuwa ni kiongozi asiyechoka kukipenda chama," amesema Sarro.

Aidha amasema chama hicho, kitatoa taarifa zaidi baadaye kuhusu maziko ya kiongozi huyo.View attachment 3309488

Chanzo Mwananchi
Apumzike kwa amani.
 
Pole sana wanafamilia, ndugu, jamaa, marafiki na wapenda haki wote.

Mungu wetu wa huruma, tunakuomba umjalie pumziko jema marehemu Elizabeth, maana Kristo Bwana alikufa msalabani kwaajili ya ukombozi wa wote wenye kulitii jina lake, na akawakomboa kwa damu ya thamani kuu.
 
Back
Top Bottom