Mwenyekiti UWT: CCM majungu yatatumaliza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti UWT: CCM majungu yatatumaliza

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kaa la Moto, Oct 5, 2010.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mwenyekiti UWT: CCM majungu yatatumaliza
  Monday, 04 October 2010 18:45

  Mwandishi Wetu, Bukoba

  MWENYEKITI wa Umoja wa wananwake (UWT) Bukoba Mjini , Mulungi Kichwabuta,jana aliibuka mjini hapa na kuwataka wanaCCM kupigania ushindi wa chama chao badala ya kuanzisha majungu katika kipindi hiki cha Kampeni.

  Mulungi alisema hayo kufuatia taarifa iliyotolewa kwenye kikao cha Mama Salma Kikwete na Katibu wa CCM kwamba mwenyekiti huyo anashiriki kuivuruga CCM.

  Akizungumza jana mjini hapa Mulungi alisema kuwa wakati wanachama na viongozi wa chama hicho wakipambana kuhakikisha ushindi unapatikana katika chama chao kuna baadhi ya watu wameanza kuchafuana hali inayoweza kuwapatia mwanya wapinzani.

  “Ni kweli wametoa shutuma kuhusu mimi kwamba nampigia kampeni Mstahiki Meya, lakini ninachoamini ni kwamba wakati huu ni kuhakikisha ushindi wa mbunge, diwani na rais, mambo ya umeya ni baada ya ushindi” alisema.

  Mulungi alisema kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakichanganya wapigakura kwa kuanza mikakati ya umeya wakati bado hawajapata hata udiwani kitu ambacho kinaweza kutoa mwanya kwa wapinzani.

  “Nadhani Mzee Ruhangisa ni mgombea wa CCM katika kata ya Kitendagulo, hivyo nguvu za kumtetea apate ushindi ni wajibu wetu sote baada ya uchaguzi wakipatikana madiwani watawajibika kuchagua meya”.

  Naye muasisi wa CCM, na mkazi wa Kitendagulu, Mzee Kassim Kalwandira alisema jana kuwa amepata taarifa za mvutano uliotokea katika kikao hicho cha CCM , mbele ya mke wa rais mama Salma Kikwete, lakini alisikitika kwa kuwa Mzee Ruhangisa hayupo nchini kufafanua.

  “Nimeyasikia hayo na hayajaanza leo, lakini kikubwa ni kujua kuwa kuna watu walianza zamani kutaka Ruhangisa asirejee katika udiwani, lakini walishindwa kwa kuwa wananchi bado wanampenda na kumkubali” alisema Mzee Kalwandira ambaye alikuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Bukoba.

  Alisema kuna baadhi ya watu ambao bado wana vidonda vya kura za maoni ambao walikuwa wanatarajia kuwaangusha baadhi ya wagombea, lakini waliposhindwa wamekuwa wakihaha kutafuta jinsi ya kuharibu.

  “Kuna maneno kuwa watu walikuwa wamechangiwa pesa na wafanyabiashara na wanasiasa ili kuwaangusha watu kama Ruhangisa, lakini wanashindwa kwa kuwa watu wana imani nao”
   
 2. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Mkuu kwenye Red vipi hapo unamili chombo cha habari nini! au wewe mwandishi wa habari
   
 3. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Huo ndio ujira wa kubinafsisha urais, UWT, JWTZ, Chama kuwa ni vya kifamilia!!!
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hii ni direct quote toka gazeti la majira mkuu. Mimi sikai Bukoba na wala sijawahi kuwa mwandishi wa habari.:A S wink:
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mwaka huu watatoana macho. Salma Kikwete anachezea pesa yetu tu bure hakuna atakaloweza kufanya maana wanacheka na kusema mambo yamekwisha lakini pembeni tunajua nani w kutopigiwa kura.
  Kigumu chama
   
 6. p

  pierre JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtaji wetu ni kura zetu.Usimpigie kura fisadi hata kama umechukua Mkwanja.Kuna watu wanapita nyumba kwa nyumba wakiwa na daftari na sh.5000 - 10,000 wanakupa wanaomba waorodheshe namba ya kadi ya kupigia kura.Hii ni usanii,kwani kwenye kupiga kura ukishapiga kura hakuna mtu anayehakiki kuona kweli jina aliloandika kura imekwenda kwa mhusika .Wadau naomba muwaelimishe wananchi kuhusu hilo,maana maeneo ya Jangwani hili limetokea,ilibidi nimwelimishe yule dada.Sasa hapa ni Dar mambo ndio hivi,tuelimishe wasio na uelewa wa kura.
   
Loading...