ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,592
BARUA MAALUM KWA WANACC NA MMU WOTE
S.L.P. 2014
LADIES ONLY
JF CC NA MMU
MODERATOR
S.L.P 000
JAMII FORUM
YAH: MWENYEKITI MPYA WA CC 2014 NA VIONGOZI WENZAKE
Rejea kichwa cha habari hapo juu chasema;
Kwa muendelezo wa mwongozo wa KATIBA ya CC hapa jamvini. CC imeona ilete uchaguzi mpya wa kumchagua mwenyekiti mpya wa CC kwa mwaka 2014 kwani mwenyekiti aliyekuwepo muda wake wa uongozi umekwisha na hata hivyo katika uongozi wake hakukuwa maendeleo yoyote kwani alisababisha watu wapigwe BAN, wakosane, na mambo ya hapa na pale ilimradi matatizo hapa jamvini ndipo uongozi ukaamua ulete mapinduzi mapya ya kumchagua mwingine kushika nafasi hiyo ambaye ataleta mwamko hapa jamvini.
Hivyo basi jopo zima la CC lilikaa na kupendekeza majina ya wafuatao ambao watakuwa viongozi hapa jamvini kwa mwaka 2014 - 2017 nao ni:-
1 Lady doctor ni MWENYEKITI
2. Mamndenyi ni MWENYEKITI MSAIDIZI
3. ladyfurahia ni KATIBU
4. Passion Lady ni KATIBU MSAIDIZI
5. amu ni MTUNZA HAZINA
6. charminglady ni MTUNZA HAZINA MSAIDIZI
Hao ndio viongozi wa sasa na hatutapenda mtu akate rufaa yoyote mjengoni wala kuharibu uongozi huo kwani hatua kali za kinidhamuna kisheria zitachukuliwa. Ni vyema wanajf wote mkawapa support ya kuwa pamoja nao na kuwasaidia pindi wawaombapo msaada wa hali na mali ili kuimarisha mjengo wetu.
Tunawatakia kila la kheri katika uongozi wao
Kwa pamoja tunajenga mjengo wetu
Wasalaamu;
Ladyf
Last edited by a moderator: