Mwenyekiti halali wa CUF ashiriki usafi

Mwenyekiti halali wa CUF ashiriki usafi

fa67b7ee6a7a8818358ea90f1af9d9c0.jpg
fb5a0ee9784a5f4d0b3d293904e32680.jpg
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya The Civic United Front, mhe. Julius Mtatiro yuko nchini Afrika ya Kusini kwa safari ya kikazi ya siku 5 akikiwakilisha chama.

Mhe. Mtatiro amealikwa na taasisi za kidemokrasia za FPD na ADI za Kusini mwa Afrika na ataviwakilisha vyama vya upinzani vilivyoko Afrika ya Mashariki na ukanda wa SADC.

Katika Mkutano huo mhe. Mtatiro amepewa fursa ya kuwasilisha mada juu uzoefu wa changamoto zinazovikumba vyama vya Upinzani Afrika Mashariki. Mada hiyo itawakilishwa mbele ya viongozi mashuhuri wa vyama vya upinzani walioko Kusini mwa Afrika wakiwemo viongozi wakuu wa DA ya Afrika ya Kusini, MDC ya Zimbabwe n.k.

Mhe. Mtatiro pia amepata mwaliko maalum wa Mazungumzo ya faragha na kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Afrika ya Kusini (DA), mhe. Mmusi Maimane, ambapo watazungumzia juu ya uimarishaji wa uhusiano wa kidugu uliopo kati ya DA na CUF ikiwa ni pamoja na kupanga Programu za kujengeana uwezo kati ya vyama hivi viwili.

Pamoja na mambo mengine mhe. Mtatiro pia atakutana na wakuu wa taasisi za FPD na ADI kwa ajili ya mazungumzo maalum ya uimarishaji na ukuzaji wa mahusiano ya kimataifa kati ya CUF na taasisi za Kidemokrasia za Kusini mwa Afrika.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano na Umma,

The Civic United Front (CUF)
29 Oktoba 2016.

Link. https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/1140585/
Mwenyekiti wa CUF Mtatiro safarini kikazi, Afrika ya Kusini
 
Kweli siasa mwanaharamu, hao wanaomlinda nakumbamwaka jana walimtwanga virungu pande za Mbagala halafu leo wanampetipeti. What a shame..!!??
 
Mbona simuoni Msajili akimsaidia Bwana yule usafi
 
huu mgogoro una takribani mwezi sasa lkn ukimya wa kambi ya akina maalim unanifanya nifikirie kwamba hata wao wanakubaliana kwamba prof ndo mwenyekiti halali.
 
Kashasahau kile kipigo alichopewa na polisi?? Hao hao wanaomlinda baada kukubali kumtumikia mukulu……
 
Uzuri wa Prof Hana Papara. Akina Seif wamejipelek a kwny Corner wenyewe kwa kukimbilia Mahakamni. Hukumu ikitoka sijui ndio watarudi kwny Meza ya Mazungumzo?
 
Huyu muigizaj mzur kama muigzaj machachar wa vichekesho ana macho flan hv ya bei kal
 
Mtatiro amepewa mwaliko wa vyama vya siasa, yuko SA ni mtoa mada

"Nashiriki mkutano maalum unaoangazia Changamoto za Vyama visivyo madarakani. Nitawasilisha MADA mbele ya wakuu wengine wa vyama akiwemo #Mmusi_Maimane, kiongozi wa DA ya Afrika Kusini, Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani nchini Zimbabwe, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani nchini Zambia, Lesotho n.k. Kutoka Afrika Mashariki, ni CUF pekee ndiyo imepata heshima ya kuwakilisha. Mkutano huu umeandaliwa na FPD na ADI (Mashirika yanayosimamia Demokrasia, Kusini mwa Afrika). Mada ntakayoiwasilisha ntaifasiri baadaye na kuwawekea mtandaoni. Wikendi njema.

Julius Mtatiro,
Johannesburg."
CHADEMA haikualikwa?
 
Piga kazi lipumba
Waonyeshe kuwa Akili ndogo haiwezi ongoza Akili kubwa
 
Back
Top Bottom