Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Arusha, Nanyaro anasakwa na polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Arusha, Nanyaro anasakwa na polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwan mpambanaji, Nov 3, 2011.

 1. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Habari kutoka ndani ya polisi mkoani hapa zinasema wanamtafuta Nanyaro ambaye pia ni diwani wa Levolosi,kuhusiana na mgomo unaoendelea wa vifodi,wana taarifa kuwa huyu Kamanda wa BAVICHA ndio yupo nyuma ya sakata hili,kutokana na ushawishi wake mkubwa kwa siasa za Arusha.
  Pia wanachadema 25 kutoka kwenye eneo la December maarufu kama mtaa wa CHADEMA wanashikiliwa kituo kikuu cha polisi toka jana
   
 2. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwani mgomo unaendelea hata leo???
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  chadema arusha hawatarudi nyuma...
   
 4. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Polisi wanazo tabia za mbwa mwenye kichaa(kung'ata kila anachokiona)kukamata kamata watu hovyo hovyo bila sababu zozote za msingi.Kwa nini walienda kuwakamata makamanda Wa Chadema maeneo yao ya kazi?
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Watawakamata wangapi? Magereza zitatosha? Anyway, ngoja tuone! Wanaweza wakamkamata Nanyaro na kumweka ndani, ila fikra za mabadiliko ya kweli haziwezi kufungwa wala kuwekwa ndani!
   
 6. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,322
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  Polisi wa arusha wangeacha kazi yao nakujiunga kwene majukwaa ya siasa. Wameacha kazi yao ya kulinda raia na mali zao wanatetekeleza amri za viongozi wanaotetea ccm ili waendelea kulea vitambi vyao na kuhofia cdm kila kukicha.
   
 7. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa wa vifodi wanagoma bila ya sababu ya msingi. Sumatra wawafutie leseni wote waliogoma.
   
 8. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mbona unashuhudia kwa mbali?
  Waombee msaada toka Al Shabab na Al Kaeda
   
 9. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Polisi hawalindi maslahi ya ccm kwa sababu ni chama-dola, ila kwa sababu ndicho chama pekee kinachowahakikishia ulinzi kwa uchafu unaofanywa nao (polisi). Rejea uchafu kama tuhuma za rushwa, biashara haramu na za magendo zote ikiwa ni pamoja na madawa ya kulevya, vipodozi vilivyopigwa marufuku nchini, sukari, gongo, bange nk.
  Wanajua dhahiri kuwa cdm haitaruhusu kamwe upumbavu huu kutendeka ndio sababu ya wao kutumia nguvu kubwa kuidhoofhrha, lakini hawatashinda kamwe.
   
 10. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Duuh, huyu jamaa ndio anaendesha daladala zote hizo za Arusha. Polisi nao sometimes hawataki kufikiri kabisa.
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu Mzee, Arusha hakuna mgomo ni porojo tu za Pro-CDM JF
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Ajipeleke tu polisi akakutane na Lema, Jela huo ndio upambanaji unaotakiwa
   
 13. k

  king kong Senior Member

  #13
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna kurudi nyuma songa makamanda
   
 14. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nashauri IGP Said Mwema agombee Urais Kupitia Chama chake cha Police ambacho ni Ccm C" na Zuberi Agombee Ubunge Arusha kwa kupitia chama chao cha Police ambayo ni Ccm C"
   
 15. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,669
  Trophy Points: 280
  Kwani we hujui elimu zao?
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo Arusha bado kuna mgomo?
   
 17. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Kwa story niliyo ipata kuhusu hilii la Bwana Nanyaro Kutafutwa na Police hapo Arusha ni kuwa Police wana hisi kuwa Diwani huyo kuwa ndio muhusika mkuu wa Tukio la kugoma kwa Usafiri wa Daladala a.k.a Viford hapo arusha lakini Police hawana Ushahidi wa kutosha kama kweli Diwani huyo ndie muhusika mkuu bali wao wana hisi hivyo kwahiyo Police hufanya kazi pia kwa hisia ambazo pia huwapa kero wananchi wengi kwa ujumla nchi nzima Police najua fika waliwashika hao vijana wa December na kuwa weka ndani tena Police wao ndio walienda kuwakamatia maeneo yao ya kazi mchan kweupe kwa kuwashinikizia makosa kuwa walihusika na maandamano jamani hivi hawa police watupe sasa Ushahidi wa picha au CCTV camera kwa kile wanacho dai kilikuwa ni maandamano imekuwa sasa ni uonevu na kuvuruga amani ya wakazi wa Arusha na huko ndiko kutatoke vurugu kubwa sana hapa nchini na ikiongoza na mukali wa watu wa arusha mjini kisa siasa na chuki na hizi zote ni pandikizi za CCM kushindwa uchaguzi wa jimbo hilo na Kijana Lema ambao wao CCM wanadai kuwa ni kijan tuu hoi hae lakini wamesahau kuwa watu wengi wa Arusha wameisha ichoka CCM hilo ndilo tatizo ambalo viongozi wa serikali kisiasa wanalijua na huku wakifumbia macho kuwa hawalijui.

  My Take;

  Police ya Arusha Inaatarisha maisha ya wakazi wa arusha kuwa na ukosefu wa amani wao wakizani wanafanya kazi bora huku wanachafua kabisa Taifa letu katika ukurasa wa Democrasia ya vyama vingi kwa kukubali au kuwanyenyekea wakubwa wanao shikilia Dolla kwa kuwanyanyasa Raia wasio na hatia.

  Hilo Seke seke la Police na Raia au wanachama wa CDM hapo arusha kwa sisi ambao twazijua siasa za arusha ni Police kuwa watumwa na vibaraka kwa vigogo kwa kutii order flani ili kuhakikisha Upinzani usiwe na nguvu Arusha Mjini na hali halisi ni kuwa vijana wengi wako upinzani,

  Plice mwaacha kazi ya kukimbizana na raia tena wafanya biashara wakubwa wanao vuja sukari kwa magendo kwenda nchi jirani huko kwa tumia njia za Tarakea, Himo, Tarime kwenda kenya na Kagera kwenda Uganda,Rwanda Burundi Na kigoma kwenda Rwanda na Burundi hadi Congo. wao ni kukali akupambana na kitu maandamano huku mambo ya kuhujumu uchumi ukitambaa kwa kasi kwenye mipaka yetu ya tanzania na yakiibuliwa na wananchi hao hao na waandishi wa habari yet police wao wanakalia kujali au kijiingiza kwenye si a sa this is outrageous na udhaifu wa hali ya juu katika jeshi la police. Police wana tolewa same mwanga kwnda arusha kupambana na wana CDM badala ya kuwapeleka huko Tarakea au Himo hii inaingia akilini? au ni kuwapa uwoga wananchi wa hapo arusha.?? Majuzi hapa Naibu waziri wa viwanda Lazaro Nyarandu akihojiwa na Power Break Fast Cloud FM alikili kuwa kuna uhalamia wa kuvusha sukari mipakani na akasema huko kagera na ndiko ataanzia kwenda na kufuataia Tarakea na Himo police wetu hawajasema lolote hata kutoa taarifa kwa UMMA kuwa inawataadharisha wale wote wafanya biashara za magendo kuvusha sukali kwa kuwapa tamko kali basi hawajafanya ila vya maandamano wanaweza kudhibiti na hiyo intelligensia yao kwanini isiwasaidie huko kwa wavusha sukari? Kwani ni wazi kuwa Nao Police wana husika kwa kiasi fulani kuvusha sukali nje ya mipaka ya nchi yetu

  Police hawajaja na kutupa live wao kwanini saaaana wao wamejikita sana na kupambana na upinzani esp pale raia wanadai haki zao Police wamekua makaburu wa viongozi makaburu weusi wa nchi hii tena?

  At the End unakuta sasa wananchi wengine wanarubuniwa na kuulizwa huyo mbunge wenu kawafanyia nini mpaka sasa hivi tusiwe wajinga au mbumbu hivi maendeleo ya Jimbo fulani yana letwa tuuu basi na mbunge kwa pesa yake mfukoni au Ni budget ya serikali inavyo panga ili mfuko huo uzisambaze fedha husika katika hayo majimbo kwa ajiri ya maendeleo na Mbunge kazi yake ni kufuatilia fungu hilo kutoka na kwenda jimboni kwake na kusimamia shughuri zote kuhakikisha mandeleo ya jimbo hilo kupatikana na kubuni njia zingine za maendeleo katka jimbo lake ili apate fungu lingine. sasa kama serikali inachelewesha kwamfano utataka kumuliza mbunge tena nini kimefanyika ? Mwajua serikali ya CCM sio wajinga wao wanajua fika wamekosa majimbo fulani muhimu ambayo yako kwa upinzani kweli maendeleo katika maendeo hayo yatakuwa kwa kasi kama kwa majimbo mengine waliyo yadhibiti wao CCM??

  Nyakati hizi ni nyakati za kupambana na Urasimu wa nchi hii kuto kutupoa haki zetu na kuwa kila kukicha wanasifia nchi yetu ni ya Amani kweli amani bila Haki wananchi wengi wamekuwa na kasumba ya kusema basi ipo siku jamani ipo siku hiyo yaja lini inatubidi tusimame kidete kuitaka haki yetu ya kimsingi ya kuhoji kwanini hiki kiko hivi na hiki kiko vile na tupate majibu na yote haya ni sisi wananchi kutoshupalia kuijua katiba na kupambana kuitaka katiba inayo tushirikisha sisi sote hapo ndipo serikali itautambua uwpo wetu lasivyo tutabakia kuwa watumwa wa vigogo wachache katika nchi hii. Kuifanini nchi yako ni kudai HAKI yako
   
 18. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Tunavyosikia kuwa mgomo haupo tena,

  Tatizo la Arusha ni kubwa sana na si tu hata kwa wana siasa. kwa mtu aliye wahi ishi huko arusha nadhani atakubaliana nami kuwa Police wa arusha utendaji kazi wao kweli unashaka kubwa sana kwani police wa Arusha nilivyo wajua nikuwa wao nao ni wafanya bishara wanajihusisha sana na jamii kwa shughuri nyingi tu ambalo hatukatai kama mikoa mingine ilivyo ila Police wanacho kosea kabisa ni kuto kutenganisha Kazi za Police na Kazi zao Binafsi huko Uraiani, Police wengi wao ni wamiliki wa Daladala, bisahara za Taxi na wauza magari na wengine wako kwenye Mirungi na ni walaji wakubwa hebu uliza mtaa wa Mtakuja sukuma rufiji Uhuru rumumba -Mwanza huko Arusha maeneo ya Msikiti wa bondeni ni biashara za mirungi hutembea furuuuuuu, Hili Police wanarijua lakini mmmh wao hawalichukulii serious kabisa.
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hakuna mgomo wala nini. Mbwembwe tu hizo
   
 20. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  hizo porojo wanafanya kwa ajili ya nani sasa.
   
Loading...