Mwenye Uwezo awaeleze Wazanzibar hili

Mwenye Uwezo awaeleze Wazanzibar hili

Mpaka karume anauwawa mwaka 1972 Zanzibar haikuwa na Katiba. Karume alikuwa natawala kwa amri 'presidential decrees'. Katiba ya Uhuru ya 1963 ilfutwa baada ya Mapinduzi. Katiba ya kwanza rasmi ya Zanzibar ilitungwa mwaka 1984. Kwa hiyo Karume hakurekebisha Katiba ya Zanzibar. Tusipotoshane.

Inawezekana unayoyasema ni kweli mkuu,lakini mawazo yangu mungano ni nchi mbili zilizoungana yaani tanganyika na Zanzibar,kama zanzibar ilifuta katiba yake 1963 wakati mapinduzi bado hayajafanyika na ikatengeneza katiba yake 1984 ilikuwa na uwezo wa kuirekebisha katiba waliyoitengeza kutokana na maslahi ya zanzibar na watu wake....

Kama serikali ya mungamo wameliona hilo la zanzibar kurekebisha katiba yake ni makosa kwanini wakaliacha lifanyike.....
 
Kwa mujibu wa Hati ya Muungano Katiba ni kati ya mambo 11 ya awali yaliyokubaliwa kuwa ya Muungano. Kwa hiyo Zanzibar haina mamlaka kikatiba ya kufanya lolote kuhusu hayo mambo 11. Ni Bunge la Jamhuri ya Muungano linaloweza kubadili katiba kuyaongeza au kuyapunguza.

Kaka,Katika urekebishwaji wa katiba ya zanzibar hayakuyagusa hayo mambo 11 ambayo waasisi wa mungano walikubaliana yawee ya mungano,je unajua kuwa hayo mambo 11 ya mungano yamefikia 21....

Katiba ya Zanzibar imerekebishwa lakini bado tunasikia malalamiko ya kero za mungano....CCM imekula kwao hizi zinazoitwa kero za mungano walikuwa na uwezo wa kuzirekebisha muda mwinigi kabla hayajafikia haya,lakini kutokana na uroho wa madaraka wa chama tawala ndio maana tumefikia hapa

Hii ngoma hairudi nyuma wananchi wamesha amka siku hizi dunia imekuwa ndogo,kuna internet utawazi umekuwa mkubwa hakuna cha kuficha.....
 
Mpaka karume anauwawa mwaka 1972 Zanzibar haikuwa na Katiba. Karume alikuwa natawala kwa amri 'presidential decrees'. Katiba ya Uhuru ya 1963 ilfutwa baada ya Mapinduzi. Katiba ya kwanza rasmi ya Zanzibar ilitungwa mwaka 1984. Kwa hiyo Karume hakurekebisha Katiba ya Zanzibar. Tusipotoshane.

Marais Karume wapo wawili Karume sr na Karume jr
 
Unamawazo za kikoloni kweli eti halafu munajitia kuuita muungano.

huu ni ukoloni wa tanganyka kw znz na tutaupinga kw nguvu zetu zote.

kwa hyo kwa akili yako unajua kwmb Tanganyika inawatawala Znz..basi kazi ipo km ndo mnavyodhan
 
Muungano wa serikali moja inaamana uko tayari kupoteza TANGANYIKA yako? Na Kwanin ukatae TANGANYIKA yako?

Nilikuwa namwelewesha huyo mdau Mtabe kwamba muungano wa vitu viwili huzaa kimoja na si viwili tena. Na kwa kuwa hawataki hivyo, let them go.
 
Last edited by a moderator:
Pengine hujaelewa nikuulize KATIBA IPI NI BATILI KWA WENGINE? maana Zanzibar wana katiba yao inayowapa mamlaka ya kujiwekea mambo yao likiwemo hilo la maamuzi ya kuwa nchi au si nchi hivyo ndivyo walivyoamua na ndio maana tokea awali baada ya muungano Zanzibar ipo TANGANYIKA NDIO IMEPOTEA au hujuwi? Sasa KATIBA IPI INA UHALALI KWA WAZANZIBARI? unavyoona wewe UNAJALI ILE YA JAMUHURI TU UMESAHAU ILE YA ZANZIBAR? MWAKA HUU KILA MWENYE SUBIANI WA KITANGANYIKA(SAMAHANI) UVUMBA NA UBANI ULIOTIWA UTAMUATHIRI KWA KWA KUANZA KUPIGA MAYOWE NA KUWEWESEKA..... MARA KATIBA YA Tanzania IMEVUNJWA NA ILE YA ZANZIBAR, kIKWETE KARUHUSU kuvunjwa katiba N.K. NASEMA TENA LAZIMA Tanganyika IJE JUU IKAE NA MSHIRIKA MWENZAKE WAPANGE MUSTAKBALI WA UBIA WAO ( MUUNGANO) vitisho havisaidii. Na kumbuka tayari serikali mbili zimefeli kitambo( miaka 50) iliyopita. Tujiulize hivi kweli tunataka muungano kweli au tunataka malumbano ? kwa sasa TATU NDIO MPANGO MZIMA. MOJA HAIWEZEKANI NA MBILI HAZIVUMILIKI.

Ka.a kwa miaka hamsini haikuwezekana kukaa na kupanga, itawezekana leo? Zanzibar imebalehe, inataka kuanza maisha yake. ONDOKENI, mtuache na Tanganyika yetu. Then majuto ni mjukuu.....
 
Kama Zanzibar sio nchi sasa Tanganyika imeungana na nini,,,,

Mkuu napenda Kurudia,,,Zanzibar wamerekebisha katiba yao,kila siku tunasikia malalamiko ya mungano pande zote mbili kwanini hizi kero hazikurekebishwa na chama na serikali inayotawala....mpaka imefikia hapa.

Katiba sio msahafu wala Biblia,Kutokana na mungano tuliokuwa nao Zanzibar ina uwezo wa kurekebisha katika yake kwani mambo ya ndani ya zanzibar sio ya muungano
Zanzibar ilisita kuwa nchi pale iliposalimisha mamlaka yake ya ki-dola kwa Tanganyika na kiti chake katika umoja wa mataifa kikaondolewa kabisa! Zanzibar ilibakiziwa mamlaka ya kijimbo; yaani kufanya chaguzi zake za ndani, mambo ya kugawa ardhi, kusimamia wavuvi nk! Mamlaka ya kusimamia usalama wa raia, ulinzi, mambo ya nje, fedha, kugawa mipaka ya mikoa nk yalipewa Tanganyika! Kumbuka jina Tanzania lilikuja miezi kadhaa baada ya Zanzibar kujisalimisha Tanganyika!

Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, Zanzibar imefanya uhaini au kwa maneno mengine imeasi!

Chama tawala hakikushindwa kurekebisha kero, bali kilichukua mkakati hafifu! Kwanza kwa kuifuta ASP- chama kilichokuwa kinaongoza Zanzibar kwa kukiunganisha na TANU kuunda CCM na pili taratibu kilikuwa kinapunguza mambo ambayo Zanzibar ilikuwa inajisimamia na kuyaongeza katika muungano; kwa maneno mengine kuyaweka chini ya udhibiti wa Tanganyika a.k.a. Tanzania.

Kuhusu kwamba katiba siyo msaafu wala biblia ni kweli ndiyo sababu JK aliruhusu Zanzibar kuanza na kufanya mchakato wa kubadlisha katiba!! Kinyume na matarajio ya JK na Watanganyika wengi Zanzibar ikavuka mipaka na kutengeneza katiba ya KIHAINI na kujitangaza kuwa nchi!

Narudia kusema kitendo hiki hakivumiliki na Watanganyika hawako tayari kuona kinaendelea!!
 
Kelele wee Nyang'au...mmekua mkichua Fedha kwa muda wote halau eti mnatuita kupe...wdhulumifu wakubwa!
 
sio mikakati hafifu...Ni mikakati pole pole ili Tangaznyika iendelee kuibia znz...
 
Muungano wa serikali moja inaamana uko tayari kupoteza TANGANYIKA yako? Na Kwanin ukatae TANGANYIKA yako?

Ukiitwa mtanganyika kipato chako kitaongezeka? Hospitali dawa zitapatikana kwa sababu tu kuna tanganyika? yani issue ni nini kwani hapo?
 
Zanzibar ilisita kuwa nchi pale iliposalimisha mamlaka yake ya ki-dola kwa Tanganyika na kiti chake katika umoja wa mataifa kikaondolewa kabisa! Zanzibar ilibakiziwa mamlaka ya kijimbo; yaani kufanya chaguzi zake za ndani, mambo ya kugawa ardhi, kusimamia wavuvi nk! Mamlaka ya kusimamia usalama wa raia, ulinzi, mambo ya nje, fedha, kugawa mipaka ya mikoa nk yalipewa Tanganyika! Kumbuka jina Tanzania lilikuja miezi kadhaa baada ya Zanzibar kujisalimisha Tanganyika!

Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, Zanzibar imefanya uhaini au kwa maneno mengine imeasi!

Chama tawala hakikushindwa kurekebisha kero, bali kilichukua mkakati hafifu! Kwanza kwa kuifuta ASP- chama kilichokuwa kinaongoza Zanzibar kwa kukiunganisha na TANU kuunda CCM na pili taratibu kilikuwa kinapunguza mambo ambayo Zanzibar ilikuwa inajisimamia na kuyaongeza katika muungano; kwa maneno mengine kuyaweka chini ya udhibiti wa Tanganyika a.k.a. Tanzania.

Kuhusu kwamba katiba siyo msaafu wala biblia ni kweli ndiyo sababu JK aliruhusu Zanzibar kuanza na kufanya mchakato wa kubadlisha katiba!! Kinyume na matarajio ya JK na Watanganyika wengi Zanzibar ikavuka mipaka na kutengeneza katiba ya KIHAINI na kujitangaza kuwa nchi!

Narudia kusema kitendo hiki hakivumiliki na Watanganyika hawako tayari kuona kinaendelea!!

Haahahaha imekula kwenu,watanganyika wa leo sio wa jana,watanganyika walio wengi na wao wanataka taifa lao 😉
 
Ukiitwa mtanganyika kipato chako kitaongezeka? Hospitali dawa zitapatikana kwa sababu tu kuna tanganyika? yani issue ni nini kwani hapo?
Issue ni Kwanin watanzania bara walio wengi HAWAITAKI TANGANYIKA? Sio Suala la kuongezeka kipato wala dawa kugaiwa hospitali.KWANIN HAWAITAKI TANGANYIKA?. Wazanzibari hawanwagiwi dawa wala hajaongezewa kipato Kama unachokitaka ww kuongezeke kwasababu eti mtanganyika Lakin wanajinadi na kujisifia Kama wao ni Wazanzibari.
 
Kwa nini wewe unaitaka tanganyika?
 
Kwa nini wewe unaitaka tanganyika?

Sana sababu najua ikifika TANGANYIKA basi zanzibar nayo itakua imewasili.najua ww hutaki mpaka uwe na uhakika wa kuongezeka kwa kipato!!!
 
Sana sababu najua ikifika TANGANYIKA basi zanzibar nayo itakua imewasili.najua ww hutaki mpaka uwe na uhakika wa kuongezeka kwa kipato!!!

Ninachotaka mimi ni maisha yangu yaimarike, kama serikali 10 zitasaidia hilo fine, kama 1, au 2 au 3 vyovyote vile sawa tu i dont care.
 
Bila kumung'unya maneno vifungu hivi vya katiba ya Zanzibar vimekiuka katiba ya muungano na ni vya kihaini! Hivyo kwa mamlaka ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anatakiwa kuifuta katiba hii na kuwafungulia mashtaka ya kihaini wote waliohusika katika kuiandaa katiba ya Zanzibar!

mwambie hyo raisi wako ajaribu tu aone mziki wa wazenji kama hamtujui ndo mtajua mara hii mnajitoa fahamu kama vile hii Zanzibar ilikua koloni lenu vile, wekeni heshima Zanzibar ni nchi huru kabla hata Tanganyika. pam bav zenu hadi hasira kwa u jing a wenu
 
Back
Top Bottom